Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Sasa mtoto anatafuta nini hapa?
Mahusiano haya ni mshike mshike baina ya mbingu na ardhi au magharibi na mashariki na haijulikani hadi leo ni nini kina waunganisha,

Kipo kinacho waunganisha tofauti na mapenzi ya dhati mara nyingi hata mimba hutokea bila kujipanga,

Mtizamo:

Nyote wawili ni wenye hisia lakini wewe ni mwenye kuwa annoyed na makusudi yake ya ufanyaji mapenzi.

Yeye ni mtu wa kupenda kukaa nyumbani jina lake la utani kiroho ni manyama uzembe yani mvivu na wengi wao huwa ni wenye usafi wa nje tu.

Wakati wewe ni tofauti na yeye, wewe ni mwenye mihemko na msukumo wa kutoka na kupenda mambo mapya na ya sasa hivi sasa hivi bila kuchelewa na pia kupenda uhuru bila kubanwa banwa.

Yeye ni mwenye wivu mkali na pia ana husda ya chini chini na hutaka mambo yaende jinsi anavyotaka yeye na mambo yake ni mwenye kupenda mwenyewe jinsi ya kufanya mambo anavyotaka na hujiweka kwenye kivuli cha dini na hujifanya wanaroho safi lakini hamna kitu hawa ni sawa na kuishi na mafia bila kujua. Na anapokuwa na wewe mwenye msimamo hukuona kama vile ni mbishi na kiburi husikii ya wengine hali ya kuwa yeye ndio mwenye kiburi na gubu,

Japo kuwa yeye ana bahati sana ya kutengeneza pesa. Lakini wewe ni mzuri katika kuponda pesa, Ukipata pesa matumizi yako ni ya hali ya juu sana, zinayayuka kama moto na pale zinapoisha roho yako ndio hutulia.

Safari ndefu ya mapenzi inaweza kuwa ngumu kwenu kwenda, ingawa mkiishi sana itafikia sehemu utapenda style yake ya matumizi na kujinyima ili kufanikisha maswala ya nyumbani.

Rakims
Mkuu nami hujanijibu ni muda sasa
Hyo ya I 11 nove
 
Mwanaume jina I 11 Novemba
Mwanamke Z 15 June
Wewe ni mwenye kuvutika nae kutokana na tabia yake ya uchangamfu na yeye zaidi kwako ni mwenye kuvutiwa na tabia na utata ulio nao. Kwa muda fulani utaona kuwa yeye anavutiwa zaidi na tendo la ndoa mnapokuwa pamoja yaani anavutiwa zaidi na vile unavyo au utakavyokuwa ukimfanyia.
Lakini yeye ni kama kinyonga kwa maana ni mtu wa kubadirika badirika na hili lipo wazi kwake na hii inakuwa kwako ni ngumu ambaye wewe ni mtu mwenye asili ya msimamo na kutimiza jambo kwa ufasaha ukiamua kulifanya na wewe ni mpenzi kipofu yaani unasifa ya kuwa ukipenda umependa yaani una mapenzi ya kihindi,
Sasa kwa yeye ambaye kidogo ana udhaifu wa kutokutulia na mwenye tamaa ya maendeleo au vitu vyenye kuendelea ukilegeza kidogo tu basi huweza kukuondoka , wakati wewe ukiwa kwenye kuhangaika kumpata mpenzi ambaye utaweza kumtawala na kummiliki,
Kiuhalisia wewe una asili ya upweke na hupenda kujitenga na watu na mashughuli au mchanganyiko lakini yeye ni mwenye kupenda mipango ya nje na kupenda shughuli yaani kiguu na njia.
Mtakuwa na maisha mazuri kiasi ya furaha.
Lakini mapema sana utaanza kuona yeye anaanza kutafuta njia za kuachana ili akachakatie mbele.
maana kwako ataona ni sawa na jela.

Rakims
 
Wewe ni moto wa jaha na yeye ni moto wa nyasi;

ni watu mnaendana vizuri tu ya kuzingatia ni kwamba yeye na wewe nyote mna moto wenye kufanana kwa maana moto wa nyasi huwezi kuanza wenyewe na pia moto wa jaha huzuka tu na kuwaka wenyewe hivyo couple yenu ni nzuri ila ina vichekesho vingi.



Yeye kwako ni mwenye joto la kukutosheleza,

Nyote wawili ni wenye kujituma, kujishughulisha na wenye kupenda kuwa pamoja vile vile kutoka pamoja.

Pia nyote wawili ni wenye kupenda raha au maisha mazuri,

vile vile kutakuwa kati yenu kuna migogoro;

hii ni kwa sababu nyote ni wakali na wenye kupenda ukweli,

Mabishano yatakuwepo na yakianza nyumba inakuwa kama kunawaka moto;-



Pia linapokuja suala la muingiliano yaani ufanyaji wako wa tendo kwa pupa sio kila mara yeye atavumilia



Pia hata hivyo kati yenu mna hisia za ajabu mkiwa pamoja,

hali ya ucheshi na kufurahia ushirika wa kila mmoja.

ni watu ambao hamuoni tabu kufanya mapenzi popote hisia zikiwakamata.



SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake kuu za hisia ni kwenye miguu na mapacha yake unaweza kurudi kwenye quotes za nyuma ukaona kuna mtu nimeshamuelezea

Rakims
Shukrani sana mkuu.
 
ME 1/9 - M
KE 6/02 - N

Naomba Muongozo Mtaalamu
Sawa mkuu kwa mtizamo unaonekana ni mtu mwenye mwenendo wa mchanga mwekundu na yeye ni upepo wa kimbunga kwa mtizamo huu tu ni watu ambao hamuendani lakini nitakufafanulia hapa kwa ziada maana mnaendana kwa asilimia 28 tu.

Nyote mnaonekana ni wenye busara na mko vema kiakili na ni wenye mtazamo wa upendo katika mwanzo mwanzo. Wito wake na mawazo pamoja na mitazamo yake hukuona huwa unachukulia poa na rahisi rahisi tu. Pia nyote kila mtu ana mitizamo yake tofauti na mwenzie na pia wewe ni mtu mwenye tahadhari sana kwake linapokuja swala la kuonyesha hisia zako nae fikra zake huwa mbali sana na mawazo yake pia ni mtu akiwa na wewe hata ukiongea anakuwa anawaza vitu vingine yeye anakuwa ni mwenye kuvutika na watu tofauti na wewe na hata ukimuuliza interest zake zinakuwa ni tofauti zaidi kutoka kwako yaani vigezo vyake unakuwa hukidhi. Wewe ni mtu unaonekana mwenye kujitafutia mambo yako na mwenye kutaka kufanikisha yako unayo yataka wewe na kujihifadhia pesa.
Lakini yeye anakuwa ni mtu wa kuwaza na kumaliza muda wake katika ubunifu,maono, na hujiona kama Bikira amehifadhiwa, mwenye busara,
na kuonyesha vitendo sana kuhusu matamanio yake.
Kama unawaza kuwa nae kindoa acha mawazo hayo unapotea na vile vile hata urafiki tu kwenu kuendana hakuna.

SEHEMU YAKE YA HISIA;

Sehemu yake ya hisia zaidi ni supu za miguu na ankles. Gusa,papasa,tomasa au mbusu sehemu hizo basi ukifanya hivyo utaona hisia zake zinapanda kwa kasi na anakuwa radhi hilo ni eneo nyeti sana kwake na wengine wao hupenda kusafishwa miguu saloon hivyo Kugusa,
kusugua, kupapasa, au kumbusu sehemu hii ya mapenzi ya anatomia kwa kiasi kikubwa humuamsha hamu ya tendo.
mfanyie kumbembeleza kifundo cha mguu, kusonga hadi supu kama massage laini, na uone jinsi anajibu haraka.
Wanamaji hupenda kuwa na miguu ya chini na vifundo vyao vya miguu vilivyotiwa ujazo mfano mguu wa bia hupenda pia mchezo wa kumwagiwa maji miguuni.
Kama hatua ya awali ya kufanya mapenzi, mpe massage nzuri ya miguu. Tumia vidole vyako au kucha, na na uwe kama unampatia ganzi kiasi
utaona analalama kwa upole. Anza kwenye vifundo vya miguu, na ueleze polepole duru kuzunguka mfupa wa kifundo cha mguu.
Mpake mafuta kwenda juu kwa taratiibu hadi eneo lote la nyuma uone mguu umelegea Wakati wa kufanya mapenzi, jitahidi kushika miguu yake na kuifanyia mitelezo utaona anazidi kutoa sauti za mahaba na mawadah.
japo kuwa hamuendani hii inaweza kukusaidia kwa nafasi kubwa kuweza kumkamata.

Rakims
 
Me 26/05 S
KE 25/05 M
Kwa mtizamo mnaonekana nyote wawili ni wenye asili ya upepo wa pumzi hivyo katika vitu vyenu vingi nyie ni kama pacha wa kiroho lakini hiyo haimaanishi kuwa mmekamilika kwa sababu mnaendana kwa asilimia 83%
ingawa mna thamani kubwa ya muendano mtizamo wenu unakuwa
Hakuna mfano wa mahusiano kama yanapokuwa yamejengwa na watu wawili wenye mtizamo huu wa upepo ulio wa kuendana vizuri kwenye haiba,
wenye msisimko na furaha kama wa wewe na mwenzio mnaonekana ni watu ambao hamtawahi kuchoshana au kuchokana kirahisi kwa maana nyie ni kama mapacha na ni wenye nia moja kwa kila jambo ;-
kasi yenu katika mahusiano inashika namba za juu mkiwa pamoja na mnakuwa ni sawa na mfano wa kuigwa kwa mahusiano ya wengine ndio hawa mkikutana utasikia ndoa zingine zinawapigia mfano kuwa unawaona fulani na fulani.

Nyote ndoto zenu kila mmoja kwa mwenzie ni kubwa na hakuna kati yenu anaweza kumkatia tamaa mwingine.
Pia ni wenye mazungumzo ya kuvutia hata chat zenu mtu mwingine akitizama anaweza kutamani jinsi mnavyojibizana na jinsi mnavyoweza kuelewana katika maongezi pia mahusiano yenu yanaonekana kuwa na marafiki wengi na pamoja mnaweza kuwa mnafanya makaribisho ya chakula au sherehe mkiwakaribisha watu wanakuwa wanawatamani sana.
Sex ni mchezo mzuri na uliojaa matani mengi kwenu lakini ndio mahusiano yenu kuna kipindi yanaweza kuwa kama ya juu juu, yasio imara, na msiokuwa na utulivu hasa mkiondoka mazingira ya nyumbani /chumbani na mkikaa muda mrefu bila kukutana na kucheza cheza kimwili basi kila kitu kinakuwa machafuko mkikosa tendo kwa muda ikiwa mnajua au hamjui basi huzuka chokochoko za ugomvi wa maneno.

Rakims
 
Ke-26/11 jina D

Me -10/05 Jina N
MTIZAMO WAKO KWAKE;

Wewe ni mtu mwenye tabia za maji na yeye ni mtu mwenye tabia za udongo kwa mjumuiko huu unaonyesha kabisa nyinyi kuendana ni vigumu na hata kama mnapendana vipi itakuwa dhoruba tu ndani.
Kwa mtizamo anaonekana yeye ni mtu wa kupenda utawala na ukubwa kwa kuongoza mambo/kupelekesha- ambapo wewe unaonekana sio mtu wa kupelekeshwa na hautakubali hilo.
Pia wewe ni mtu wa kuhitaji mabadiriko,anuwai,matukio ambapo hayo humfanya yeye kujihisi tofauti na wewe kwa kuwa yeye ni mtu wa ambaye hujifanya ni mjuaje na incharge wa mambo yanavyokuwa yanakwenda katika miliki yenu na kujiona ni mtawala mzuri wa tabia za nyumbani na hujiona ni mwenye hekima na heshima na imani zaidi kuliko wewe;-
yeye anakuwa ni mtu wa kutaka kufanya mambo ambayo teyari yana uhakika na kutaka kufanya mambo yenye uhakika,
wakati wewe unakuwa upo teyari kufanya chochote kinachowezekana.
Na pia wewe ni mtu wa kusema chochote kinachokujia na nimtu wa kumdondoshea maneno tu randomly yanayokujia kichwani kwa fikra yako ambayo humfanya kuanza kujawa na hasira taratibu. Pia kuna tatizo la pesa katika mahusiano yenu, hiyo ni sababu wewe unataka kuzalisha pesa kwa yanayowezekana leo hali ya kuwa yeye anawaza kuhusu mambo ya kesho (ukifa unaniachaje)
Mna muda mfupi sana kwenye mahusiano yenu.

MTIZAMO WAKE KWAKO:
Mapenzi yenu yanaweza kwenda kama tu ataweza kujikaza vizuri kuwa na wewe au kukuvumilia kwa maana mtizamo wake kwako wewe ni mtu ambaye huvumiliki. wote mnavutiwa zaidi kwa muonekano wa mwenzi wake, kwa tamaa zake yeye alizonazo katika kufanya tendo anakuwa anavutiwa zaidi na ufanyaji wako. Lakini ni mtu inamuwia ugumu katika kuvumilia tabia yako ya kupepesa macho na kutizama mambo mapya(wanawake wa nje) wewe ni mtu wa kuchukulia kila jambo poa poa na rahisi rahisi inapokuja katika maswala ya mahusiano na tendo la ndoa wakati yeye ni mtu muda mwingi anataka kuwa serios kwenye mahusiano na kutawala. hali ya kuwa wewe ni mtu ambaye hutaki kutawaliwa kimapenzi na mtu yoyote hakuna baya kwenu lakini ni watu wenye kupishana mara kwa mara uhawara kwenu inakuwa ni starehe kuliko ndoa. maana mnaweza kukaa kwenye uhawara miaka ila mwezi tu ndoa ikawa ndoana.
Mahusiano yenu ya ndoa yatakuwa ni vichekesho tu.

SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni shingo na koo ndio maeneo ambayo kuna hisia zake kubwa za kiwazimu ikiwa;- utagusa eneo hilo,kumbusu na kutomasa eneo hilo hata kama umekaa nae basi utampandisha kwa kasi sana hisia zake na hasa ukiwa umekaa karibu nae ukawa unamgusa hapo chochote unachosema kinaingia kwenye akili yake na roho yake moja kwa moja kuhusu wewe.

Ukimbusu eneo hilo vizuri na kumng'ata kichokozi akiwa kalala chali na kwenye koo lake basi utaona maajabu.
Fanya mbinu hii pia itakuongezea umaarufu kwake

Mfanyie massage hii ili kuweza kumfanya siku yake yote ajihisi yupo kwenye raha:

(1)Akiwa kalala kwa mgongo wake muwekee mitetemo kwenye shingo yake karibu na mizunguko ya masikio yake kwa kutumia vidole vyako tumia miondoko ya taratibu sana kwa maana sio punda huyu kama kina fulani huyu anataka vitu sensitive rudia hivyo hadi uone vipele vimesimama kwenye mikono yake. (Be very
gentle kuzunguka sehemu ya pipe za hewa kwenye shingo vinginevyo utamniga).

(2) Kumbuka ni mtu mwenye kupenda zaidi kufanyiwa hivyo akiwa kalala kwa tumbo lake hivyo fanya hivyo hadi kukaribia eneo la muunganiko wa uti wa mgongo lakini usitoke nje ya shingo maana umeme utakatika halafu ataona unamtembezea wadudu.
Ukianza kuona vinyweleo vimesimama na vipele basi jua chini hali si shwari wacha niishie hapa na Ramadhan hii nisije nikafanya mambo magumu masaa yamebaki machache.

Ikiwa utamgusa au kumfanyia manjonjo sehemu za shingo yake basi ni mtu mwenye kupata hisia za kiwazimu na wewe ikiwa atajua kucheza na mapaja yako yako basi ataweza kukupeleka mbali sana kihisia hisia zako siwezi kukwambia sana kwa maana wewe unamtizamia yeye.

UTAMVUTIA VIPI:-
Yeye kwanza sio mtu wa papara ni mtu anapenda kama ni utafiki ama mahusiano basi yaanze taratibu kama vile unajenga nyumba mapenzi kwake anataka uanzie msingi kwanza hivyo inakutaka kuwa ni mtu mwenye subira kuweza kummudu kimapenzi na subira wewe muda mwingine ni kitu huwa,
Mbinu;
kwanza kabisa kama ndio unaanza nae basi hakikisha kuwa unakuwa ni mtu wa kwanza kumtafuta na usiende nae kwa pupa kama hujagusa katika kujifanya ni mtu mwenye subira sana basi moja kwa moja hutampata kwa maana kama ni wa dada wazamani huyu atakwambia nisubiri miezi 9 nikufikirie.
Muonyeshe kuwa upo radhi kuwepo muda wote pale anapokuwa anakuhitaji na ujionyeshe kuwa wewe ni mtundu mtundu. Yeye hupenda mtu anaekuwa taratibu taratibu na kama unaweza kumsababisha kucheka cheka basi huna muda mrefu unayoyataka utapata. Pia utaanza kumuona nae ni mtu anautundu utundu na kupenda utani utani na anapenda mtu mwenye kumvutia kwa yale anayoyafikiria akilini kwake yaani unatakiwa kujipendekeza kuuliza unataka niwe vipi?

Tabia zake za kero ndogo ndogo ni mategemeo yake uzifurahie na ujifanye kucheka anapoongea upumbavu au jambo lisilo na maana kwako.
Na kama akisema kwa utani ukajibu kwa utani basi moja kwa moja anakufungulia moyo wake na kuona hakuna mtu kama wewe duniani hapa na anaweza kukuganda kama kupe pia utani wa kimwili kama kumgusa mwili na kumminya minya ni vitu anapenda kama ni mke wako basi jaribu leo hata akinuna ukifanya hivyo anakaa sawa. Ni mtu kama unataka kumtoa basi anapendelea sehemu za hadhi ya juu kidogo na anapenda sehemu anayoenda kuwe kuna watu wanaojua nini wanafanya hasa wapishi. Mnunulie kinyaji kisichokuwa na kilevi ndio mapenzi yake kama sio mlevi lakini kama ni mtumiaji basi utakuta ni mpenzi wa wine.

Mazingira ya nyumbani ukimpikia hata chochote tu hujihisi special sana na hataskia la mtu kuhusu wewe valia mavazi ya kupika unapomuandalia chakula na hakikisha muonekano wako uwe ni safi mfanyie hivyo hata mara moja kwa mwezi utaanza kuona anatoa machozi
Ikiwa mazungumzo yanachelewa basi jitahidi asikushinde kimaongezi na wala usikwame katika kuzungumzia mnayoyapenda hasa akianza kuongelea pesa muhimu tabaka hili ni mwanamke mwenye kupenda pesa na kuigiza hajali pesa.

Pia tengeneza account mbili tatu za bank ili akitizama aone kabisa ni mtu mwenye kushughulika na mambo ya saving hata kama huna pesa atatambua ukipata utatunza.
Usihodhi mazungumzo.
anapoanza kuzungumza usimkatishe na usiwe mzembe katika kutoa sifa akifanya kitu hata cha kipuuzi nyumbani,kwenye gari yake,mapambo ni watu wenye kupenda kusifiwa wanapofanya mambo madogo.

Rakims
 
Kwa mtizamo mnaonekana nyote wawili ni wenye asili ya upepo wa pumzi hivyo katika vitu vyenu vingi nyie ni kama pacha wa kiroho lakini hiyo haimaanishi kuwa mmekamilika kwa sababu mnaendana kwa asilimia 83%
ingawa mna thamani kubwa ya muendano mtizamo wenu unakuwa
Hakuna mfano wa mahusiano kama yanapokuwa yamejengwa na watu wawili wenye mtizamo huu wa upepo ulio wa kuendana vizuri kwenye haiba,
wenye msisimko na furaha kama wa wewe na mwenzio mnaonekana ni watu ambao hamtawahi kuchoshana au kuchokana kirahisi kwa maana nyie ni kama mapacha na ni wenye nia moja kwa kila jambo ;-
kasi yenu katika mahusiano inashika namba za juu mkiwa pamoja na mnakuwa ni sawa na mfano wa kuigwa kwa mahusiano ya wengine ndio hawa mkikutana utasikia ndoa zingine zinawapigia mfano kuwa unawaona fulani na fulani.

Nyote ndoto zenu kila mmoja kwa mwenzie ni kubwa na hakuna kati yenu anaweza kumkatia tamaa mwingine.
Pia ni wenye mazungumzo ya kuvutia hata chat zenu mtu mwingine akitizama anaweza kutamani jinsi mnavyojibizana na jinsi mnavyoweza kuelewana katika maongezi pia mahusiano yenu yanaonekana kuwa na marafiki wengi na pamoja mnaweza kuwa mnafanya makaribisho ya chakula au sherehe mkiwakaribisha watu wanakuwa wanawatamani sana.
Sex ni mchezo mzuri na uliojaa matani mengi kwenu lakini ndio mahusiano yenu kuna kipindi yanaweza kuwa kama ya juu juu, yasio imara, na msiokuwa na utulivu hasa mkiondoka mazingira ya nyumbani /chumbani na mkikaa muda mrefu bila kukutana na kucheza cheza kimwili basi kila kitu kinakuwa machafuko mkikosa tendo kwa muda ikiwa mnajua au hamjui basi huzuka chokochoko za ugomvi wa maneno.

Rakims
Me 26/05 J
Ke 26/02 C
 
Me - 16 April - A.
Ke - 12 March - V
Wewe ni moto wa jaha na yeye ni maji ya kisima, wawili nyie mahusiano yenu ni baina ya mbingu na ardhi achilia mbali tabia zenu za kinyota hata kuendana hamuendani kwa umbali na tofauti zenu za kinyota mmoja ni wa kwanza na mwingine ni wa mwisho. Ni sawa na mahusiano baina ya fukara na tajiri siku zote dharau huwa ipo tu.

Mtizamo:

Wewe ni mtu ambaye utakuwa unalazimisha kumvuta nje ya kisima kwa maana makazi yake ni kisima, na wewe utalewa kwa maajabu yake na vishawishi vyake kimwili.
Wewe ambaye huwa ukipenda hutaki kuskia la mtu/shetani wala muazini na mwenye kujiamini kupitiliza basi kwa mara ya kwanza mnapokuwa nae kwenye mahusiano utaona huyu ndiye chaguo langu na nimepata.
Tabia yako ya ujasiri na drama na ndoto zake huleta matukio mengi sana kwenye mahusiano yenu.
Mitizamo yenu kila mmoja ana mtizamo wa tofauti sana na mwenzie.
Wewe ni mwenye kujipa uhakika wa mambo na muonekano wako wa sura unaonyesha ni wa kuvutia machoni kwa jinsia tofauti na yako. Yeye ni mwenye kuwa na aibu na mwepesi kuongozwa au kuamrishwa,
Wewe ni mwenye kupenda kutawala na yeye ni mwenye kupenda mtu wa kumtegemea yeani yeye ni mwenye nyota tegemezi. Ili kuweza kuwa couple yenye furaha hii inataka umakini zaidi kwako maana sote tunafahamu ni nini hutokea ukitumbukiza moto kisimani.
Hivyo kwenye dinya dinya utaona raha sana kuwa nae isipokuwa kuna maisha baada ya ngono.

Rakims
 
Me 26/12 E
Ke 28/02 P
Mahusiano haya ni baina ya mchanga wa pwani na maji ya kisima kuna visima pia vinakuwa na mchanga wa bahari au mweupe chini hivyo couple hii inawezekana.

Mtizamo:

Wewe ni mwnye uwezo wa kutoa na kumpa katika kila sector ambayo yeye anatamani katika mahusiano kuanzia kumtimizia na kumkamilishia yale yote anayotamani katika mapenzi au kutoka kwako na wala hilo kwako sio tatizo hata katika kumfikisha kwenye tendo kwako ni rahisi sana na yeye kufurahia zaidi na husikia raha pale tu unapoonyesha dalili za kumtaka kimwili hata kama kakasirika utaona anaanza kulegeza uzi,

Nae pia ni mwenye kukutamani na hakuna kitu wewe unapenda kama kutamaniwa na yule uliyenae kwenye mahusiano yaani akionyesha tu hata kukutizama kwa jicho la huba wewe hoi.

Kama ilivyo kwa nyota yako kuwa na kutambulika ni nyota ya watu wa serikalini au viongozi basi ndivyo ulivyokiongozi mzuri kwake ambaye yeye hata ikitokea kampoteza hujihisi kuchanganyikiwa na huona maisha yake yameharibika kama kapoteza mzazi, ndio maana wengine utakuta wanakuwa wagumu kuingia kwenye mahusiano kwa kuhofia siku ya kuachana. Lakini yeye anakuwa na nia ya dhati ya kukufuata kwa yale unayomuongoza.

Ingawaje mtasumbuka sana kwenye malezi ya watoto na matatizo ya uzazi lakini ikitokea hili limeenda sawa basi katika watu ambao watakao tamba kwamba oeni mpate kutulia na kufarijika wewe utakuwa ni mmoja wao.

Ladha yake ya ajabu katika mapenzi inaweza kukuathiri kisaikolojia pale mnapogombana ukaona mambo hayaendi ni vile utamu wake utakugusa sana rohoni kuliko kimwili. Mapenzi yake ukarimu na hisia zako kali za uaminifu vinachanganyika na kufanya kila mmoja ajisikie yuko salama na analindwa katika mapenzi na mwenza wake.

Hakika nyinyi ni watu wawili tofauti ambao mtakuwa mmekutana na mwenza sahihi kwa maana kila mmoja atakuwa ni mwenye kuvutika na kujiona kapata kwa mwenzie mtu sahihi.

Rakims
 
Me 26/05 J
Ke 26/02 C
Kwa mtizamo wewe unaonekana ni upepo wa chini na yeye ni maji yaliyotulia(kisima) kwa muunganiko huu inaonyesha dhahiri kwamba ni watu wawili hamuendani hata kwa kuendana kwenu ni kwa asilimia 9 pekee hivyo kwa hapa hata urafiki tu kwa ushauri huwezi kuwa nae kirafiki hakuna popote ambapo mnaendana maana hata kwenye kukutana kimwili ni asilimia 15 tu hakuna kitu kinaenda pamoja nae rohoni ni mtu hamuendani kwa vyovyote lakini kama tu unataka kujua muunganiko wenu hakuna kwenu nyinyi ni baina ya mbingu na ardhi na hata ukilazimisha sana utajitesa wewe na ndugu,jamaa,marafiki hakuna atakae mkubali labda kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu jitahidini kila mtu atizame muelekeo mwingine.
Lakini kama utang'ang'ana nae huyo huyo naweza nikakuchambulia kwa undani zaidi

Rakims
 
Me 07/10 M
Ke 27/01 R
Katika mahusiano haya wewe utakuwa na tabia ya uvivu hii ni kutokana na uchochezi wa jinsi vile yeye anakuwa kifanya tendo na wewe,
Ni nyota mbili zenye asili moja lakini tabia tofauti hasa ukizingatia kwamba wewe ni upepo wa juu na yeye ni upepo wa kimbunga kwa vyovyote vile kuna kipindi ataanza kukuperekesha.
Wawili nyie mna urafiki mzuri hasa katika kila mmoja kumfurahia mwenzie na mna vibes katika kujichanganya na watu, pia mtajikuta ni wenye kupenda sanaa moja hata katika kujihusisha na mambo ya kijamii.
wawili nyie mtaenjoy sana mapenzi kwa upande wa kirafiki zaidi kuliko upande wa kihisia.
Kwa wewe ambaye mara nyingi mambo yako huwa huna uhakika na kuwa na mashaka utafurahishwa na yeye jinsi akili yake ilivyo sharp katika kufanya maamuzi sahihi.
Kama ni mapenzi ya dhati na kujaliana na ukaribu na ulifiki pamoja na kufurahi pamoja basi nyote wawili ni wenye kuendana sana.

Rakims
 
Back
Top Bottom