SoC01 Nitaishije Maisha Yenye Faida

SoC01 Nitaishije Maisha Yenye Faida

Stories of Change - 2021 Competition

Genius jack

New Member
Joined
Aug 28, 2021
Posts
4
Reaction score
42
Hivi ulishajiuliza kwanini upo hai mpaka leo?

Hili ni swali gumu sana lakini sio kila mmoja anaweza kutoa majibu sahihi, kwa ufasaha wa swali hili ni lazima mtu awe alishajiuliza ni kwanini kwanza anaishi. Ndipo aje ajiulize juu ya ukomo wa maisha.
Lazima tukubali hakuna kitu kinaweza kutokea chenyewe hivyo ni lazima kuna aliyevifanya na anayevishikilia, Ni mjinga tu anaweza kuamini Mungu hayupo na anayefikiri ametokea tu.

Tukubali au tukatae ni lazima kila mmoja ajue kuna siku hatakwepo Duniani haijalishi ana nguvu kiasi gani umaarufu au fedha kiasi gani.
Sasa nini cha kujua unapojiuliza kwann upo hai hadi leo.

Tambua ni Neema ya Mungu inakufanya uwe hai hata leo.
Hapa utagundua ugonjwa uliowauwa wengine sisi bado tupo hai sio kwa sababu tunajua kujilinda sana au niwajanja sana hapana Bali kuna kustahili pasipo stahili yaani ndiyo neema hiyo, neema ndio inatupa akili na maarifa ya kuwa waangalifu na Ndio inatushikilia juu ya tahadhari zote tunazozichukua.

Alexander the Great mmoja wafalme wenye nguvu sana kuwahi kutokea alipokuwa anapambaniwa kuwa uhai akiwa anaumwa alitoa maagizo matatu kwa waliokuwa wanamhudumia.

Agizo 1. Aliwaambia Nikifa jeneza langu libebwe na madaktari hawa akimaanisha wakati wako unapofika hata madaktari hawawezi kukusaidia kuishi tena teknolojia na ujuzi vina mwisho wake.

Agizo 2. Wamwage dhahabu na fedha kuelekea kwenye kaburi lake akimaanisha fedha na Mali hazikuweza kumsaidia wakati wake ulipofika.

Agizo 3. Azikwe amefungua mikono akionyesha ulimwengu hajaondoka na kitu duniani alizaliwa hana kitu na anaondoka hana kitu.

Kwanini nataka utafakari hili ni sababu nataka ujue haya maisha yana mwisho wake hivyo inampasa mtu uweke bidii kama utaishi milele na ujiandae kama unaondoka Kesho, Tunapaswa kuishi haya maisha kama hata ukijua ni lini unaondoka hutataka kubadilisha chochote utaishi vilele maana unaishi sawa.

Ukishajua Ni rehema na fadhili
za Mungu Wala sio ujanja wetu tunapumua leo hii ni Mungu ametupa Nafasi hiyo tuishi maisha yenye amani na furaha.

Haya ni machache ya kuzingatia unapoishi ili maisha yako yawe na faida.

1. Usionee wengine.
Watu huwaonea wale ambao wanajua hawana watetezi au mayatima au yeyote asiye na nguvu na kutengeneza majeraha makubwa kwa wengine si sawa kuonea au kudhulumu kitu cha mwingine. (Iwe ni mapenzi, fedha, cheo usidhulumu haki ya mtu)

2. Ishi kwa upendo na kusaidia wengine.
Upendo ni zaidi ya kutoa kitu kwa wengine upendo unaenda mbali kuangalia hata kusudi la kufanya jambo na kile unachotegemea ukipate kwa unachokifanya.
Usifanye vitu kutafuta Sifa na ili uonekane na watu, Fanya kwa siri na upendo Mungu ndie anayekutazama na atakubariki.

3. Usiwe na majivuno.
inakupasa kutokuwa na majivuno sababu hujui yanayoweza kutokea kesho, unaweza ukawa na Mali zako na ukajiona umefanikisha tayari ghafla yanatokea mafuriko au majanga ya moto na kuharibu ulivyovitegemea, Hivyo tunapaswa kuwa na maisha yaliyojaa unyenyekevu.

4. Samehe wanaokukosea.
Tuwe na rehema na msamaha katika maisha unakuwa umefanikiwa sana kama unaweza kumsamehe mtu anapokukosea haijalishi unaona amekosa vipi, unapozidi kushikilia jambo ndivyo unavyojitesa wewe zaidi na kuumiza moyo wako.

Hitimisho: Kwa machache haya Amua siku zilizobakia uishi maisha ambayo hutajutia mwisho unapofika ishi maisha ambayo hautatamani upewe nafasi nyingine mwisho unapofika maana umeridhika kwa siku ulizopewa kuishi.

#Ipigie kura Post hii ni Upendo tu.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom