Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Mimi wa kiume 24_04 jina S
Yeye 08_04 jina V
Hapa geuza kinyume maelekezo yake ndio yako na yako ndio yake
Punda na Ng'ombe



Mahusiano haya ni mshike mshike baina ya mbingu na ardhi au magharibi na mashariki na haijulikani hadi leo ni nini kina waunganisha,

Kipo kinacho waunganisha tofauti na mapenzi ya dhati mara nyingi hata mimba hutokea bila kujipanga,

Mtizamo:

Nyote wawili ni wenye hisia lakini wewe ni mwenye kuwa annoyed na makusudi yake ya ufanyaji mapenzi.

Yeye ni mtu wa kupenda kukaa nyumbani jina lake la utani kiroho ni manyama uzembe yani mvivu na wengi wao huwa ni wenye usafi wa nje tu.

Wakati wewe ni tofauti na yeye, wewe ni mwenye mihemko na msukumo wa kutoka na kupenda mambo mapya na ya sasa hivi sasa hivi bila kuchelewa na pia kupenda uhuru bila kubanwa banwa.

Yeye ni mwenye wivu mkali na pia ana husda ya chini chini na hutaka mambo yaende jinsi anavyotaka yeye na mambo yake ni mwenye kupenda mwenyewe jinsi ya kufanya mambo anavyotaka na hujiweka kwenye kivuli cha dini na hujifanya wanaroho safi lakini hamna kitu hawa ni sawa na kuishi na mafia bila kujua. Na anapokuwa na wewe mwenye msimamo hukuona kama vile ni mbishi na kiburi husikii ya wengine hali ya kuwa yeye ndio mwenye kiburi na gubu,

Japo kuwa yeye ana bahati sana ya kutengeneza pesa. Lakini wewe ni mzuri katika kuponda pesa, Ukipata pesa matumizi yako ni ya hali ya juu sana, zinayayuka kama moto na pale zinapoisha roho yako ndio hutulia.

Safari ndefu ya mapenzi inaweza kuwa ngumu kwenu kwenda, ingawa mkiishi sana itafikia sehemu utapenda style yake ya matumizi na kujinyima ili kufanikisha maswala ya nyumbani.

Source:
Rakims
 
Male: 20 November
Female: 4 February
Mahusiano haya ni baina ya maji ya moto na upepo wa kimbunga hii ni fahari wawili hawakai zizi moja na pia hawa ni wagomvi wawili walio kubaliana kila mmoja akae upande wake wa dunia,

Mahusiano yenu yapo hivi:

Wewe utakuta ni mwenye kuwa na matakwa mazito ya kihisia, lakini yeye hata kuruka nae mara moja sio jambo zito kwake kwa upande wako yaani kumvulia nguo kwako yeye kwake ni jambo la kawaida wala halina uzito wowote katika hisia zake, kwake yeye wewe kukutana nae kimwili ni kama tu kupanua upeo wake wa yeye kukujua zaidi wala sio jambo la ajabu na kumfanya ajihisi yupo kwenye serious relationship.

Wewe ni mtu ambaye hutaweza kuvumilia jinsi yeye atakavyo kuwa anachukulia mapenzi yako kirahisi rahisi.

na kila mara unaweza kuwa na hisia kwamba hayupo serious na wewe isipokuwa ni part time tu.

Yeye binafsi ni mtu ambaye ni mwenye kuvutiwa zaidi na vya nje hata hivyo vya nje akiingiza ndani bado atavutiwa na vya nje tu hata ukiwa kwenye ndoa nae huyu hashindwi siku moja kukwambia umalaya upo kwenye damu you deal with it or leave it.

Japo akimpata anaemmudu kinyota huwa mpole kama kondoo.

Kitu ambacho wewe kitakutia wivu wa ajabu na vile una asili ya wivu, basi utataka kujaribu kumtawala na utakuta kila mara anakuvuruga jinsi anavyopenda uhuru na alivyo na mood za kuswing basi safari yenu itakuwa ngumu.

Wewe utakuta ni mwenye kupenda kuwa nyumbani na yeye utakuta ni mwenye kupenda uhuru wa kuendelea hadi mwisho kila mtu atashika njia yake.

Mkilazimisha nyie ni mtu na jamaa yake wasioelewana wanaochangia nyumba kulipia kodi.

Rakims
 
Me : 22 February
Herufi ya mwanzo F

Ke: 25 September
Herufi ya mwanzo
Wewe ni mwenye tabia za Maji yaliyotulia na yeye ni Upepo wa juu hivyo kwa mfuatano huu wa mahusiano hamuendani na mtaacha labda uwe mtumwa wake nayo utavumilia kwa muda kisha yatakushinda utatafuta pengine
Japokuwa ni watu mnapendezana mkiwa pamoja,wabunifu na mapenzi yenu yanaweza kujaa kujidanganya, Nyinyi ni watu ambao mkikutana mnaweza kuingia haraka sana kwenye mapenzi na yakawa moto lakini ni short fuse.
Wewe (Pisces) unategemewa kuwa ni mtu mwenye kupenda kusaidiwa kihisia katika mapenzi na ni mtu mpole na mkimya mwenye upepo kwa watu tofauti tofauti, lakini hutapata kujaliwa kihisia kwake kwa maana yeye hupenda mapenzi ya kujirusha na ya kukimbia kimbia.
Japo anaweza kukuigizia ni mtulivu, lakini ukweli ni kwamba yeye (Libra) ni mtu ambaye hata kuvumilia muda mrefu anaweza kukukimbia labda utumie nguvu za ziada.
Pia nyote mnaonekana kupenda kuwa pamoja nyumbani, Japo wewe kimtizamo wa akili yake anakuona ni mzembe katika kutafuta pesa,hali ya kuwa yeye ni mtu wa kutaka kufurahisha nafsi yake na mwenye matumizi.
Mara nyingi akiwa na wewe atajiona kabanwa na hana uhuru wa kufanya anayoyataka kitu ambacho humfanya kukuchukia taratibu. Nyinyi ni watu ambao hamtoshani hata kimwili na vile vile kwa kuwa tu mnafikishana basi lakini kama mtakuwa ni marafiki wa mbali watu wanawaita wapasha viporo mtaendana.

Sumary:
mnaonekana kuendana tu kwa asilimia 29.

SEHEMU ZA HISIA.
Ni mtu mwenye hisia zaidi katika kiuno chake kama unataka kumpumbaza katika tendo basi muombe kucheza cheza nae ili akikatika uwe umemshika kiuno na ukimgusa kisehemu kile wanachotumia kuchoma sindano za matak* basi yeye huhisi raha sana na hisia za kiwazimu na pia anapenda kuoga pamoja hasa ukimsponge eneo hilo na makalio yake
Ukifanya utundu zaidi eneo hilo chochote unachotaka atafanya lakini ndio hivyo mtaishia njiani

Rakims
 
Me:23/07 D
Ke:20/04 R
Mahusiano haya Simba haki yake ya kutaka uhuru na kutawala mahusiano inakuwa inaendeshwa na kujaribu sana kupingana dhidi ya dhamira ya Ng'ombe kutaka kupeleka mambo jinsi anavyotaka yeye.

Wawili hawa wote ni wenye nyota thabiti yaani zisizopinda hivyo hakuna ambaye atataka kupindishwa na mwenzie jinsi anavyotaka mambo au kurekebishwa vita huanzia kwenye tabia ya simba ya kutaka usafi na Ng'ombe usafi wake ni wa nje tu.

Utakuta mara nyingi Simba anakuwa ni mwenye kughadhabishwa na Ng'ombe na Ng'ombe zaidi anakuwa na kiburi chake cha asili.

Utamshangaza kwa tabia yako ya matumizi ya kujiachia na hali ya kuwa yeye ana asili ya Ubahiri na uchoyo hata kwa wazazi pia. Yeye ni mwenye tahadhari kubwa na makusudi sana;

Wakati wewe ni mwenye kupenda kujitanua na kujiachia kupita kiasi.

Asili ya Simba hupenda kutukuzwa kama mfalme sasa kwa yeye Jeuri utakuta kila mara anakupinga kiuhalisia huyu kwako ni mpinzani na wala sio mpenzi haijalishi mna mapenzi kiasi gani au umemfanyie nini baadae atakuona hufai tu. Na pia wewe ni mfalme binafsi hivyo kunyenyekea yoyote kwako sio rahisi zaidi unapenda kusikilizwa na kuheshimika.

Mnapoelewana zaidi ni wakati wa kufanya ngono tu.

Ubinafsi mwingi sana kati yenu na ndio kitakacho wagombanisha maana hakuna kati yenu anaekubali kuambiwa ukweli kama ni mbinafsi lakini wote nyie wabinafsi.

Rakims
 
Mimi ke-26/11 D
Mme. 13/05 N
Wewe ni mtu mwenye tabia za maji na yeye ni mtu mwenye tabia za udongo kwa mjumuiko huu unaonyesha kabisa nyinyi kuendana ni vigumu na hata kama mnapendana vipi itakuwa dhoruba tu ndani.
Kwa mtizamo anaonekana yeye ni mtu wa kupenda utawala na ukubwa kwa kuongoza mambo/kupelekesha- ambapo wewe unaonekana sio mtu wa kupelekeshwa na hautakubali hilo.
Pia wewe ni mtu wa kuhitaji mabadiriko,anuwai,matukio ambapo hayo humfanya yeye kujihisi tofauti na wewe kwa kuwa yeye ni mtu wa ambaye hujifanya ni mjuaje na incharge wa mambo yanavyokuwa yanakwenda katika miliki yenu na kujiona ni mtawala mzuri wa tabia za nyumbani na hujiona ni mwenye hekima na heshima na imani zaidi kuliko wewe;-
yeye anakuwa ni mtu wa kutaka kufanya mambo ambayo teyari yana uhakika na kutaka kufanya mambo yenye uhakika,
wakati wewe unakuwa upo teyari kufanya chochote kinachowezekana.
Na pia wewe ni mtu wa kusema chochote kinachokujia na nimtu wa kumdondoshea maneno tu randomly yanayokujia kichwani kwa fikra yako ambayo humfanya kuanza kujawa na hasira taratibu. Pia kuna tatizo la pesa katika mahusiano yenu, hiyo ni sababu wewe unataka kuzalisha pesa kwa yanayowezekana leo hali ya kuwa yeye anawaza kuhusu mambo ya kesho (ukifa unaniachaje)
Mna muda mfupi sana kwenye mahusiano yenu.

MTIZAMO WAKE KWAKO:
Mapenzi yenu yanaweza kwenda kama tu ataweza kujikaza vizuri kuwa na wewe au kukuvumilia kwa maana mtizamo wake kwako wewe ni mtu ambaye huvumiliki. wote mnavutiwa zaidi kwa muonekano wa mwenzi wake, kwa tamaa zake yeye alizonazo katika kufanya tendo anakuwa anavutiwa zaidi na ufanyaji wako. Lakini ni mtu inamuwia ugumu katika kuvumilia tabia yako ya kupepesa macho na kutizama mambo mapya(wanawake wa nje) wewe ni mtu wa kuchukulia kila jambo poa poa na rahisi rahisi inapokuja katika maswala ya mahusiano na tendo la ndoa wakati yeye ni mtu muda mwingi anataka kuwa serios kwenye mahusiano na kutawala. hali ya kuwa wewe ni mtu ambaye hutaki kutawaliwa kimapenzi na mtu yoyote hakuna baya kwenu lakini ni watu wenye kupishana mara kwa mara uhawara kwenu inakuwa ni starehe kuliko ndoa. maana mnaweza kukaa kwenye uhawara miaka ila mwezi tu ndoa ikawa ndoana.
Mahusiano yenu ya ndoa yatakuwa ni vichekesho tu.

SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu.
Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake

Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very
gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.
Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe ikiwa atajua kucheza na mapaja yako yako basi ataweza kukupeleka mbali sana kihisia hisia zako siwezi kukwambia sana kwa maana wewe unamtizamia yeye.

UTAMVUTIA VIPI:-
Yeye kwanza sio mtu wa papara ni mtu anapenda kama ni utafiki ama mahusiano basi yaanze taratibu kama vile unajenga nyumba mapenzi kwake anataka uanzie msingi kwanza hivyo inakutaka kuwa ni mtu mwenye subira kuweza kummudu kimapenzi na subira wewe muda mwingine ni kitu huwa,
Mbinu;
kwanza kabisa kama ndio unaanza nae basi hakikisha kuwa unakuwa ni mtu wa kwanza kumtafuta na usiende nae kwa pupa kama hujagusa katika kujifanya ni mtu mwenye subira sana basi moja kwa moja hutampata kwa maana kama ni wa dada wazamani huyu atakwambia nisubiri miezi 9 nikufikirie.
Muonyeshe kuwa upo radhi kuwepo muda wote pale anapokuwa anakuhitaji na ujionyeshe kuwa wewe ni mtundu mtundu. Yeye hupenda mtu anaekuwa taratibu taratibu na kama unaweza kumsababisha kucheka cheka basi huna muda mrefu unayoyataka utapata. Pia utaanza kumuona nae ni mtu anautundu utundu na kupenda utani utani na anapenda mtu mwenye kumvutia kwa yale anayoyafikiria akilini kwake yaani unatakiwa kujipendekeza kuuliza unataka niwe vipi?

Tabia zake za kero ndogo ndogo ni mategemeo yake uzifurahie na ujifanye kucheka anapoongea upumbavu au jambo lisilo na maana kwako.
Na kama akisema kwa utani ukajibu kwa utani basi moja kwa moja anakufungulia moyo wake na kuona hakuna mtu kama wewe duniani hapa na anaweza kukuganda kama kupe pia utani wa kimwili kama kumgusa mwili na kumminya minya ni vitu anapenda kama ni mke wako basi jaribu leo hata akinuna ukifanya hivyo anakaa sawa. Ni mtu kama unataka kumtoa basi anapendelea sehemu za hadhi ya juu kidogo na anapenda sehemu anayoenda kuwe kuna watu wanaojua nini wanafanya hasa wapishi. Mnunulie kinyaji kisichokuwa na kilevi ndio mapenzi yake kama sio mlevi lakini kama ni mtumiaji basi utakuta ni mpenzi wa wine.

Mazingira ya nyumbani ukimpikia hata chochote tu hujihisi special sana na hataskia la mtu kuhusu wewe valia mavazi ya kupika unapomuandalia chakula na hakikisha muonekano wako uwe ni safi mfanyie hivyo hata mara moja kwa mwezi utaanza kuona anatoa machozi
Ikiwa mazungumzo yanachelewa basi jitahidi asikushinde kimaongezi na wala usikwame katika kuzungumzia mnayoyapenda hasa akianza kuongelea pesa muhimu tabaka hili ni mwanamke mwenye kupenda pesa na kuigiza hajali pesa.

Pia tengeneza account mbili tatu za bank ili akitizama aone kabisa ni mtu mwenye kushughulika na mambo ya saving hata kama huna pesa atatambua ukipata utatunza.
Usihodhi mazungumzo.
anapoanza kuzungumza usimkatishe na usiwe mzembe katika kutoa sifa akifanya kitu hata cha kipuuzi nyumbani,kwenye gari yake,mapambo ni watu wenye kupenda kusifiwa wanapofanya mambo madogo.
 
Mimi - 19/01 L (me)
Yeye - 25/09 P (ke)
Rakims
Mahusiano haya ni sawa na watu wawili waliokosa uelekeo hawa ndio ukiskia mtu kakosea kuoa au kuolewa.
Wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni upepo wa juu licha ya kutokuendana hata kukaribiana hamkaribiani,
hili utajionea maana ya ile kauli kwamba unaweza kukaa kwenye uhawara miaka 10 lakini mwaka mmoja wa ndoa ukakushinda.

Mtizamo upo hivi:
Wewe ni mtu mwenye kuvutiwa na yeye kwa sababu ana mvuto ambao wewe unajikuta ni mtu wa kumbembeleza pamoja na kubembelezea mapenzi. Upendo mlionao unaweza kukuokoa kwa kipindi fulani lakini hizi ndio ndoa ambazo wenza huwa wanarushiana ngumi maana ni uvumilivu hadi una fikia hatua ya kukata tamaa.
Japo mtafanikiwa kupata watoto kirahisi na mtazaa watoto wazuri kwa kuwa tu mnaingia mlango wa 5 kwenye ndoa yaani kizazi na mali lakini mateso ni makubwa kuliko mapenzi.

Yeye ni mtu mwenye tamaa na wewe kwenye mahusiano kwa muda huo ambao utakuwa nae au mtakao kuwa pamoja.
Elewa ya kwamba mahitaji yake katika mapenzi kuna jinsi na hali atakazo kuwa anataka uwe na wewe hutakuwa na uwezo wa kumpatia, Kikubwa wapo ni hisia haijarishi utafanya nini kwake hataona ukweli wa hisia zako kumpenda na ataona ni maneno tu.
Pia kutoshelezana kwenu ni kwa uchache sana yeye anapenda sana mauno na wewe magoti kidogo itafikia sehemu itakuwa ni mtihani kipindi hiki kwanza utakua huelewi elewi utakuwa unaona kama ni mtu asiyesomeka,
Baadae mwezi wa 9 hadi wa 10 kama hujamuoa anaweza kukwambia anaona uelekeo wa maisha hauoni na kuna uwezekano mkubwa mwezi huo wa mwaka huu akaanza kujihusisha na mtu mwingine na pia utapata habari kupitia mawasiliano yake kwa hivi sasa.

Atapenda mambo ambayo hutaweza kumtimizia kwa wakati anaoutaka sio kwamba huna uwezo wa kutimiza na akiwa tofauti na mtu mwingine utaona hiyo tabia hana atakuwa nayo kwako.

Na katika hali za kujionyesha na kuwaonyesha watu kuwa ana jambo fulani ni tabia ambayo wewe huna kitu ambacho yeye hupenda mtu aliyenae awe hivyo
Na utakuwa ukimuheshimu kwenye mahusiano na yeye atakuwa anakuchukulia kama ni mpuuzi atakuona mbinafsi na unakosea na mapenzi hayapo hivyo na utatolewa kasoro kila mara.

Baada ya hapo kwenye mahusiano hukugeuka na kuanza
kuangalia mahali pengine na kukuweka uwe na wivu nae kwake ni starehe yake japo ni jambo litakalo kuwa linakutesa.

Japo kuwa ni mtu mzuri kwa watu wengine kwako wewe mahusiano haya ni Kichocheo cha maafa (Sijataka kwenda deep sana kwenye case ya wazazi ambayo ndio inanifanya nikwambie ni mtu asiyekufaa.

SEHEMU YA HISIA:
Kiuno chake ndio sehemu inapotawala hisia yake utaona analalama kiuno kinasumbua ili tu kupata kupapaswa na kukandwa eneo hilo.

Rakims
 
Aisee hii ni hatari. Yaani hii miaka 4 ya ndoa ni ya mateso balaa. Unayoyasema ni kweli, huwa nawaza kuwa haya mambo wife anafanya sio yeye ni shetani anamtumia, maana sio ya kawaida.
 
Yangu bado hujajibu mkuu

Me 5/8 herufi O

Mimi Ke 17/8 herufi V

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Hatima yako mwenyewe huijui utajuaje za wengine. Acha utapeli na uvivu. Tafuta njia sahihi ya kupata kiki hata riziki mwanangu
 
Hatima yako mwenyewe huijui utajuaje za wengine. Acha utapeli na uvivu. Tafuta njia sahihi ya kupata kiki hata riziki mwanangu
Upo sawa mkuu au ni stress za maisha zinakutesa, kiasi kwamba hata makala unayochangia huijui? Al muhimu hata username yako tu inaonyesha ni mvivu kiasi gani na tapeli kwa kujiita baba wa yote.
Usijali kila mtu anapitia ugumu na urahisi wa maisha kwa njia zake alizokadiriwa na Mungu hivyo kama yako yanapelekea kurukwa na akili pole sana mwenyezi Mungu atakuongoa na kukusaidia. Hii makala haina udini wala uchawi ni maarifa kama maarifa mengine basi na wewe uzichangie jambo usilokuwa na maarifa nalo.

Rakims
 
Mimi Me 12/08 A

Yeye Ke 22/10 A
Rakims
Wawili nyie ni sawa na moto wa mkaa na upepo wa juu;
Upande wako (simba) wa ubunifu unaendana sana na yeye (Mizani) ambaye ni mwenye kuvutiwa na shughuli za kijamii sanaa za urembo.Wewe ni mwenye kuvutiwa zaidi katika mapenzi na yeye,
Zaidi ya yeye kwako lakini mtindo na ubunifu wako kwenye mapenzi ni rahisi sana kuweza kumpata yeye na kumtawala vema, Kwa maana yeye ni mgumu kufanya maamuzi na hivyo hapo wewe ni rahisi sana kuweza kumpata yeye kiutawala na hakuna kitu wewe hupenda kama utawala wa mapenzi.
Mara nyingi hamta kuwa ni wenye kwenda sawa kwa maana wote wawili ni wenye kupenda sana vitu vizuri na vyenye kung'aa.
Kila mmoja atataka kumzidi mwenzie ili kupata yeye atantion.Lakini kitandani wewe ni Master kwenye mahusiano yenu na hiki ndicho wewe unachopenda zaidi kuwa mshindi kitandani. hata umpe kidogo tu huyu ni mwenye kuridhika sana. Couple hii haina maelezo mengi isipokuwa kikubwa ni mna nafasi ya kuendana.

Rakims
 
Aisee hii ni hatari. Yaani hii miaka 4 ya ndoa ni ya mateso balaa. Unayoyasema ni kweli, huwa nawaza kuwa haya mambo wife anafanya sio yeye ni shetani anamtumia, maana sio ya kawaida.
Pole sana mkuu.l

Rakims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…