Nitampataje mume mwenye vigezo hivi?

Maneno yako swadakta mkuu huwezi amini nimejaribu kumsaidia kusachi kwenye google napata results kama zako tena baada ya kubadilbadili ila ukiweka kama anavyotaka yeye inajibu NO RESULTS FOUND:A S thumbs_down:
:laugh::laugh::laugh::laugh:Mohammed bana eti NO RESULTS FOUND ha ha ha ha ha
 
Kwa nini huyu dada ameiga avatar yangu? huyu ana kashfa na ni nungayembe la mjini tu hili hana lolote, we dada badilisha hiyo avatar usinisababishie ban bwana?
Maty nilifikiri ni mdogo wako bana nilitaka kumwambia Kimey ajitose ulingoni l.o.l!!!!!!!!
 
Kwa nini huyu dada ameiga avatar yangu? huyu ana kashfa na ni nungayembe la mjini tu hili hana lolote, we dada badilisha hiyo avatar usinisababishie ban bwana?
:coffee::coffee::coffee:

We Elodii...Avatar ya Maty ni picha yake halisi, inakuwaje mtu mwingine aitumie kutafutia mabwana?
 
Dada yangu alishawahi kunitania kuwa eti niwatongoze wale ninaowapenda na nikitu ambacho siwezi hata kujaribu kufanya. Jamani nisaidieni au ndio niendelee kusubiri ubavu wangu kutoka kwa Mungu?

Nikiripoti kutoka Uvunguni mm ni Fidel
 
kwani wewe huna vigezo hivyo nipate mkwe na uwe umemsaidia kijana mwenzio:coffee:

Mimi nina wewe mpaka kieleweke nataka kwenda kwa kadhi atoe fatwa... maana sikulala usiku wajana nikagundua tunahusiana kwa mbali sanaaaaa yaani huko udigoni ndanindani kwa mababu wa mababu! Khaaaa unataka kunikosesha raha mwana wa mwanamke mwenzio!
 

CPU acha uchonganishi!! Kwa nini ufanye mambo mabaya huku ukiwa unajua kabisa unafanya ubaya!! Respect CPU don't do that and don't say that. This is not Maty am sure!!
 
hivi hizi avatar ni picha zenu za ukweli au:coffee:
 

Vigezo vyote ulivyotaja ninavyo. Mimi ni mtumishi wa serikali. Kipato changu ni cha kati. Bahati mbaya nina mtoto wa kiume wa kujifunzia. Ana miaka mitatu. Ifikapo tarehe 26 Februari nitatimiza miaka 32 kamili. Unasemaje bibie? Ebu na wewe jidescribe kidogo ili nikupatie namba yangu ya simu. I'm serious!
 
Babu nenda google such andika beautiful african girls then click images pale juu utaiona hiyo picha mi nilivyoina nikaipenda naiona kama mimi vile. Huyo mdada/shoga nashangaa kuitumia ana lake jambo ila sio picha yangu halisi kahakikishe kwa google.

Hivi kumbe si picha yako...mi kila siku najua ni yako...mmefanana asee.

sasa punguza munkari au mPM umwombe aiondoe...labda hakujua, si umeona tarehe alizoingia JF? Kaingia siku ya bethdei ya CCM.....so akili za kuambiwa.........
 
Dada yangu
Imeandikwa kwenye vitabu vya msahafu kuwa MKE MWENYE BUSARA MTU HUPEWA NA BWANA, na pia NITAKUPA MWENZA MNAYEFANANA NAYE. Sasa ufanyeje? Jibu ni moja tu. KUOMBA BWANA AKUPATIE MWENZA.
 
Susy chukua hizo criteria halafu google...wanaume wa aina hii wapo wengi tu...hata mtaani kwetu wapo!
 
Originally Posted by Susy

Wapendwa nawasalimu!!

Ninatumai kila mtu ana sifa za ama mke au mume anayemtaka, rafiki zangu wa JF, napenda sana nipate mume mwenye vigezo hivyo hapo nilivyovitaja lakini kila siku imekua kinyume kabisa na matarajio yangu.

1. Awe Mkirsto
2. awe mweupe
3. awe na feature ya maisha, kwani fedha hutafutwa
4. awe mrefu wa wastani
5. kuanzia miaka 30 kuendelea

Dada yangu alishawahi kunitania kuwa eti niwatongoze wale ninaowapenda na nikitu ambacho siwezi hata kujaribu kufanya. Jamani nisaidieni au ndio niendelee kusubiri ubavu wangu kutoka kwa Mungu?

Naombeni mawazo yenu, pengine nafikiri hadithi za kujenga magorofa hewani.


Vigezo si vibaya sana ila nafikiri rangi haina mchango wowote katika mapenzi ya kweli, kwani unaweza kumpata huyu mweupe akawa na mapungufu mengine mengi hasa ya kiutendaji.
 

wewe umeonyesha ubaguzi wako waziwazi unaleta mambo ya makabulu eeh na tena wewe mdini mkubwa!
 

Mkuu njoo nikuuzie mkorogo nadhani unavigezo vyote kasoro hiyo ya weupe umelalama mpaka unatia huruma na kupiga chepua kuwa wewe huna mapungufu kiutendaji.
 
wewe umeonyesha ubaguzi wako waziwazi unaleta mambo ya makabulu eeh na tena wewe mdini mkubwa!

Amesema mweupe hakusema Mzungu!!!! hivi wale waenyeji wa Kondoa sio waafrika? Au mhe mzee wetu wa vijisenti unaionaje Rangi yake? hapo sijakwambia umwangalie Mwapachu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…