Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
Na Elius Weston Ndabila.
+255768239284
Hili si jambo la kawaida la mtu wa kawaida kujitokeza hadharani nakusema ipo siku atamshauri Rais ajiudhulu nafasi yake ya kuliongoza Taifa.
Nimetafakari sana hadi kufikia maamzi haya. Nitajitoa kwa niaba ya Watanzania kumshauri Rais kuachia nafasi yake ya kuliongoza taifa hili.
Sababu yangu itakuwa ni moja tu, nayo itakuwa ni “KUNA MAHALI UMEKOSEA”. Ninaamini nitakuwa shujaa wa Taifa hili.
Ninatambua fika kuwa Tanzania tulimhitaji sana mtu kaliba ya Magufuli kuliko kitu chochote. Lakini haitazuia kumshauri ajiuzulu itakapobidi.
Ninajua Tanzania ilimhitaji hasa nikirejea historia ya huko nyuma. Ninakumbuka miaka ya 2010 hadi 2012 miaka ambayo kulikuwa na migomo mingi vyuo vikuu watu walisema tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa serikali ya CCM.
Na wapo waliosema Kikwete ni Vasco Dagama yani anatembea sana na wengine wakaenda mbali wakasema ni dhaifu akiwepo Mh Mnyika.
Watanzania hawa hawakuishia hapa, wakasema kwa mahali nchi ilipofikia inataka tupate Rais dikteta ambaye hatasikiliza chochote.
Watanzania walisema wanataka Rais dikiteta ili maendeleo yakimbie. Wengi wao walisema Mzee Wilbroad Slaa ana element hizo hivyo angefaa kuwa Rais.
Lakini kabla huyo aliyeitwa dikiteta Slaa hajaingia uwanjani kupambana aliaamua kuachana na Chama Cha CHADEMA kwa kudai kupokelewa kwa Mzee Lowasa Waziri Mkuu Mstaafu ndani ya CHADEMA ni sawa na kuhamishia choo chumbani unakolala.
Wakati huo CCM ilikuwa imekwisha mteua DKT JOHN MAGUFULI kuwa mgombea wao.
Baada ya CCM kushinda aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM kipindi hicho Mzee Jakaya Mrisho Kikwete moja ya maneno kwenye hotuba yake alisema , ‘’mlikuwa mnasema mimi mpole mpole hivi dawa ni kuwaletea mkali zaidi na ninasikia ameanza kutema checheeeeee”
Kwa tafsiri rahisi kutoka kwenye hotuba ya JK CCM haikuleta Rais dikiteta kama Watanzania walivyokuwa wanaomba mara zote, bali wao waliamua kuleta Rais mkali atakayesimamia sheria za nchi na kuilinda katiba ya nchi kwa nguvu zote.
Ndicho anachokifanya Rais kwa kuwa Tanzania ni Sovereign state. Kwa wasomaji wa vitabu munawezakusoma vizuri kwenye kitabu cha Hobbes moja ya wanafalsafa wa zamani kwenye kitabu chake kinachoitwa HOBBES’S MORAL AND POLITICAL PHILOSOPHY kwenye moja ya kurasa zake ameandika the state of nature is taste of war.
Mimi itakapofikia asilimia mia moja ya Watanzania wote wakaanza kumshangilia Rais Magufuli kuwa anafanya kazi nzuri nitamshauri ajiuzulu.
Nitamshauri ajiuzulu kwa kuwa nitaamini kuna mahali amekosea. Kiongozi anayefanya kazi zake vizuri hawezi kupendwa na watu wote, lazima wawewepo wa kumkosoa usiku na mchana hasa ukizingatia wapo ambao siasa ni fursa.
Tofauti ni kuwa wanaotetea fursa zao ni za ndani ya nchi na wanaopinga na kukosoa wanategemea zaidi shukurani toka nje.
Siku ikitokea watu wote wakamuunga nitaamini kuna kitu Rais amekosea anahitaji kujisahihisha au kuachia ngazi.
Nitaamini kuwa nguvu ya ndani imezidiwa na nguvu ya nje (MABEBERU). Na mara zote ili uweze kufanya kazi vizuri lazima wawepo wa kukukosoa, kukubeza na lazima wawepo vibaraka watakaokuwa wanajaribu kukukwamisha.
Nyerere alikwamishwa sana lakini hakukata tamaa(Rejea kundi la akina Ntuteke sanga). Ilifika mahali akatolea mfano kuwa ukigeuka nyuma utakuwa jiwe, wewe hata ukipigiwa kelele songa mbele usigeuke nyuma utakuwa jiwe(Nyerere voice).
Mzee Mwinyi hata yeye alikosolewa sana lakini baada ya kumaliza muda wake wale wale waliokuwa wakimkosoa walianza kumpongeza Mwinyi na kuanza kumkosoa Mkapa.
Waliokuwa wakimkosoa Mkapa baada ya Mkapa kumaliza muda ndio hao hao walimpongeza sana Mkapa baada ya kumaliza muda wake na kuanza kumkosoa Kikwete.
Hata hivyo waliokuwa wakimwita Kikwete dhaifu, Vasco Dagama ndio ambao wengine sasa ni wakosoaji wakubwa wa Rais Magufuli na wakisema wamemiss utawala wa Kikwete.
Hence Rais Magufuli don’t perturbed with such words, this is just normal for Tanzanian.
Tegemea shukrani zao kuanzia 2026 ukiwa unapumzika huko Chato. Muhimu endelea kuwasamehe na kuendelea kuwafanyia Watanzania mambo makubwa ili wakaendelee kukulilia ukiwa umeshastaafu.
Mungu alikuwa na uwezo wa kumumaliza Shetani lakini alimuacha na kumshusha huku duniani ili aendelee kushuhudia ukuu wa Mungu.
Mimi nitakushauri ujiuzulu kama Watanzania wote wataona mapinduzi ya barabara kwa miaka yako minne, wataona mapinduzi ya sekta za elimu, viwanda, afya, kilimo, usafiri wa anga na majini.
Watanzania wote wataona ulivyodhibiti nidhamu kazini, ulivyodhibiti rushwa, ulivyodhibiti safari za nje na utoroshaji wa madini lakini pia ulivyoongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi toka bilioni 800+ hadi 1.3+ billion kwa mwezi haitoshi kuhamia tu Dodoma ni imekuwa nongwa.
Ninatambua haya wengine si rahisi kuyaona kwa sasa si kwamba ni insanity, blind wala immature age rahasha wao wanasubiria umalize muda wako ili waanze kukumwagia sifa.
Wapo wanaoishi na kupata fedha kwa kugeuza kazi ulizofanya kuwa ni najisi. Yaani unachofanya wanakifanya kuwa kinyume chake.
Kadiri unavyochapa sana kazi ndivyo unavyozidi kuwabana vibaraka kwani wanajua unawabania riziki yao ya kesho.
Usitegemee kungwa mkono na watu wote, siku ukiungwa na watu wote ujue kuna mahali umekosea na hapo ndipo nitajitokeza kukushauri ujiuzulu.
Kwa sasa gia unayotumia ni sahihi.
“Africa is a paradox which illustrates and highlights neo-colonialism. Her earth is rich, yet the products that come from above and below the soil continue to enrich, not Africans predominantly, but groups and individuals who operate to Africa’s impoverishment”. KWAME NKURUMA