Nitafuta soko la vifaa vya hospital ninazo machine zote.

Nitafuta soko la vifaa vya hospital ninazo machine zote.

damcon

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
214
Reaction score
72
wakuu nina machine zote X ray,ultra sound,microscope,za kupima kansa,kupima moyo,vitanda vya surgery,kupima ubongo,kuzalisha,hospita uniform vyote ni from uk etc natafuta mteja +255652715232.
 
Mkuu ulikuwa na hospitali? Kwanini tusishirikiane kufungua hospital?
wakuu nina machine zote X ray,ultra sound,microscope,za kupima kansa,kupima moyo,vitanda vya surgery,kupima ubongo,kuzalisha,hospita uniform vyote ni from uk etc natafuta mteja +255652715232.
 
bro tafuta madaktari wawili na nesi na secretary thn unaanzsha hosptal brother,trust me yan u will make it so fast
 
Ukitaka jengo linalofaa kwa hospitali lipo.
 
wakuu nina machine zote X ray,ultra sound,microscope,za kupima kansa,kupima moyo,vitanda vya surgery,kupima ubongo,kuzalisha,hospita uniform vyote ni from uk etc natafuta mteja +255652715232.

damcon hii field nadhani huijui vizuri. Naona uandishi wako. Vifaa vya kupima kansa, kupima ubongo. Ninaamini hujaleta kabisa hivyo vifaa ila wataka watu watoe order then uagize; kwani kama ushaagiza bila kujua soko kuna vifaa utakaa navyo daima. Pia naamini hivyo vifaa ni used. Hospitali nyingi huwa haziwezi kununua vifaa vipya kwa sababu ya bei. Usilete mzigo wowote, hususani ya gharama kubwa bila kufanya survey. Kuna vifaa waweza leta; lakini vinahitaji consumables ambazo supply yake haitakiwi kukatika. Sasa watu wakiona consumables si za uhakika au ni ghali; katu hawanunui. Hapa ni sawa na Printers za HP kutumia wino wa HP.
Nakushauri mtafute daktari yoyote anaye practice awe anakushauri soko la biashara lako. Ikiwezekana wasiliana na private clinics. Uliza wanavyohitaji. Kama waweza tafuta mfanyakazi sehemu kama Anudha; ambao ni gurus wa kuuza vifaa vya tiba anaweza akakupa tips.
Umeshauriwa kuanzisha hospitali. Ni mradi mzuri wa muda mrefu. Lakini hailipi haraka kama watu wafikiriavyo. Ukiacha gharama za vifaa, bado kuna ujenzi au renovations na pia staffs. Hospitali yaweza anza leta matokeo mazuri at least miaka miwili baada ya kufungua; na tena itategemea na sehemu ilipo pamoja na sifa za madaktari waliopo. Pia watanzania walishazoea kupewa afya bure; sasa ndio wanajifunza kujihudumia kwa suala la afya. Hivyo wako sensitive sana; hususani mikoani.
Mwisho; hata kama waagiza vifaa usisahau kuleta vifaa vinavyoendana na teknolojia ya sasa. Unakuta mtu analeta vifaa ambavyo viko obsolete. Inakuwa hasara. Kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom