Uchaguzi 2020 Nitamwaga Sukari ziwa Victoria

Uchaguzi 2020 Nitamwaga Sukari ziwa Victoria

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2015
Posts
9,558
Reaction score
12,335
Pamoja na kuwa

1. Wamefanya siasa miaka mitano peke yao.

2. Wanajisifia kufanya makubwa kila siku

3. Wamejenga Flyovers.

4. Wamenunua ndege, uwanja wa ndege Chato.

5. Wanatupigia magoti kwenye kampeni.

6. Wanatupa Fiesta bure kila mkutano

Ila bado sijasahau

1. Sakata la vyeti feki, dhuluma

2. Utekaji nyara Roma na wenzake nautekaji mwingine

3. Kupotea kwa Ben Saanane, Azroy Gwanda

4. Kupigwa Risasi kwa Tundu Lissu

5. Kupigwa risasi kwa Akwilina

6. Kura hela za rambirambi Bukoba kisha kusutwa kuwa hajaleta tetemeko, hapangiwi.

7. Kunyang'anywa korosho kisha kutishia kupiga mashangazi.

8. Dhuluma uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

9. Kutishiwa kuwa tusipochagua CCM hatuletewi umeme wala maji.

10. Kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani.

11. Ubabe wa polisi kila siku.

12. Kufungiwa kufanya kampeni kwa Lissu, Mdee, Maalim Seif, Mayor Jacob na wengine.

13. Kufungiwa kwa magazeti.

Kwa hayo machache tu, halafu wanajitamba wataunda serikali iwe isiwe maana kupiga kura kwingine ni sawa na KUMWAGA SUKARI ZIWA VICTORIA.

Basi hata kama jina la Lissu wataweka mwisho, ukurasa wa 2 au wa 100, nitalifata hukohuko NIKAMWAGE SUKARI ZIWA VICTORIA [emoji41].
Uchaguzi 2020 - Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

IMG_20201016_143813_506.JPG
 
Back
Top Bottom