Originally Posted by
Susy
Wapendwa nawasalimu!!
Ninatumai kila mtu ana sifa za ama mke au mume anayemtaka, rafiki zangu wa JF, napenda sana nipate mume mwenye vigezo hivyo hapo nilivyovitaja lakini kila siku imekua kinyume kabisa na matarajio yangu.
1. Awe Mkirsto
2. awe mweupe
3. awe na feature ya maisha, kwani fedha hutafutwa
4. awe mrefu wa wastani
5. kuanzia miaka 30 kuendelea
Dada yangu alishawahi kunitania kuwa eti niwatongoze wale ninaowapenda na nikitu ambacho siwezi hata kujaribu kufanya. Jamani nisaidieni au ndio niendelee kusubiri ubavu wangu kutoka kwa Mungu?
Naombeni mawazo yenu, pengine nafikiri hadithi za kujenga magorofa hewani.
Vigezo si vibaya sana ila nafikiri rangi haina mchango wowote katika mapenzi ya kweli, kwani unaweza kumpata huyu mweupe akawa na mapungufu mengine mengi hasa ya kiutendaji.