OmaryElias
Member
- May 3, 2023
- 11
- 34
Sijui nimemkosea nin mwenyezi Mungu mimi kama kuna kosa napiga magoti natoa chozi mbele yako nisamehe nitoe kwenye haya mateso.
Natoa historia yangu fupi, sina elimu ya uandishi maana elimu yangu ya shuleni ni ndogo.
Kwa majina yangu ni Juma Elias Chacha, ni mwenyeji wa Tarime Bomani ndo nyumbani kwa baba mama yangu. Ni mwenyeji wa Singida Nkalakala Wilaya ya Makalama.
Mimi ndio mtoto wa kwanza anafuata mdogo wangu, mimi na mdogo wangu hatukuweza kupata malezi ya mama, mama alituacha baada ya kukosana na baba, baadae baba aliondoka akatuacha nyumbani akaenda mgodi wa Buhemba (Ilasaniro) tukawa tunaishi pale nyumbani mimi, mdogo wangu na bibi.
Maisha yalikua ni magumu sana, baba alikua anatuma hela kwa mbinde. Maisha yanasonga huku nasoma, nikamaliza elimu ya msingi ile nataka kuingia kidato cha kwanza nikapat matatizo ya kiafya ya uvimbe tumboni.
Tukazunguka mahospitali kupata tiba mwishoe nikapata nafuu, niliporudi sikuweza kuendelea na elimu ya sec nikawa nipo nyumban. Jamani mtanisamehe simu yangu ni ndogo haina uwezo wa kubeba maneno yote.