Nitamuita Shujaa wa Taifa Mbunge yeyote atakayependekeza kodi kwa Wabunge

Anza na kodi mshahara wa Rais kwanza awe mfano
 
Unajua hawa wabunge ni watu wa hovyo sana! Wanadhani huku mitaani kuna watu wasiowajua kabisaaa! Hili ni kundi lenye ubinafsi na upuuzi. Hawalipi kodi inayostahili halafu wanajidai kueleza umuhimu wa kulipa kodi.
 
Anza na kodi mshahara wa Rais kwanza awe mfano

Rais mara nyingi wana posho ,rais hata akipewa elfu 45 kwa mwezi hatoi hata 100 kujihudumia ,mahitaji yote yapo kwenye bajeti ya ikulu ambayo ni zaidi ya 900 bilioni kwa mwaka.
 
Swali mbona mshahara wake haukatwi kodi?

Kwani mshahara wake analipwa na nani? Maana nachojua ikulu ndio rais chochote anachotaka rais kinatekelezwa! Je bajeti ya ikulu inapelekwa wapi? Accounts za ikulu nani mwenye control DGIS au Sponsor?
 
Kila baada ya miaka mitano anakula milioni 300 kiinua mgongo hapo hujaweka maslahi mengine, ndiomaana wanakuwa mazuzu ilimradi tu hela yake aipate pindi muda wake unapoisha , yani ilitakiwa kama nchi zingine huko zilizoendelea kama mtu sio tajiri hakuna kuwa mbunge period, sio hawa wakwetu ambao ubunge ndio ajira
 
Hatmaye, shujaa niliyekuwa namtafuta amepatikana. Ni Mbunge Jerry Slaa ....!!

Kwa habari zaidi fungua link hapo chini.

 
Atakua verified akipeleka hii hoja bungeni.
 
Amepatikana shujaa na avikwe taji la Mbunge wa kitaifa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…