Nitaondokana vipi na tatizo hili?

Nitaondokana vipi na tatizo hili?

Mchumia Rungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
1,438
Reaction score
826
Hi all!

Nina tatizo la usingizi. Kila ikifika saa 4:00 usiku ni lazima nipatwe na usingizi mzito kiasi kwamba wakati mwingine hushindwa hata kuosha kinywa changu kabla ya kulala!

Na jinsi mwili unavyokuwa umechoka, hata inanilazimu kuto kumpa wife haki yake ya chakula cha usiku. Nashukuru wife ameshafika point ya kunielewa kwa hilo.

Lakini nataka kuanza masomo ya elimu ya juu, hakika kwa usingizi huu naamini nitashindwa shule hii. Niliwahi kufika hospitali, nilijibiwa hakuna tatizo ilihali najiona nina tatizo.

Tadhali wataalam nipeni mawazo, nitaondokana vipi na tatizo hili la usingizi? Kama kuna dawa Niambieni ili nijaribu jaribu la kuitumia pengine nitapona.
 
Dawa ya usingizi ni kulala
Au kutokana na kazi zako labda unachoka sana
Jaribu kupanga ratiba yako vizuri na ufanye mazoezi
Mazoea ndio hujenga tabia
 
Dawa ya usingizi ni kulala
Au kutokana na kazi zako labda unachoka sana
Jaribu kupanga ratiba yako vizuri na ufanye mazoezi
Mazoea ndio hujenga tabia

Nashukuru kwa ushauri wako hasa huo wa mazoezi. Kwa hakika mazoezi nilishaacha miaka mingi kutokana na mazingira ninakoishi ni mbali na ninakofanyia kazi. Naondoka saa 12:30 asubuhi na ninarudi saa 2:00 usiku. Hapo swala la mazoezi kweli ni zero. Unafikiri naweza kufanya mazoezi gani hapo kwangu tena usiku? Kulala mchana haiwezekani kama mazingira yangu ya kazi yalivyo si rafiki.
 
jilazimishe kuamka saa 11 fanya mazoezi ndio uoge uende kazini..
 
Nashukuru kwa ushauri wako hasa huo wa mazoezi. Kwa hakika mazoezi nilishaacha miaka mingi kutokana na mazingira ninakoishi ni mbali na ninakofanyia kazi. Naondoka saa 12:30 asubuhi na ninarudi saa 2:00 usiku. Hapo swala la mazoezi kweli ni zero. Unafikiri naweza kufanya mazoezi gani hapo kwangu tena usiku? Kulala mchana haiwezekani kama mazingira yangu ya kazi yalivyo si rafiki.
Nunua kamba ya mazoezi ukiamka kila siku uruke asubuhi mara 50 mpaka 100 hope utajiskia poa
 
tatizo ni kazi ngumu na sidhani kama unakunywa maji mengi.pia size ya mwili wako kama ni bonge ndo majanga.
ukubwa majanga, zingatia ushauri huu
 
Back
Top Bottom