Kwanza pole sana . Pili ni muhimu kufahamu hiyo hasadi ni nini na inaathiri vipi na jinsi gani ya kujikinga .
Hasadi ni hali ya mtu kutaka neema au mambo mazuri ambayo mtu anayo ya muondokee hata kama yeye hata pata faida yeyote. Hivyo basi ile hali ya mtu kuchukia moyoni mwake juu ya jambo zuri ndio hupelekea madhara kwa mtu.
Hasadi ni tofauti na Kijicho kwa maana Kijicho kinatokana na jicho la mtu mwenyewe kuangalia kitu au mtu madhara hutokea hapa ni kusema kwamba sio kila hasadi ni kijicho ila kila kijicho ni hasadi . Vitu hivi vina maelezo marefu sana ila kwa ufupi wake ndio hivyo, Hasadi na Kijicho ni tofauti na uchawi nitaelezea kwa muhtasari pia kuhusu uchawi na dalili zake. Kwanza tuanze na dalili za hasadi
DALILI ZA HASADI NA KIJICHO.
1. kuharibikiwa mambo yako hata kama unaona deal done ghafla mambo huwa tafrani.
2. Kuwashwa mwilini au baadhi ya maeneo kuuma hasa unapokuwa umevaa vizuri sana
3. Kama una gari au mifugo linaweza haribika na hakuna sababu ya msingi au wanyama kufa ovyo. Hapa ndio utaona wengi huzindika magari, nyumba na mifugo yao kwa waganga wa matunguri.- Njia ambayo binafsi sio katika imani yangu, Nishauri tu muombe Mungu akukinge na mabalaa, kwani ushirikina ni dhambi mbaya sana.
4. watoto wachanga hupatwa na Kijicho na hasadi sana na sababu moja wapo ni kuwa watoto wadogo huvutia na kupendeza machoni pa watu that is nature..na pia Kuna wanawake wengi hawawezi shika ujauzito hivyo ukiona mtoto mdogo analia sana kiasi sio kawaida yake huwenda akawa kufanyiwa hasadi au Kijicho.
Twende kwenye mambo ya ulozi Kwanza tufahamu kuwa uchawi ni ushirikina na hii ni fani kubwa sana najua hapa kuna wajuvi sana wanaelewa nacho maanisha.
Kwakifupi uchawi wowote lazima uhusishwe na majini hivyo hapa kuna hitaji umakini mkubwa na maelezo ya msingi kwa mtu kuelewa .
Uchawi upo wa aina nyingi na hufanywa kwa njia mbalimbali. Nitaelezea baadhi.
1. Uchawi kwa njia ya hewa
Huu mtu upewa kitu na mchawi au mganga - nasema hivyo kwa kuwa wengi katika waganga ndio wachawi, kitu hicho huambiwa aning'inize juu ya mti au popote ambapo upepo ukivuma hicho kitu kita tikisika madhara humkuta mkusudiwa apa ndio utaona mtu ghafla kichaa kimelipuka ghafla kimepoa. Ndio maana ukichunguza katika miti mikubwa aghalabu iliyo porini utaona kuna vitu vimening'inizwa.
Nb: hicho kinachoning'inizwa ndio uchawi wenyewe ambao umefungamana na jini husika.
2. Uchawi kwa njia ya maji.
Hapa mtu hupewa kitu akatupe baharini au kama ni dawa basi aichanganye kwenye maji au kuogea ili kufanikisha jambo husika.
3. Uchawi kwa njia ya moto
Hapa mtu hupewa vitu vya kichawi achome au kijifukiza wengi hufanya aidha kwa kujua wanapata tiba sahihi au kutokujua lakini mara nyingi waganga wakitoa dawa za namna hizi huwa wamepewa maelekezo na jini na hivyo uchawi huo hufunganishwa na jini.
4.Uchawi kwa njia ya Udongo.
Hapa mtu hupewa kitu akafukie sehemu yake ya kazi, nyumbani, au makaburini ili apate matakwa yake .
Ni vizuri tufahamu kuwa kuna sababu ambazo hupelekea uchawi ufanyike kwa njia ya maji, hewa , udongo au moto na njia hizi hutofautiana kwa mtu na mtu hii ni katika elimu za kishirikiana ambazo ni shiriki kubwa muda ni mchache siwezi kutolea maelezo kila kitu.
DALILI ZA MTU ALIYEROGWA.
1. kuota ndoto mbaya kama kukimbizwa na nyoka, simba au mnyama yeyote hatari.
2. Kuhisi vitu vinatembea mwilini mwako na mwili kuwasha sana.
3.Kubadilika kitabia ghafla hasa kutoka tabia nzuri na kwenda tabia mbaya na ghafla mtu Kupenda maovu na maasi kupitiliza kama uzinzi, wizi, kusengenya n.k
4. Ugomvi na mke au mume au na ndugu ambao hauna sababu za msingi - hapa ndio hukuta kosa dogo mtu hutamani kuua
5. Kuhisi upweke na mwenye kukataa tamaa na kuchukia watu wema hasa wachamungu- hapa ndio mtu akikutana na kiongozi wa dini au mchamungu anakasirika sana na hataki kuongea naye.
6. Kupata maradhi ambayo hospitali wakiangalia wanasema upo sawa ila unaumwa sana
7. Kuanguka na kupandisha majini - japo hapa ieleweke kuwa kuna dalili za mtu mwenye majini pia kwani sio kila mwenye majini amelogwa ila kuwa na majini huweza kuwa ni dalili umefanyiwa ulozi
8. Hasira kupitiliza na ugumu wa riziki na mambo kukwama hovyo.
9. Kuitwa mchawi na hali yakuwa wewe sio mchawi na saa nyingine kuota unawanga au umezungukwa na paka. Lakini pia kuota una kula nyama mbichi
10. Kupoteza nguo zako hasa za ndani katika mazingira tatanishi na kunyolewa nywele ndotoni au kuweweseka sana usiku
Dalili ni nyingi sana na hudhihirika katika uchumi wako, afya yako, familia yako au mahusiano yako na jamii. Ni vizuri kuwa makini na ndoto zetu kwani ndoto ni moja katika njia ambayo Mungu hutumia kuwasiliana na mwanadamu kiroho. Hivyo yatupasa kuwa makini na ndoto zetu.
Mwisho niseme kuwa mambo mengi yanayotokea katika maisha yetu Mungu hutupa alert na hutujulisha kiroho ni vile tuu sisi wanadamu hatupendi kuzingatia mambo ya msingi na badala yake tunazingatia mambo ya hovyo matokeo yake tunakuwa na maswali mengi katika maisha yetu ambayo badala ya kupata majibu tunapata maswali zaidi. All in all maswala ya uchawi ni maswala ya kiimani zaidi, Njia pekee na sahihi ya kujinasua katika tatizo hili ni kumtegemea Mungu na kujibidiisha kufanya mema na kumuomba yeye ambaye hakuna liunalo mshinda.