Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 40,828
- 99,523
Sawa mkuu.....Mwezi wa nane mwishoni alikuwa field
Naomba nikukumbushe ili kwa pamoja twende sawa pasipo hisia za kuonewa.
Wewe ulijiunga Jf tarehe 26 April 2018, na bilashaka ulijiunga kwa ID hii ya Lovehate ambayo inasadifu jambo lililo jificha nyuma yake yamkini ulijeruhiwa na mapenzi. Na hadi unajiunga Jf na unafungua ID hii maana yake ulikuwa una majeraha makubwa moyoni, ambayo pengine yamekuwa yakikupa maumivu kila wakati na kukufanya mwenye hasira na mpweke zaidi.
Ikiwa kama umeachwa mwezi April 2019 na huyu ulie mkabidhi moyo wako, yawezekana sana kwamba mwanzo aliamuwa kuku kubali na kukusaidi kwasababu alikuhurumia(hakukupenda) kutokana na pengine simulizi uliyo muhadithia kuhusu maumivu yako ya awali, na kwakuwa pengine wakati huo hakuwa kwenye mahusiano ndipo alijikuta anakuwa na wewe.
Yawezekana sana mpenzi wako amefikia hatua ya kukuacha kwasababu amekuwa akikuona ukitumia muda mwingi kukumbuka maumivu ya mahusiano yako ya awali (hata mimi naona hivyo) na hii hali haiku mfurahisha. Yawezekana umekuwa mnyonge zaidi kutokana na mahusiano yako ya awali, hali ambayo imepelekea asiione nafasi yake kwako.
Moja kati ya hizi sababu ndio zimepelekea mwenzako aamuwe kukuacha kwasababu haioni furaha kuwa na mahusiano na mtu ambae ni mjeruhiwa wa mapenzi.
Huo ni mtazamo tu, naomba usinikasirikie