Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini ikiwa Taifa Stars itafuzu AFCON mwakani 2024

Pale wapeleke Yanga tu, maana wanamjua shughuli yake na huyo USM ALGER alikuwa na starters 4 jana. Teh teh teh.
 
Hata tukifuzu huko tunaenda kutia aibu, tutakula vipigo hadi tuchakae
 
Nafasi ya Stars kufuzu Afcon ni kubwa sana. Uwezo wa kuisimamisha Algeria kwao upo kwa kutumia wachezaji wa Yanga. Wanacheza popote bila hofu.

Kocha Adel apange mabeki watatu wa kati Bacca, Nondo na Kennedy na kujaza viungo wengi Mudathir, Mauya na Mzamiru wote wanakaba hadi upepo pembeni acheze Farid Ili tupoteze muda kwa kumiliki mpira na kuvizia counter attacks!

Mbele wabaki kina Samata, Kibu, Sopu na Msuva,

Sasa ni zamu yetu Afcon Njia nyeupeee! Uganda watapigwa goli nyingi Niger hawapendi dharau kwao!
 
Tangu tumecheza nao mbinu zote iz zilishafeli na hatujawahi toboa zaid ya vipigo vya goli 7 tu
 
Tutanunua hii mechi.

Siku hizi hata sisi na Giants africa, mbinu hasi tunazo.

Yanga na Simba waungane kwenye figisu chama lifuzu
 
Eti wachezaji wa Yanga, unadhani Marumo wale?

Halafu kwani timu inaingiza wachezaji wangapi uwanjani?
 
Ukiangalia Algeria sasa hivi wanafanya rotation kubwa ya wachezaji. Ni moja ya nchi zenye hazina kubwa ya wachezaji wanaocheza nje ya nchi. Nimeangalia kikosi kilichoanza dhidi ya Uganda, hakuna mchezaji hata mmoja aliyeanza mechi ya leo dhidi ya Tunisia.
 
Hivi taifa halina vijana wenye vipaji mikoani wakawekwa kambini? Uchaguliwe mkoa wenye baridi nyanda za juu vijana wafuliwe vizuri! Nimeangalia ile mechi kama sio juhudi binafsi za msuva watu walikuwa wanakimbia kimbia tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…