Retail traders wengi ni day traders hivyo macroeconomics kwao ni kama kujisumbua na kupoteza muda, yeye analenga kupata pips 40 to 70 chap kwa masaa kadhaa. Sasa mtu kama huyo aende kuchambua sijui geopolitics ya nini....!
Mwanzoni niliwahi dhani hivyo ila baadaye nikagundua kuwa hata scalpers wanatakiwa kuwa na knowledge hata ndogo ya Macroeconomics hasahasa kuelewa ile economic calendar.
Ngoja nikupe mfano tokea Jumatatu na wiki iliopita, Taifa la Jumuiya ya Wachina walitoa data ya kushuka kwa PMI , hii ilimaanisha imports ni chache kuliko exports, baada ya taarifa hiyo tu, EURUSD alishuka mpaka siku ya Alhamisi maana ukanda wa Euro huwa wanapigwa sana na news kutoka uchina. Hapo daytraders na scalpers walikuwa wanatafuta sell setups tu mwisho ikiwa Alhamisi saa kumi na mmoja jioni kupisha ADP news na Jolts jobs opening. Baadaye news mbaya ikatoka kwa USD, maana yake ni kuwa Unemployment imeongezeka mwezi June so matraders wanaamini kuwa itakuwa ngumu kwa FED kuraise interest rates ila wataamua kupause, EURUSD&GBPUSD NA GOLD zikaanza kujitune kubuy since Alhamisi, hapo daytraders na scalpers wanabidi watafute buy setups na NFP akawa upande wa buyers maana Kuna correlation kubwa sana ya ADP, Unemployment claims na JOLTS JOBS OPENING.
Katazame charts na economic calendar utaelewa nachokiandika.
Mfano wa pili ni Uchaguzi wa Uturuki, Rais Erdogan alipochaguliwa kuwa Raisi, aliweka mtazamo wa kuwa hapa lazima tu-cut interest rates, USDTURKISH LIRA ikapanda, hapa daytraders inabidi atafute buysetups tu Kila siku mpaka pale atakaposikia wamebadilisha maamuzi , ilipanda kwa wiki tatu, imagine ungekuwa na hii knowledge, hata kutaka pesa za mentorship huwazi kabisa ni ndogo mno kwa pesa zilizopo sokoni kwa dump money.
Mfano wa mwisho, JPY pairs , mwangalie GBPJPY na pairs za JPY, Gavana mpya wa Bank of Japan alitangaza kuwa Japan wataremain na low interest rates ya 0.1% alaf Mr. Bank Of England, Bank of Australia, FED wao wanafanya rates hike . JPY kagawa utamu mwezi mzima............na ukimtazama GBPJPY, hakuna technical traders angewaza kuingia maana angejiona amechelewa na pia price ilikuwa Haifanyi collection, kama USDTURKISH LIRA.
ANYWAY NAKUPA MSEMO MMOJA WA BEST SINGAPORE FOREX TRADER, KAREN FOO " 90% OF RETAIL TRADERS LOSE MONEY BECAUSE THEY HATE MACROECONOMICS WHICH MOVES THE MARKETS".
MWISHO AMINI UNACHOKIAMINI, ILA IN A LONG RUN TUTAZALISHA WATU KAMA ONTARIO WANAODANGANYA WATU KUPITIA MENTORSHIP KUWA TECHNICAL ANALYSIS IS ENOUGH. WAULIZE KWANN SASA WANAFUNDISHA KWA PESA WAKATI WANASEMA FOREX INA PESA NYINGI SANA.
Karen Foo anafundisha Bure kabisa. Michael J Huddleston, mgunduzi wa SMC ukisikiliza Twitter space zake yeye huwa ni Macroeconomics tu.