Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

ME 14/08
KE 10/06

kuna zawadi yako pia mtabiri
 
Me 19/12
Ke 7/01

Herufi Me - D
Herufi Ke - R

Msaada wako Rakims
Ipo hivi kwa mtizamo wewe ni mwenye asili ya moto wa nyasi na yeye ni mchanga wa bahari kwa haraka tu hapa mnakuwa hamuendani mkuu kwa maana mpo tofauti sana kwa maana;-
Yeye anaonekana ni mwenye kufurahiwa sana na wewe kwa kipindi cha awali yaani mwanzoni na wewe atakuona ni mwenye matumaini makubwa lakini vile vile wewe,
Mtizamo wako kwake unakuona ni sawa na mtu aliyejitosheleza lakini nyote kwa pamoja kwenye mahusiano yenu mapema sana utaanza kukasirishwa na matakwa yake ya uhuru bila masharti.
atahisi kuwa huna uwezo tena wa kuweza kumuamini kwa maana tabia za kutaka uhuru zaidi zitatia dosari mahusiano yenu
Na tabia ya kujichanganya, matumizi na kutokujali kwako ikianza kujidhihirisha moja kwa moja na yeye mshipa wa subira utakatika kwa maana matakwa yake yanaonekana ni mtu mwenye kutaka mwenza ambaye atatulia nyumbani/ndani lakini wewe ni mwenye kutaka mwenza mwenye kumruhusu kufanya chochote unachotaka muda wowote.
Kamba yoyote au lolote linalowaunganisha kuwa kwenye mahusiano au ndoa basi haina maisha marefu na huishia kukatika.
Huna tofauti na mtu aliyeoa kwa kuonyeshwa picha

rakims
 
Mimi me 20/10 A
Yeye. Ke 06/06 I

Rakims
Wawili nyie ni wenye asili ya upepo wa juu na upepo wa chini wote ni asili ya upepo na mnaweza kuwa mnaendana hata tukirejea kwenye asilimia mnaendana kwa asilimia 78 kwa mtizamo wenu wawili tukianza na wewe mwenyewe mwenye nyota ya Mizani ni kwamba unaeleweka kuwa ni mwenye kupenda raha na mwenye moyo wa hali ya juu yaani mwenye kujitolea sana katika kusaidia,

Tukirejea kwenye mahusiano yake kwa upande wako anaonekana ni mtu mzazi sana yaani mwenye kuweza kulea vema na huruma,

Nyote wawili ni wenye hamu ya kutaka kujua mambo,wakali(yaani wenye mvuto unaokaribiana), na mwenye upendo. Kwenu, upendo ni jukwaa lisiloisha hoja kiukweli,furaha na michezo ni zaidi ya kawaida kweny wala hakuna wivu au kutaka kutawalana kimahusiano kunaweza kuwavuruga yaani mpo sawa,

Lakini wawili nyie sio wenye kujali ya watu wala kujali katika kuoneana wivu ni watu ambao mkiwa pamoja kila mmoja anakuwa na hamu ya kutaka kumfurahisha mwenzie,

Mahusiano yenu yamejaa mijadala mingi kuliko vitendo yani porojo nyingi vitendo haba. kutokuwa na maamuzi kabisa, kwa hivyo kutakuwa na mijadala mingi lakini sio vitendo vingi.

Walakini, wote wawili mnajua jinsi ya kutumia haiba yenu katika kuwafanya watu wengine wawafanyie mambo.

Mkiishi nyumba moja ni wenye kutesa sana wafanyakazi kama mtakuwa nao maana mnatuma too much.

Rakims
 
Mkuu Rakims

Mimi mwanaume
Tarehe 1 April jina T

Yeye mwanamke
Tarehe 30 November jina A.
Wewe ni moto wa jaha na yeye ni moto wa nyasi;

ni watu mnaendana vizuri tu ya kuzingatia ni kwamba yeye na wewe nyote mna moto wenye kufanana kwa maana moto wa nyasi huwezi kuanza wenyewe na pia moto wa jaha huzuka tu na kuwaka wenyewe hivyo couple yenu ni nzuri ila ina vichekesho vingi.



Yeye kwako ni mwenye joto la kukutosheleza,

Nyote wawili ni wenye kujituma, kujishughulisha na wenye kupenda kuwa pamoja vile vile kutoka pamoja.

Pia nyote wawili ni wenye kupenda raha au maisha mazuri,

vile vile kutakuwa kati yenu kuna migogoro;

hii ni kwa sababu nyote ni wakali na wenye kupenda ukweli,

Mabishano yatakuwepo na yakianza nyumba inakuwa kama kunawaka moto;-



Pia linapokuja suala la muingiliano yaani ufanyaji wako wa tendo kwa pupa sio kila mara yeye atavumilia



Pia hata hivyo kati yenu mna hisia za ajabu mkiwa pamoja,

hali ya ucheshi na kufurahia ushirika wa kila mmoja.

ni watu ambao hamuoni tabu kufanya mapenzi popote hisia zikiwakamata.



SEHEMU ZAKE ZA HISIA:
Sehemu zake kuu za hisia ni kwenye miguu na mapacha yake unaweza kurudi kwenye quotes za nyuma ukaona kuna mtu nimeshamuelezea

Rakims
 
Mimi Me: E 07/05
Yeye Ke:. H 02/06
Wawili nyie ni wawili wasioendana hata kitabia,
Wewe ni mtu mgumu na asiyebadirika kitabia na mwenye msimamo mkali,
Yeye ni mwenye kuruka, kutotulia, kutetereka.
Lakini mnaweza kupata kila mmoja kuvutia kwa na mwingine kwa sababu hizi za tabia ya kila mmoja kwa mwingine—
kwa kipindi fulani,
Yeye atavutika na wewe jinsi ulivyo na shauku/hamu nae lakini wewe utaanza kuhisi mapema kukosa ulinzi wa kimapenzi kwake kama kusalitiwa na yeye.
Jambo hilo litaanza kumchukiza, na wewe ni ngumu sana kuweza kuendana nae vile atakavyo kuwa ni mwenye tabia za kutaka ladha mpya kwenye mahusiano.
Moja kwa moja Matakwa yako kwake na vigezo vya mwanamke unaetaka kuwa nae yatamshinda nae ataanza kutafuta njia za kukutoroka.

Rakims
 
Mwanaume
Tar: 9 April jina R

Mimi Mwanamke
Tar: 28 April jina A

Mtoto wetu.
Tar: 29 April jina N

Cheki hapo boss Rakims
 
Mimi ke 11/2 H
Yeye me 25/9 L
Yeye mwenye uchangamfu na hisia anapoungana na wewe mwenye shauku, basi ngono kwenye huwa ni matani na michezo, Pia ujuzi na ujanja wake katika mapenzi anajua jinsi gani ya kukuingia jeuri na utundu wako hapo unakuwa unatulizwa.

Ni wenye kupendezewa kila mmoja na akili/fikra ya mwingine jinsi inavyofanya kazi na mnaonekana ni wenye kupenda muziki aina moja,kumbi za sinema pamoja na wasanii au sanaa. Nyote wawili mtajikuta ni wenye kupenda parties na watu wengine na pia mnaweza kuwa ni wenye kupenda kushughulika na shughuli aina moja au mtizamo mmoja katika uchakarikaji.

Wala hamtakuwa ni wenye kuzozana kwamba nani awe kiongozi na nani awe mfuasi kwa maana nyote wawili ni wenye kupenda haki sawa.

Hii couple yenu inapendeza sana,

lakini mkikaa muda mrefu bila kuoana basi kuna mmoja ataachia ngazi. Lakini kama mnataka maisha marefu mmoja wenu atasettle down.

Rakims
 
ME 14/08
KE 10/06

kuna zawadi yako pia mtabiri
Sawa mtizamo unaonyesha wewe ni moto wa mkaa na yeye ni upepo wa pumzi,
mnaendana sana japokuwa kwenye ndoa mnaingia katika mlango wa nane mlango wa kifo na ufufuo.
Mtizamo unaonyesha ni watu mnaweza kuingia haraka kwenye mapenzi au ndoa kwa sababu ni watu mnaweza kuwa na mtizamo mmoja na wenye kupenda mambo mengi yanayoendana.
Hivyo vitu vyenu vingi nyote wawili ni maisha ya kijamii,sherehe,theater(movies & tv-shows) marafiki wengi pamoja na uchangamfu.
Yeye anaonekana anaweza kufungua (joie de vivre) kama ni mtu wa kufuatilia sana series na movies utaelewa namaanisha nini yaani anaweza kukuletea furaha tele ya maisha, mambo yenu ni watu wa kukimbizana na aina mbali mbali za burudani na furaha ya maisha. Nyote mnaonekana kila mmoja ni mwenye kumtafutia mwenzio kuona raha ya maisha kupitia yeye.

Unaonekana ni mtu mwenye kufurahia imagination zake zinazompeleka mbali kimawazo na vile vile uchangamfu wake chumbani na utani/uchokozi unafurahia sana kucheka na kufurahi mkiwa chumbani na ni mtu wa kupata hasira na kuishiwa hamu ya kufanya tendo pale anapojaribu kuweka userious kidogo chumbani.

Yeye anaweza kuwa kichocheo kikubwa cha wewe kuwa na wivu kwake kwa sababu ya njia nyepesi yeye aliyonayo katika kugawa/kusambaza upendo kwa watu tabia yake ya kucheka na kila mtu hukufanya kuamsha hisia zako za wivu .
Unaonekana ni mwenye mihemko na mkali zaidi kuliko yeye. Maisha yenu pamoja yanaonekana ni yenye kusisimua na kukasirisha at the same time,
Lakini mnaweza kukaa kwa furaha na amani ikiwa yeye tu atakuwa muaminifu na kuendelea kubaki hivyo. Vinginevyo tofauti na hapo ni Puuf! hadithi ya mapenzi ya dhati inakuwa imeishia hapo.

Hiyo ni kutokana na wewe asili yako ni kuwa ni mtu mwenye moyo mkubwa na hisia kali na usiyeweza kuvumilia usaliti na mwenye kuweka kitu kwenye roho kwa muda mrefu sana japo ni mwepesi kusamehe ila ni mgumu kusahau.
Karibu tena
Rakims
 
ME 18/2 - R
KE 08/2 - Y

Rakims
Baina ya wawili nyie ni sawa na kidole na pete

Nyote mnakuwa ni wenye kutamaniana yaani kila mmoja ana tamaa na mwenzie, na hasa katika kufurahia ucheshi wa kila mtu na mwenzie

Uvumbuzi, maendeleo, kuvutiwa upya kusiko na kifani kwa kila mmoja kati yenu ni jambo la kawaida sana na vile vile mnafaana katika tendo na wenye kushirikiana kwa maslahi mapana

Nyote wawili kila mmoja wenu anajihusisha na yote kwa mwenzie na katika shughuli zote na urafiki pia na kushirikishana kama ni wacheza kamari basi mngecheza pamoja pia kulingana na mnavyoendana.

Mambo mengi ya kujishughulisha kwa nje mnaweza kuwa mbali katika kufanya mambo yenu lakini hilo sio tatizo kwenu. hamna kitu ambacho mnachobishana sana zaidi mwisho wake ni kukubaliana nyote mpo kibusara zaidi kuliko kihisia. mapenzi yenu hayatakuwa mazito sana lakini yatakuwa ni yakuvutia yaani hampo deep sana lakini mtu vema.

Rakims
 
15/1 me - m
26/9 ke - sa
Mahusiano haya ni sawa na watu wawili waliokosa uelekeo hawa ndio ukiskia mtu kakosea kuoa au kuolewa.
Wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni upepo wa juu licha ya kutokuendana hata kukaribiana hamkaribiani,
hili utajionea maana ya ile kauli kwamba unaweza kukaa kwenye uhawara miaka 10 lakini mwaka mmoja wa ndoa ukakushinda.

Mtizamo upo hivi:
Wewe ni mtu mwenye kuvutiwa na yeye kwa sababu ana mvuto ambao wewe unajikuta ni mtu wa kumbembeleza pamoja na kubembelezea mapenzi. Upendo mlionao unaweza kukuokoa kwa kipindi fulani lakini hizi ndio ndoa ambazo wenza huwa wanarushiana ngumi maana ni uvumilivu hadi una fikia hatua ya kukata tamaa.
Japo mtafanikiwa kupata watoto kirahisi na mtazaa watoto wazuri kwa kuwa tu mnaingia mlango wa 5 kwenye ndoa yaani kizazi na mali lakini mateso ni makubwa kuliko mapenzi.

Yeye ni mtu mwenye tamaa na wewe kwenye mahusiano kwa muda huo ambao utakuwa nae au mtakao kuwa pamoja.
Elewa ya kwamba mahitaji yake katika mapenzi kuna jinsi na hali atakazo kuwa anataka uwe na wewe hutakuwa na uwezo wa kumpatia, Kikubwa wapo ni hisia haijarishi utafanya nini kwake hataona ukweli wa hisia zako kumpenda na ataona ni maneno tu.
Pia kutoshelezana kwenu ni kwa uchache sana yeye anapenda sana mauno na wewe magoti kidogo itafikia sehemu itakuwa ni mtihani kipindi hiki kwanza utakua huelewi elewi utakuwa unaona kama ni mtu asiyesomeka,
Baadae mwezi wa 9 hadi wa 10 kama hujamuoa anaweza kukwambia anaona uelekeo wa maisha hauoni na kuna uwezekano mkubwa mwezi huo wa mwaka huu akaanza kujihusisha na mtu mwingine na pia utapata habari kupitia mawasiliano yake kwa hivi sasa.

Atapenda mambo ambayo hutaweza kumtimizia kwa wakati anaoutaka sio kwamba huna uwezo wa kutimiza na akiwa tofauti na mtu mwingine utaona hiyo tabia hana atakuwa nayo kwako.

Na katika hali za kujionyesha na kuwaonyesha watu kuwa ana jambo fulani ni tabia ambayo wewe huna kitu ambacho yeye hupenda mtu aliyenae awe hivyo
Na utakuwa ukimuheshimu kwenye mahusiano na yeye atakuwa anakuchukulia kama ni mpuuzi atakuona mbinafsi na unakosea na mapenzi hayapo hivyo na utatolewa kasoro kila mara.

Baada ya hapo kwenye mahusiano hukugeuka na kuanza
kuangalia mahali pengine na kukuweka uwe na wivu nae kwake ni starehe yake japo ni jambo litakalo kuwa linakutesa.

Japo kuwa ni mtu mzuri kwa watu wengine kwako wewe mahusiano haya ni Kichocheo cha maafa (Sijataka kwenda deep sana kwenye case ya wazazi ambayo ndio inanifanya nikwambie ni mtu asiyekufaa.
Zaidi ya hapo siwezi kukuelezea mengi kwa maana details zako umeandika kipuuzi na kifupi.

SEHEMU YA HISIA:
Kiuno chake ndio sehemu inapotawala hisia yake utaona analalama kiuno kinasumbua ili tu kupata kupapaswa na kukandwa eneo hilo.

Rakims
 
Yeye mwenye uchangamfu na hisia anapoungana na wewe mwenye shauku, basi ngono kwenye huwa ni matani na michezo, Pia ujuzi na ujanja wake katika mapenzi anajua jinsi gani ya kukuingia jeuri na utundu wako hapo unakuwa unatulizwa.

Ni wenye kupendezewa kila mmoja na akili/fikra ya mwingine jinsi inavyofanya kazi na mnaonekana ni wenye kupenda muziki aina moja,kumbi za sinema pamoja na wasanii au sanaa. Nyote wawili mtajikuta ni wenye kupenda parties na watu wengine na pia mnaweza kuwa ni wenye kupenda kushughulika na shughuli aina moja au mtizamo mmoja katika uchakarikaji.

Wala hamtakuwa ni wenye kuzozana kwamba nani awe kiongozi na nani awe mfuasi kwa maana nyote wawili ni wenye kupenda haki sawa.

Hii couple yenu inapendeza sana,

lakini mkikaa muda mrefu bila kuoana basi kuna mmoja ataachia ngazi. Lakini kama mnataka maisha marefu mmoja wenu atasettle down.

Rakims

Naomba unijibu ya kwangu Rakims
 
Mwanaume
Tar: 9 April jina R

Mimi Mwanamke
Tar: 28 April jina A

Mtoto wetu.
Tar: 29 April jina N

Cheki hapo boss Rakims
Sasa mtoto anatafuta nini hapa?
Mahusiano haya ni mshike mshike baina ya mbingu na ardhi au magharibi na mashariki na haijulikani hadi leo ni nini kina waunganisha,

Kipo kinacho waunganisha tofauti na mapenzi ya dhati mara nyingi hata mimba hutokea bila kujipanga,

Mtizamo:

Nyote wawili ni wenye hisia lakini wewe ni mwenye kuwa annoyed na makusudi yake ya ufanyaji mapenzi.

Yeye ni mtu wa kupenda kukaa nyumbani jina lake la utani kiroho ni manyama uzembe yani mvivu na wengi wao huwa ni wenye usafi wa nje tu.

Wakati wewe ni tofauti na yeye, wewe ni mwenye mihemko na msukumo wa kutoka na kupenda mambo mapya na ya sasa hivi sasa hivi bila kuchelewa na pia kupenda uhuru bila kubanwa banwa.

Yeye ni mwenye wivu mkali na pia ana husda ya chini chini na hutaka mambo yaende jinsi anavyotaka yeye na mambo yake ni mwenye kupenda mwenyewe jinsi ya kufanya mambo anavyotaka na hujiweka kwenye kivuli cha dini na hujifanya wanaroho safi lakini hamna kitu hawa ni sawa na kuishi na mafia bila kujua. Na anapokuwa na wewe mwenye msimamo hukuona kama vile ni mbishi na kiburi husikii ya wengine hali ya kuwa yeye ndio mwenye kiburi na gubu,

Japo kuwa yeye ana bahati sana ya kutengeneza pesa. Lakini wewe ni mzuri katika kuponda pesa, Ukipata pesa matumizi yako ni ya hali ya juu sana, zinayayuka kama moto na pale zinapoisha roho yako ndio hutulia.

Safari ndefu ya mapenzi inaweza kuwa ngumu kwenu kwenda, ingawa mkiishi sana itafikia sehemu utapenda style yake ya matumizi na kujinyima ili kufanikisha maswala ya nyumbani.

Rakims
 
Back
Top Bottom