Nitajie wachezaji watatu waliokuhamasisha kuupenda mchezo wa soccer

Ingekuwa zama hizi nafikiri ungejiunga Yanga princess
 
1. Roberto Carlos
2. Roberto Carlos
3. Roberto Carlos

Napenda sana Mashuti hata nikiwa kwenye 6×6 napenda sana kupiga Mashuti
 
1. roberto baggio akiichezea juventus

2. youri djorkaeff akiichezea internazionale milano

3. ian wright akiichezea arsenal
 
Hahaaa kumbe na wewe ushawahi kuwa Ball bender, sasa si ungeingia kwenye mpira tu pengine saa hii ungekuwa Ulaya, na jina lako lingekuwa linaimbwa kama kina Asisat Oshoala huko
 
Ronaldo de lima na zidane.. ronaldinho is my favourite player of all time ila alikuja badae kipindi ambacho nishakua mlevi wa soka.
 
1. Hamisi Kinye
2. Ahmed Amasha
3. Athumani Juma Chama

Mijinga itakuja kuuliza na kushangaa.
 
Inatosha kusema wengi waliochangia huu uzi ni 33+

Miaka inaenda wakuu

Timu ya taifa ya Brazil ilinifanya nilipende sana soka, hasa fainali ya World Cup ya 1994 walikichafua sana, Brazil vs Italy

Sikuitazama hii mechi nilikuwa bado chalii ila mzee alikuwa na VHS tape ya hiyo fainali nilipokuwa nikiitazama mara kwa mara nikaanza kujiita Rivaldo nilipokuwa nacheza mpira na wenzangu

Ronaldinho akafanya niipende Barça
 
Legendary na miaka yako 60
 
Lete ubuyu wao basi.😀😃😄😁😆 mi ni Edibily Lunyamila miaka ya 1993 na mpaka wakawa wananiita Lunyamila wa huku kwetu nyakatuntu keisho Karagwe. Tulikuwa tukisikiliza Mpira kwenye RTD kipindi hiko.

Baadaye niliipenda Yanga baada ya Edo kuja YANGA na pale yanga ilipokuwa na akina Costantine kimanda, Nonda Shabani "Papii" Anwar Awadh n.k Hapo ndipo niliipenda Yanga rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…