Nitaepukaje hali ya kujisikia mchovu baada ya kula?

Nitaepukaje hali ya kujisikia mchovu baada ya kula?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Hiyo hali imeshakuwa kero sasa!

Mara nyingi, nikishakula tu, najisikia uchovu kiasi cha kutamani kulala, hata kama ni Mchana. Haijalishi kama nimekula chakula kidogo tu, nitajisikia tu kulala.

Kuna jinsi ya kuiepuka hiyo changamoto?

Asanteni!
 
Tatizo unakula carbohydrate. End product ya carbohydrate ni alcohol inayokulewesha na kujikuta umechoka. Ilinitesa sana kipindi nipo A level. Cha msingi ukijiskia kulala usilale
 
Kula matunda kwa wingi na upunguze vyakula vya wanga
Shukran sana mkuu. Unanishauri nitumie matunda gani hasa?

Nataka nijiwekee kama wiki moja ya kula matunda tu kuanzia Asubuhi mpaka Usiku ili nione mwitikio wake. Sitakula chakula kingine chochote zaidi ya matunda. Matunda gani niyape kipaumbele?

Kwa niliko, matunda yanayopatikana kirahisi kwa sasa ni ndizi mbivu, maembe, parachichi, tikiti maji, matango, na tende.

Tende huwa haikosekani kwangu.
 
Tatizo unakula carbohydrate. End product ya carbohydrate ni alcohol inayokulewesha na kujikuta umechoka. Ilinitesa sana kipindi nipo A level. Cha msingi ukijiskia kulala usilale
Pengine mkuu! Nakumbuka na mimi hiyo changamoto ilinianza nilipokuwa "A" Level, miaka mingi iliyopita. Lakini sasa nashangaa siku hizi hata nikiamua kutokula Usiku chakula kilichopikwa, badala yake nikaamua kula matunda tu au juisi, bado hiyo hali ya kujihisi uchovu inanijia. Sijui ni hali ya kisaikolojia, kwamba pengine mwili umeshakariri kuwa nikila Usiku kinachofuatia ni kusinzia?

Lakini nashukuru mkuu. Nitakuwa nikienda kinyume na hiyo hali. Sitalala kama sitaki kulala hata kama nitajisikia kulala. Na hilo ninalianza rasmi leo. Leo ratiba yangu ni ya kukesha kwa ajili ya jambo fulani. Nitapumzika Asubuhi.

Nashukuru sana🙏🙏🙏
 
Hiyo hali imeshakuwa kero sasa!

Mara nyingi, nikishakula tu, najisikia uchovu kiasi cha kutamani kulala, hata kama ni Mchana. Haijalishi kama nimekula chakula kidogo tu, nitajisikia tu kulala.

Kuna jinsi ya kuiepuka hiyo changamoto?

Asanteni!
Ukimaliza kula tembea tembea usikae sehemu moja.. Na kama unakunywa maji baada tu ya kumaliza kula acha, subiri mpaka 30dk au zaidi
 
Shukran sana mkuu. Unanishauri nitumie matunda gani hasa?

Nataka nijiwekee kama wiki moja ya kula matunda tu kuanzia Asubuhi mpaka Usiku ili nione mwitikio wake. Sitakula chakula kingine chochote zaidi ya matunda. Matunda gani niyape kipaumbele?

Kwa niliko, matunda yanayopatikana kirahisi kwa sasa ni ndizi mbivu, maembe, parachichi, tikiti maji, matango, na tende.

Tende huwa haikosekani kwangu.
Achana na tende kula parachichi na matango zaidi na vinywaji vitamu na soda acha kbs pia mfatilie Dr boaz mkumbo YouTube atakufungua zaidi kiakili
 
Side effects za kula viporo mkuu
Kwa hapo utakuwa umenisingizia mkuu! Labda kama ni vile nilivyokula kipindi nikiwa shule ya Msingi. Kipindi hicho ilikuwa ni kawaida kula hata kiporo cha ugali maharage Asubuhi Kabla ya kwenda shuleni.
 
Back
Top Bottom