Rayamikhal
Senior Member
- Sep 14, 2026
- 110
- 207
Habari za leo Jf. Nimewaandalia kisa kingine siku ya leo.
'Habari mimi ni kijana mtanashati mwenye muonekano wa pesa lakini kwa bahati mbaya mimi sina elimu ya juu, sina kazi ya maana sana kifupi Sina chochote ukilinganisha na muonekano wangu.
Wakati tumeamishiwa site mji x macho yangu yalimuona mwanamke mzuri na Moyo wangu ukampenda sana. Hali ya binti yule ilionekana ni Bora na hakuwa na shida za kimasikini kama mimi hapa. Wazo langu la kwanza nilipomuona lilikuwa ni kumuoa na kumfanya mke wangu kabisa.
Nilifanya njia zote ili nijiweke karibu nae, niliazimisha nguo kali kwa marafiki ili nimvutie na anione mwenye pesa na mvuto. Siku ya kwanza mazungumzo yanaendelea akaniuliza Mimi ni nani! Nilimjibu tu harakaharaka kuwa mimi ni profesa. Muda ukaenda akanikubalia kabisa nikaenda na kwao kujitambulisha.
Niliuza baadhi ya vitu vyangu geto pamoja na michango ya washkaji nikamchumbia mtoto kwa mahali ya million 1. Japo haikuwa kubwa kwao Ila nilikuwa nishamuandaa kisaikolojia mchumba kwaiyo haikuwa kazi ngumu. Walinipa mke nikaingia nae mpaka chimboni kwangu mkoa mwingine na kwao, naishi Nyumba ya kupanga na maisha ni magumu hata pesa ya kula tu ni mtihani.
Mke wangu hakusema chochote kile alikuwa tu ananiangalia anaishiwa maneno, muda umepita kama miezi 5 mke wangu akaniweka chini tuzungumze. Mke wangu akaniambia niseme Mimi ni nani kwa mara ya pili bado nikarudia kusema Mimi ni profesa jicho likiwa kavu kabisa.
Akasema kunavijana walikuja home na kumwambia wananidai laki 3 ambazo nilikopa wakati namsafirisha mke kuja kuja huku na pia alisema wale jamaa wamesema Mimi kazi yangu ni vibarua tu wala sijasoma kivile na wenyewe wanashangaa kwanini nilioa. Mimi namwambia Nini binti wa watu na kumuacha siwezi kabisaa maana nishampenda? '
Guys, kisa ni hicho 😂 kiukweli nilipokisikia kwa Mara ya kwanza nikasema tu kwa hali hii kuolewa itachukua muda sana maana utapeli umekisiri. Nahitaji mawazo yenu guys! Huyu anaejiita mtanashati sijui tumfanye nini kwanza maana nishachanganyikiwa.
~rayamikhal