Nilishakutana na case kama hiyo, na hata ku-format ilikuwa inagoma. Ukifikia umeamua kuzitosa hizo data, na ukijaribu ku-format pia ikashindikana, fuata ushauri huu:
- Disconnect Hard-drives za computer yako
- Boot computer kwa kutumia Windows XP CD (Sijajaribu CS ya Vista)
- Fuata instructions kama vile unataka kuinstall OS kwenye hiyo flash. Ikifika sehemu ya kuchagua drive, chagua hiyo flash, na iambie installa ii-format
- Ikimaliza kuformat, disk yako iko safi. Baadaye nadhani setup ita-fail anyway kwa sababu space ni ndogo
- Zima computer
- Unga hard-drives zako ulizozitoa kabla
Nimekumbuka sasa kwamba kama una flash inayogoma hata ku-formatiwa kwenye XP kwa sababu ilichomolewa bila kufuata taratibu, ukiiingiza kwenye Vista, Vista ina-gundua kwamba hiyo flash ina matatizo na itakuomba ruhusa ya kui-fix. Ukiiruhusu itaifix na nadhani ma-fie yako yanabaki vile vile. Jaribu hili kama jaribio la mwisho kama ushauri wote hapo juu umeshindikana.