Nitakuwepo ifikapo Mwaka 2100

Nitakuwepo ifikapo Mwaka 2100

Lethergo

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2023
Posts
6,534
Reaction score
11,421
Nimeangalia nikahuzuka sana kisha nikapatwa na huzuni, hofu, mashaka na woga kufika Mwaka 2100. Wakuu kwa matazamio yangu ya haraka haraka kila nikilala na nikiamka napata maono ya sauti ya ndani sauti ya ndani ikiniambia mimi ni mmoja kati ya wale watu waliochaguliwa kuufikia Mwaka 2100.

Nimekua nikiiona Mwaka 2100 jinsi itakavyokua ya tofauti sana na miaka mingine yote iliyopita. Mwaka 2100 ni mwaka ambao umejaa mambo mengi sana ya kustaajabisha. Cha kushangaza ninaishi Mwaka 2025 ila ninajiona km ninauisha Mwaka 2100 ndani yangu.

Mwaka 2100 ni mwaka wa mapinduzi mengi ya teknolojia. Ninapata maono ya sauti ya ndani, sauti ya ndani ikiniambia kuufikia Mwaka 2100 nitakua nina miaka isiyopungua 100 na kadhaa nikiwa sehemu fulani nimezungukwa na familia yenye furaha, upendo na amani familia yenye watoto kadhaa wenye nyuso zenye bashasha na tabasamu muda wote, watoto wakike kwa wakiume, wajukuu, vitukuu, vilembwe, na vilembwekeze.

Sauti ya ndani inaniambia Mwaka 2100 sitaweza tena kutembea mwenyewe bali nitasaidiwa kutolewa sehemu moja kufikishwa sehemu nyingine miguu yangu haitokua na nguvu tena ya kutembea na uoni wa macho yangu utakua hafifu mno, sitokua na kumbukumbu za kutosha za matukio mengi yaliyokwisha pita miaka ya nyuma, sauti ya ndani inaniambia naweza hata nikaulizwa mwaka 2025 rais wa Nchi ya Tanzania alikua nani na nisikumbuke sababu ya uzee nitakao kua nao.

Sauti ya ndani inaendelea kuniambia mwaka 2100 nitaushehekea kwa kipindi kifupi tu baada ya hapa nitaitwa nami bila kusita nitaitika.

Je! Wewe mdau wa JF umejiandaaje kuufikia mwaka 2100?

Je! Wewe mdau wa JF Mwaka 2100 utakua na umri gani?

Je! Mwaka 2100 utakua wapi ukiwa unafanya nini?

Huu uzi ninaomba ubakie hapa mpaka ufikapo Mwaka 2100, nina hakika utafufuka tena ifikapo Mwaka 2100 na mimi nitakuwepo kuja kutoa comment yangu hapa.

Ramadhan Kareem.
Kwarezima njema.
Niishie hapa.
1st January, 2100.
 
Hahaha 🤣 🤣 😂 😂 aisee nikiwepo inshallah nitarudi apa
 
Ngiba yamba nasa.

"Siwaahidi kuishi miaka 100 kama alivyowaahidi hayati nyerere" - Kalapina
 
Sio kila mtu atafikia miaka 100.
"Ningeweza kuishi milele ningebakia mstari wa mbele nikiwapa hoja zenye uzima mkasisimka mpaka nywele,omba pepo siyo unaomba uzima wa milele,siwaahidi kuishi miaka 100 kama alivyowaahidi hayati nyerere,duniani nimeona mengi lakini jicho halijafika kilele" - Kalapina.
 
Back
Top Bottom