Nitakuwa wa mwisho Kuuamini huu Upuuzi ambao naona Simba SC yangu wanaanza kutaka Kuutumia kama sababu ya Kushindwa

Nitakuwa wa mwisho Kuuamini huu Upuuzi ambao naona Simba SC yangu wanaanza kutaka Kuutumia kama sababu ya Kushindwa

Mimi ni Simba SC damu ila sijazoea Unafiki, Ujinga na Upumbavu na nitakuwa wa mwisho pia Kuuamini. CAF kubadili Waamuzi wa mchezo Kwangu Mimi si hoja kwamba Simba SC tunahujumiwa na nimeshtushwa pia kumuona Mwanasimba mmoja ambaye pia ni Mbunge na Mwanasiasa nae bila haya / aibu akiingia katika Upuuzi huu.

Hivi ni mara ngapi hapa hapa katika Ligi Kuu yetu Simba SC huwa tunabadilishiwa Waamuzi? Je Timu pinzani huwa zinatulalamikia kwa TFF? Kama tunadai kuwa hatua hii ya CAF ni ya Kuihujumu Simba SC yetu Sisi Simba SC tulishindwa nini nasi Kuwahujumu vilivyo ile majuzi?

Hivi TP Mazembe ndiyo waliifanya Miguu ya Nahodha Wetu John Boko ilione lango lipo juu akapaisha kule badala ya Kulilenga vyema? Hivi Simba SC nani alitufanya tushindwe kuzitumia zile ' clear chances ' tulizozipata matokea yake Wachezaji wetu wakawa wanarukaruka tu kama Maharage ya Mbeya?

Simba SC msitake kuwafanya Watanzania hasa Mashabiki wetu ( GENTAMCINE nikiwemo ) kwamba ni Wajinga au Wapumbavu au labda wengine hatujawahi Kucheza mpira au hatujui Kuuchambua vile vile. Hivi kuna nani hajui kuwa Simba SC hata kama hao Waamuzi wasingebadilishwa hivi bado Kuwafunga TP Mazembe Kwao Lubumbashi ilikuwa ni ngumu?

Hivi mmejua kuwa kwa Kitendo chenu hiki cha Kulalamikia Mabadiliko haya ya Waamuzi tayari Kiufundi mmeshawaharibu Wachezaji wetu Kisaikolojia? Mimi naamini kuwa kama Simba SC ikijipanga vyema kabisa pamoja na CAF kubadili hao Waamuzi bado tunaweza Kuwafunga TP Mazembe huko huko Kwao.

Uwezo wa Wachezaji wa Simba SC hasa hawa tulionao siyo wa Kushindana na Vilabu vikubwa na hata hii kufikia tu hapa ni Bahati tu ya Mwenyezi Mungu hivyo tusitake kujifanya kama vile Sisi ni Timu bora na ina Mapafu ya Kushindana na hawa Majabali wakubwa wa Kimpira Afrika.

Mkiambiwa kuwa tumieni vizuri Uwanja wenu wa Nyumbani muwe mnaelewa na nadhani mmewaona Mamelodi Sundowns walichowafanya Al Ahly hadi wakawafunga zile Goli Tano kwa Nunge ( 5 - 0 ) wakati Sisi huku Kipaumbele chetu Kikuu kikiwa ni Kuujaza tu Uwanja na kuwa na Tiketi za ' Platinums ' za Kutosha.

Najua wana Simba SC wengi kwa Uzi huu leo mtanichukia GENTAMYCINE ila huwa silei Ujinga na Upumbavu na Unafiki Kwangu ni mwiko bali nitakuwa nanyoosha tu pale ambapo naona panabidi kufanywa hivyo. Ushauri pekee ambao nautoa ni kwamba nawaomba Wachezaji wazawa wa Simba SC kama Mdogo wangu Mkude akina Ndemla, Tshabalaa, Dilunga na Muzamiri wautumie huu mchezo kama sehemu yao ya Kujiuza ili ikiwezekana basi TP Mazembe au Vilabu vingine vikubwa viwamulike na kuwasajili ili Tanzania iongeze idadi ya Wachezaji wake wanaocheza nje.

Ni Mpumbavu tu pekee na asiyejua Mpira vyema ndiyo alikuwa anajua na kujiaminisha kabisa kuwa eti Simba SC ina ubavu / uwezo wa Kumfunga TP Mazembe Kwao ' Machinjioni ' huko Lubumbashi. Twendeni tu tukapokee Magoli yetu ya Kutosha ili yatutie Ndimu / Hasira na tukirudi sasa Hasira zetu zote tuzihamishie katika Mechi zetu za Viporo na zile za muendelezo wa Ligi Kuu ili tulichukue tena hili Kombe kisha Mohammed Dewji na Kamati ya Usajili ya Simba SC bila kusahau benchi la Ufundi likae chini na lifanye Usajili ' Kabambe ' kwa ajili ya Michuano ijayo ya CAF Champions League ambayo GENTAMYCINE naamini kuwa kama Simba SC itashiriki tena na Kusajili ' Majembe ' ya maana basi kwa Msimu ujao tunaweza hata kufika Fainali na kwa Kudra zake Mwenyezi Mungu hata Kuchukua Kombe.

Tuacheni kutafuta Visingizio vya Kipuuzi vya Kulalamika Waamuzi Kubadilishwa. Na hapa nimewadharau Kidogo Viongozi wangu mtanisamehe sana katika hili. Cha kufanya tu sasa badala ya Kulalamika kubalishiwa hao Waamuzi nadhani tutumie tu muda huu Kuwaandaa na Kuwajenga vyema Kisaikolojia Wachezaji wetu kuwa wakiona Magoli yanaingia mfululizo kwa Golikipa Aishi Manula wasiwe wanashangaa bali wajue tu ya kwamba hao ndiyo TP Mazembe na hapo ni ' Machinjioni ' Lubumbashi.

Nawasilisha.
2mbili on duty

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jama
Hata huyo Erasto Nyoni wako hapo Simba SC anaoneka mzuri na katulia kwakuwa huwa analindwa vizuri mno na ' Unsung Hero ' Kiungo ' Mtifuaji ' Mghana James Kotei ambaye ndiye huwa anahakikisha ' back line ' yote ya Simba SC iko salama na haipati madhara yoyote. Mchezaji wako mwenyewe mahiri kabisa Kiungo Jonas Gerald Mkude anakuambia hirizi yake inayomfanya awe anang'aa vyema na kutembea vizuri pale katikati huku akizitupa huku na kule na zile Kampa Kampa tena ni pale tu nyuma yake akiwa anazibwa na James Kotei ambaye hadi sasa ndiye Mchezaji pekee wa Simba SC anayeongoza Kukimbia umbali mrefu ndani ya Uwanja kuliko Mchezaji yoyote mwingine wa Simba SC hii ya sasa.
We jamaa kweli hueleweki kuna uzi mmoja umemkandia sana kotei wakati anakuja simba mpaka ukatishia kuihama timu leo wamsifia kupita maelezo 😂😂
 
Gentamycine usiwe na badilika badilika hebu angalia hapa chini ulivyoidhalilisha kamati ya usajili wakati walipomleta Kotei


We jama

We jamaa kweli hueleweki kuna uzi mmoja umemkandia sana kotei wakati anakuja simba mpaka ukatishia kuihama timu leo wamsifia kupita maelezo 😂😂

Kwani Wewe huwezi Kumchukia Mwanamke lakini baadae huyo huyo ukaja Kumuoa na Kuishi nae Maisha yako yote? Hopeless!
 
Kwani Wewe huwezi Kumchukia Mwanamke lakini baadae huyo huyo ukaja Kumuoa na Kuishi nae Maisha yako yote? Hopeless!
Sasa mambo ya mwanamke yamefikaje hapa
Afu pia huwezi jibu bila kutumia maneno yasiyo na staha. Watu Charismatic huwa hawabehave kama ww badilika
 
Sasa mambo ya mwanamke yamefikaje hapa
Afu pia huwezi jibu bila kutumia maneno yasiyo na staha. Watu Charismatic huwa hawabehave kama ww badilika

Inaonekana hicho Kipengele cha Mimi kuwa ' Charismatic Fella ' achilia mbali hivyo vingine vya ' Purely Talented, Game Changer and Entertainer ' Kinakuumiza sana Mkuu. Basi kichukue Wewe ufurahi!
 
Ongozana na Timu ili ukakae nyuma ya Golikipa Aishi Manula uwe unamsaidia tu Kuhesabu ' Vyuma ' ambavyo vitakuwa vinaingia Mkuu. Kama Timu bora kabisa ya Club Africaine wamekula ( wamefungwa ) Magoli Nane ( 8 ) kwa bila / sifuri unadhani Simba SC yetu huko itakuwaje? Tena kama Kipa Aishi Manula ' Mjanja ' kuanzia sasa ajifanya ameumia ili asipangwe na achezeshwe Deogratius Munishi ili nae pia ' azikoge ' za Kutosha kama zile Tano Tano ' alizozikoga ' Manula ili wasichekane au kudharauliana.
Nishagundua lengo lako... Huna jipya mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matokeo ya michezo mfano mpira huweza kujilikana mapema kabla ya mchezo husika!Kinajimu siku tarehe na muda wa Simba/Mazembe haukuwa wa Simba ndo maana pamoja na Rabsha zote Simba hawakufanikiwa kupata GOLI/MAGOLI,Usindi wa SIMBA ulikuwa ni draw.NA KINAJIMU MAZEMBE VS SIMBA in Lubumbashi imekaa vibaya mno kwa MAZEMBE kuliko mechi ya DAR,Kuna uwezakano mkubwa wa SIMBA kupata matokeo mazuri na huenda Mazembe wameshaliona ndo maana wameanza FIGISU za nje uwanja na hata hizo huwa hazisaidii sana coz haziwezi shindana na NGUVU YA ASILI(UNAJIMU).I attach the charts for SIMBA/MAZEMBE and MAZEMBE VS SIMBA in LUBUMBASHI.View attachment 1066581View attachment 1066582

Sent using Jamii Forums mobile app
Ina maana Simba huenda akatinga nusu fainali? Itakuwa burudani kweli kweli.
 
Ina maana Simba huenda akatinga nusu fainali? Itakuwa burudani kweli kweli.

Zijue nchi Tano ( 5 ) za Afrika zinazoongoza kwa Uchawi / Ndumba ( au Kindoki kwa Kilingala / Kikongo )

1. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( zamani Zaire au Leopold Ville )
2. Nigeria
3. Afrika Kusini
4. Ivory Coast
5. Senegal

Kazi Kwako / Kwenu.
 
Sipotezi muda na Watu walioanza Kuujua na Kuufuatilia Mpira wa Miguu pale Jose Mourinho alipoibuka na kuwa Kocha wa Chelsea tafadhali. Huna ubavu wa Kujenga Hoja na Mimi hasa katika Medani hii ya Mpira kwani achilia mbali tu Kuuchambua na Kuujua pia nimeucheza sana tu na pengine isingekuwa Ukali wa Wazazi na kutaka nijikite zaidi katika Masomo na kutopenda Mtoto wao niwe Mchezaji enzi hizo kuna uwezekano GENTAMYCINE ningekuwa nimeshamtangulia Mbwana ' Popa ' Samatta Siku nyingi mno huko Ulaya ( Ng'ambo ) Siku ukipata muda uwe unatembelea Viwanja vya Barafu au Garden uwe unaona ninavyofanya vitu vyangu hasa sehemu ya Kiungo au Beki Mbili na Tatu. Karibu sana!
Wewe boya tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana hicho Kipengele cha Mimi kuwa ' Charismatic Fella ' achilia mbali hivyo vingine vya ' Purely Talented, Game Changer and Entertainer ' Kinakuumiza sana Mkuu. Basi kichukue Wewe ufurahi!
Mkuu huwa unapenda sana ligi, usijali we liache mi ntalichukua ili nifurahi.
 
Nadhani mawazo ya mtu huwa sawa na matendo yake.Waamzi wote wana mapungufu ila wengine wamezidiwa na mapungufu.
Simba wana haki ya kulalamika kwa kuwa michezo ya kubebana caf ipo sana.
Kiukweli bila figisu kuna viashiria vya mazembe kubebwa hapo hata ikiwa si kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinajimu siku tarehe na muda wa MAZEMBE/SIMBA viko upande wa SIMBA,Itahitaji nguvu ZIADA ZA KIBINADAMU AMBAZO ZITADHIHIRIKA WAZI kupindua nguvu hzo za asili,Pia unaweza uliza swali la kinajimu na likatoa majibu tukio fulani linalokutatiza .NA attach chart ya Swali la kinajiumu kuuliza iwapo SIMBA itafuzu kwa SEMI FINAL lililoulizwa Tar 9/4 saa 12.20 katika mji wa Dar es salaam nchini TANZANIA
Screenshot_20190409-125815.png


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom