Angekua na "uelewa" japo Mdogo angeshauri tuhamie Zambia na sio Burundi. Zambia Raisi ni Mtumishi wa Wananchi, ni mnyenyekevu, amezuia matumizi ya magari ya kifahari kwa Mawaziri (Wakati yeye ana latest Toyota v8), Rais wa Zambia amegoma Katu kupongezwa na kuwakumbusha Watu wake kuwa anayoyafanya ni Wajibu wake na sio fadhila kama Mwigulu na Wenzie akina Nape wanavyotuaminisha.
Leo hii nchi nzima imejaa mabango ya kumsifia na kumpongeza Mtu mmoja, as if halipwi, as if ni msamaria mwema tu, tumejengwa kuaminishwa hivyo na wapuuzi Wachache wanaamini hivyo.
Mimi nitaenda Zambia ambako Pesa ya nchi Yao inazidi kuwa stable dhidi ya US Dollar, nchi ambayo Kuna kuaminiana na Rais hahitaji ulinzi wa mabilioni kujilinda......