Nitaendelea kuwajuza ndugu zangu kuhusu Norway

Nitaendelea kuwajuza ndugu zangu kuhusu Norway

Per Diem

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2018
Posts
2,189
Reaction score
3,724
Ni miezi imepita kidogo toka niwe nawajuza kuhusu Norway, hii ni kutokana na nilikuwa nasoma short course ya mambo ya Ship Surveying, nashukuru nimemaliza.

Kazi za bandari ndio nyingi huku, hivyo ilinibidi kujiongeza ili kujiweka sehemu nzuri zaidi na sio kila mara kuwa kibarua.

Japo najua bado changamoto itakuwepo kuaminiwa kupata kazi ambayo ni skilled Ila nipo hapa kupambana.

Nimekuta pia Message nyingi sana inbox kutoka kwa watu wengi tu, na wote wakiniuliza jinsi ya kufika huku.

Nawaomba sana ndugu zangu mnielewe, toka mwanzo nilisema sina connection yoyote ya kumfanya mtu afike huku.
Ila kama upo huku au ukabahatika kufika huku basi nitaweza kukupatia connection ya kazi lakini za unskilled tu tena hizi za bandarini na sio vinginevyo.

Hivyo nawaomba tena nirudie sina connection yoyote ya mtu kuingia huku Norway, naweka hapa wazi ili na wengine waelewe kuliko ningeanza kumjibu mmoja mmoja.
 
Bora umefunguka hata ukimpiga mtu atakuwa kataka mwenyewe
 
Mm nipo Ureno ila nafagia maofic ya watu nakufanya usafi mashuleni, na pia nshapataga nafac ya kufanya usafi kwenye uwanja wa sport lzborn mwaka mmojaa, ukijutuma nakujua nn unatakaaa utafanikiwaa ukiletaa ubisho unafeli.
 
Back
Top Bottom