Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,199
Ndugu wanaJF, nimeanza kuwasiliana na baadhi ya maadvocate kuona ni kwa vipi tunaweza kumwekea pingamizi Kikwete asigombee Urais kutokana na sababu zifuatazo:
Sababu ya kwanza Inatokana na afya ya kimwili na kiakili ya mgombea huyu: Afya yake ni yenye mashaka makubwa kiasi cha kwamba inatia shaka kama ataweza kuwa kiongozi mzuri na makini katika muda wa miaka mitano ijayo.
Afya ya mwili: Tuna kumbukumbu ya kuanguka jukwaani kwa zaidi ya mara tatu pasipo maelezo yoyote ya msingi yanayotolewa juu ya kuanguka kwake. Kwa kuwa ni nadra kwa binadamu yoyote asiye na maradhi ya kifafa kuanguka mbele za watu, na kwa kuwa Kikwete hana kifafa, naamini ya kwamba ana matatizo makubwa ambayo ni zaidi ya kifafa, na hivyo hataweza kusimamia majukumu makubwa ya kuiongoza nchi.
Afya ya akili: Kutokana na ahadi mfululizo zinazotolewa na mgombea huyu kupitia CCM, kuna dalili za wazi kwamba hayupo katika hali yake ya kawaida ya kufikiri kabla ya kusema. Tangu aanze kampeni ameshaahidi kununua meli kadhaa, na kujenga viwanja viwili vya ndege vya kimataifa zaidi ya kile cha Dar es salaam ambacho kinatia aibu kukiita kiwanja cha kimataifa.
Mgombea huyu:
Kwa ahadi kama hizi napata wasiwasi kwamba Mgombea uraisi huyu si mzima (ana tatizo la akili). Amesahau mengi aliyoshindwa kuyatekeleza wakati ambapo serikali ilikuwa na pesa za kutosha (kwa mfano kujenga reli kutoka Mtwara hadi mbeya) na sasa anaongelea utekelezaji wa ahadi nyingine ambapo nchi inaendeshwa kwa madeni. Ataweza vipi? Kwakuwa katiba inasema Rais mgonjwa wa kimwili au kiakili anapaswa kusimamishwa, basi naona ni vema akasimamishwa kabla hajaingia Ikulu na kutusababishia hasara hapo hali yake ya afya itakapozidi kuwa mbaya na kulazimika kufanya uchaguzi mwingine.
Sababu ya pili ya kumpinga mgombea wa CCM ni kwa sababu ya udhalilishaji mkubwa uliofanywa na chama chake kupitia kwa katibu wake Mkuu Yusuf Makamba,na magazeti ya serikali dhidi ya mgombea wa CHADEMA juu ya ndoa yake na upadri. Kauli za Yusuf Makamba na kejeli za magazeti ya serikali dhidi ya Dr Slaa, yamemshushia utu na heshima yake mbele ya jamii jambo ambalo halikubaliki kisheria. Kwa kukiuka sheria hii ya usawa wa binadamu na utu wa mtu, hawastahili kuiongoza nchi.
Nina tuhuma nyingine Lukuki dhidi ya mgombea huyu ambazo baadhi ya mawakili wanaendelea kuzipitia kuona kama zitaweza kutumiwa kama kigezo cha pingamizi hilo.

- ameshindwa kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kasi jijni dar es salaam katika muda ya miaka mitano aliyokuwa madarakani,
- ameliua shirika la ndege Tanzania ATC.
- Ameshindwa kuanzisha usafiri wa uhakika wa reli nchini,
- ameshindwa kuimarisha miundombinu ya barabara vijijini na mijini ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kupunguza adha ya kusafirisha mazao hayo kwenda sokoni (Na kwa bahati mbaya au nzuri barabara ndiyo tegemeo kubwa zaidi la usafiri kwa watu wa hali ya chini),
- ameshindwa kumalizia uwanja wa ndege wa kimataifa ulioanza kujengwa Songwe Mbeya wakati wa Mkapa,
- ameshindwa kukamilisha mipango ya Mkapa ya kupanua uwanja wa ndege wa JK nyerere ambao mipango yake ilianzishwa na Mkapa tangu 1997,