Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Kwa jinsi ulivyoomba mkuu nilitamani majibu yawe tofauti lakini kwa uwezo ambao niliojaliwa kwa kifupi naweza tu kukujibu kwamba hapo umekosea uelekeo,
Wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni upepo wa juu licha ya kutokuendana hata kukaribiana hakaribiani na hili utajionea maana ya ile kauli kwamba unaweza kukaa kwenye uhawara miaka 10 lakini mwaka mmoja wa ndoa ukakushinda.
Wewe ni mtu mwenye kuvutiwa na yeye kwa sababu anamvuto ambao wewe unajikuta ni mtu wa kumbembeleza na na kubembelezea mapenzi upendo mlionao unaweza kukuokoa kwa kipindi fulani lakini hizi ndio ndoa ambazo wenza huwa wanarushiana ngumi maana ni uvumilivu hadi una give up japo mtafanikiwa kupata watoto kirahisi na mtazaa watoto wazuri kwa kuwa tu mnaingia mlango wa 5 kwenye ndoa yaani kizazi na mali lakini mateso ni makubwa kuliko mapenzi.

Yeye ni mtu mwenye tamaa na wewe kwenye mahusiano kwa muda huu. Elewa ya kwamba mahitaji yake katika mapenzi kuna jinsi na hali atakazo kuwa anataka uwe na wewe hutakuwa na uwezo wa kumpatia kikubwa wapo ni hisia haijarishi utafanya nini kwake hataona ukweli wa hisia zako kumpenda na ataona ni maneno pia kutoshelezana kwenu ni kwa uchache sana yeye anapenda sana mauno na wewe magoti kidogo itafikia sehemu itakuwa ni mtihani kipindi hiki kwanza utakua huelewi elewi utakuwa unaona kama ni mtu asiyesomeka baadae mwezi wa 9 hadi wa 10 kama hujamuoa anaweza kukwambia anaona uelekeo wa maisha hauoni na kuna uweze kano mkubwa mwezi huo wa mwaka huu akaanza kujihusisha na mtu mwingine na pia utapata habari kupitia mawasiliano yake kwa hivi sasa.
Atapenda mambo ambayo hutaweza kumtimizia kwa wakati anaoutaka sio kwamba huna uwezo wa kutimiza na akiwa tofauti na mtu mwingine utaona hiyo tabia hana atakuwa nayo kwako.
Na katika hali za kujionyesha na kuwaonyesha watu kuwa anajambo fulani ni tabia ambayo wewe huna kitu ambacho yeye hupenda mtu aliyenae awe hivyo
Na utakuwa ukimuheshimu kwenye mahusiano na yeye atakuwa anakuchukulia kama ni mpuuzi,atakuona mbinafsi na unakosea na mapenzi hayapohivyo na utatolewa kasoro

Baada ya hapo kwenye mahusiano hukugeuka na kuanza
kuangalia mahali pengine. Na kukuweka uwe na wivu nae kwake ni starehe japo ni jambo litakalo kuwa linakutesa.
Japo kuwa ni mtu mzuri kwa watu wengine kwako wewe mahusiano haya ni Kichocheo cha maafa (Sijataka kwenda deep sana kwenye case ya wazazi ambayo ndio inanifanya nikwambie ni mtu asiyekufaa.

SEHEMU YA HISIA:
Kiuno chake ndio sehemu inapotawala hisia yake utaona analalama kiuno kinasumbua ili tu kupata kupapaswa na kukandwa eneo hilo.

Rakims
Mkuu asante sanaa.[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji119][emoji119]
 
Yeye hupenda sifa za mara kwa mara na Kutamaniwa na watu pamoja na kusifiwa.

na yeye milele mpinzani wake huwa ni mwenye nyota ya Ng'ombe ambaye ni wewe, Ningekuwa namfahamu huyu mwenzio ningemwambia atafute pa kwenda kwa maana wewe na yeye ni kama mbingu na ardhi vyovyote vile atakuja kukukera au utamkera mchukiane maisha hata salam zitagoma,

Matokeo yake kwenye mahusiano yenu. Kila siku yeye atataka kuabudiwa na wewe utataka kuthaminiwa hii couple haijawahi kwenda sawa hata kwa marafiki tu wa jinsia moja. Wewe utajikuta ni mwenye kupenda kuonekana hata kwa kidogo tu unachofanya yaani kuthamini sana hata kama jambo ni dogo na yeye atapenda kutukuzwa sana hata kama ni dogo.

Wapi uliwahi ona mfalme akamsujudia mtumwa au banki ikaomba mkopo kwa maskini (hutaona isipokuwa miujiza ya Mungu itokee) mkiachana wewe ni mwepesi sana kupata mpenzi wa kawaida na yeye ni mzito sana kurejea kwenye mapenzi.

Katika mahusiano yenu utakuja kumkosea kitu kidogo atakuchukia hadi maiti yako atainanga ukitangulia mbele za haki.

Hakuna kati yenu atakae pata anachotaka kwa mwenzie kwa wakati bila kutumia ubabe na nguvu ya ziada mkielewana leo kesho lazima amsha amsha ianze.

Zaidi ya kuongezea yeye ni mwenye ghazabu na wewe ni mpole.

Ghadhab, yake yeye ni kujaa kifuani fundo la miaka mingi na upole wako wewe ni Gubu.

Kuna ugomvi mkubwa kati ya tamaa zako kwa kutaka mambo yaende kwa mpangilio na yeye mwenye kuhitaji zaidi kupita hali ya maisha yani kama mna budget ya mwezi yeye yupo radhi aitumie wiki.

Kingono/tendo utapenda jinsi mnavyoendana ni balaa, lakini yeye anaangalia maisha kama duara 3 ambazo zinatakiwa kuzunguka pamoja na wewe hii itakuwia ugumu kutizama.

Muache aende kwa kina Aquarius ndio wanawezana nae na wewe tafuta Scorpio akuchangamshe vile unavyotarajia.

Rakims
Rakims vip kuhusu tendo la ndoa kutoka kwako je nitapata ?ananizungusha sana
 
Kati yenu kuna mvuto mkubwa sana wa kingono na pia mnaendana vizuri na kimtizamo mnaendana vema sana kwa maana yeye ni maji ya bahari na wewe mchanga wa bahari hivyo mna mtizamo mmoja katika mambo yenu mengi na mnaendana kwa asilimia nyingi;
Kama mtaweza tu kuwezana tabia zenu basi moja kwa moja mtakuwa na mahusiano yenye bahati na mafanikio makubwa kindoa mfano wake utasikia watu huyu kaoa leo nyota yake imeng'aa au mafanikio yake yamefunguka yupo vizuri kwa kila sekta hii ni kwa maana kuwa hata mkiingia kindoa mnapatikana katika mlango wa 12 yaani mzunguko mzima wa nyota 12 unakuwa pamoja na nyinyi bega kwa bega na kila mmoja wenu anakuwa kayapatia maisha na hakuja haja ya kuhofia riziki kwa maana kwenu mkiwa pamoja kila jambo huenda vizuri na kwa ufasaha zaidi.
Lakini kwenye mlango wa kazi pia unatakiwa sana ujitahidi kumuachia yeye pia afanye kazi na kama ni biashara mpe nafasi ya yeye kuisimamia utaona maajabu ya Mungu kwa maana wewe asili yako ni mazingira ya nyumbani na yeye ni mtafutaji mzuri na ana nyota ya mafanikio na ndio bahati yako imelalia kwake usije kumvuruga wala kumuharibia muelekeo kwani huyu unaweza kutembelea nyota yake pindi utakapofunga nae ndoa na ukitaka kuthibitisha hapa kwa watu kwamba haya mambo sio kubahatisha basi muoe siku ya jumatatu kama sio saa 1 asubuhi saa 8 mchana na kama sio hapo basi saa 3 usiku utajiuliza ulichelewea wapi kwa maana usiku wa kwanza tu mmeanza kuitumikia ibada ya ndoa matunda yake siku inayofuata hadi kuingia usiku utaona matokeo na hapa nazungumzia ndoa sizungumzii uhawara.
ni mtu sahihi kwako na ana maslahi mengi na hutaamini ukiwa nae.
na pia ni mtu ambaye anaweza kukukamilishia all the attention you need. Na vile wewe ni mtu wa aibu na mwenye hisia kali na kupenda kukosoa basi huyu kwako ni sahihi;-
Mtizamo unaonyesha wewe ni mtu wa aibu,hisia na mwenye kutaka affection wakati yeye ni mtu wa kuondoa aibu,kuponya maumivu ya hisia na kutawala ndio sifa zake basi popote utakapo hisi you are down she will lift you up haijarishi kipesa mawazo au hisia.
Tofauti zenu zinaweza kuwa kubwa sana ambazo zitaleta furaha za muda mrefu, yaani hapo ni mfano wewe ni hasi na yeye ni chanya. Perfect Match.

Rakims

Asante sana
 
Mahusiano haya ni baina ya maji ya moto na upepo wa kimbunga hii ni fahari wawili hawakai zizi moja na pia hawa ni wagomvi wawili walio kubaliana kila mmoja akae upande wake wa dunia,

Mahusiano yenu yapo hivi:

Wewe utakuta ni mwenye kuwa na matakwa mazito ya kihisia, lakini yeye hata kuruka nae mara moja sio jambo zito kwake kwa upande wako yaani kumvulia nguo kwako yeye kwake ni jambo la kawaida wala halina uzito wowote katika hisia zake, kwake yeye wewe kukutana nae kimwili ni kama tu kupanua upeo wake wa yeye kukujua zaidi wala sio jambo la ajabu na kumfanya ajihisi yupo kwenye serious relationship.

Wewe ni mtu ambaye hutaweza kuvumilia jinsi yeye atakavyo kuwa anachukulia mapenzi yako kirahisi rahisi.

na kila mara unaweza kuwa na hisia kwamba hayupo serious na wewe isipokuwa ni part time tu.

Yeye binafsi ni mtu ambaye ni mwenye kuvutiwa zaidi na vya nje hata hivyo vya nje akiingiza ndani bado atavutiwa na vya nje tu hata ukiwa kwenye ndoa nae huyu hashindwi siku moja kukwambia umalaya upo kwenye damu you deal with it or leave it.

Japo akimpata anaemmudu kinyota huwa mpole kama kondoo.

Kitu ambacho wewe kitakutia wivu wa ajabu na vile una asili ya wivu, basi utataka kujaribu kumtawala na utakuta kila mara anakuvuruga jinsi anavyopenda uhuru na alivyo na mood za kuswing basi safari yenu itakuwa ngumu.

Wewe utakuta ni mwenye kupenda kuwa nyumbani na yeye utakuta ni mwenye kupenda uhuru wa kuendelea hadi mwisho kila mtu atashika njia yake.

Mkilazimisha nyie ni mtu na jamaa yake wasioelewana wanaochangia nyumba kulipia kodi.

Rakims
Athantee

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Naomba kuuliza. Kama ni herufi ipi inatumika hapa? Watu tuna majina mawili.
1. Majina ya Dini
2. Majina ya Asili/Kiafrika.
Lipi ni kina sahihi?
 
Naomba kuuliza. Kama ni herufi ipi inatumika hapa? Watu tuna majina mawili.
1. Majina ya Dini
2. Majina ya Asili/Kiafrika.
Lipi ni kina sahihi?
Jina maarufu linalotambulika na watu wengi
 
Ke: 28/02 M
Me 24/04 K

Mimi ndio Ke
Mahusiano haya yeye anaonekana ni mwenye nguvu, mamlaka na mwenye uwezzo wa kutoa usalama kwako ambaye mara nyingi unakuwa na asili ya kuyumba yumba, Pia yeye ni mtu anaeweza kukuongezea mawazo ya ubunifu kwa kuwa wewe una asili ya ubunifu,

Wewe pia utamletea tabia ya kumjali, na pia kwake yeye utakuwa ni mwenye kujiachia, mkiwa pamoja basi mtahakikisha kuyaweka sawa mapenzi yenu na kuwekana sawa ikiwa ni pamoja na kurekebishana, nyote ni wenye mapenzi ya dhati katika mahusiano haya na wenye hisia kali, ingawa wewe ni mwenye hisia kali zaidi na na tabia yeke yeye ya kutaka kujiweka kuwa mtawala basi hukufanya kujihisi kama kakulinda na kukulindia mapenzi yako.

wakati utawala wake hukufanya wewe kujihisi umelindiwa mapenzi basi ndivyo inavyokuwa kwa maana anakuwa ni kweli kalinda mahusiano yenu na vile vile itafikia sehemu utahisi na kuona kakutosheleza na hutahitajia mwingine tofauti na yeye.

Ikiwa yeye atajirekebisha na kitabia chake cha kutaka usaliti kichini chini basi ni mtu ambaye mnaendanana nae pia katika mahusiano haya.

Rakims
 
Me 07/11-C
Ke 11/11-B
Kati yenu kuna mvuto mkubwa sana wa ngono hapa, lakini joto la kihisia haliwezi kuendelea kuongezeka milele.

Nyie ni watu wawili wanaofanana sana na maelewano kati yenu ni kidogo sana.

Ni wenye wivu wa kupindikia kila mmoja na asili ya mapenzi ya kudai mfano nimefanya hichi wewe hujanifanyia.

Wote ni wakali sana kwamba kila dhoruba ndogo haraka inakuwa kimbunga.

Nyote wawili ni wapenda shari, wenye kuchukizana, kutaka kumilikiana.

Wote wawili mpo kwenye mapambano ya mara kwa mara kulazimisha mwingine kuachia ngazi ya utawala wa mahusiano ama awe ndio sababu ya kuachana.

Mmoja kati yenu hukubali kushindwa na likitokea hilo ni mwisho wa hadithi.

Rakims
 
Back
Top Bottom