Nitajie beki bora wa kati kwasasa anayemzidi Ruben Dias wa Man City

Nitajie beki bora wa kati kwasasa anayemzidi Ruben Dias wa Man City

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kwasasa huyu ndio beki bora wa kati sio kwa ulaya bali duniani kwa mtazamo wangu. Beki mwenye matumizi makubwa sana ya akili, anajua kujipanga kwenye nafasi kwa muda sahihi, anafanya sana interception, rejea mechi ya jana ya Man City dhidi ya PSG.

Amewafanya hata mabeki wenzake wa Man City akina John Stones na Laporte warudi kwenye viwango vyao. Guardiola alifanya usajili sahihi sana hapa, na kwakuwa hakusajiliwa kwa mbwembwe, basi pia anafanya kazi yake kimyakimya.

Nitajie beki wa kati aliyebora kwasasa kumzidi Ruben Dias, karibuni kwa mjadala...
IMG_8087.jpg

IMG_8086.jpg
 
Mbape alikuwa hayuko kwenye fom
Ngoja second leg tuone
 
Back
Top Bottom