wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Elimu sio kusoma tu, kuna mazingira ya kusomea, walimu kusaidia wanafunzi, teknolojia, n.k.
Kusomesha mtoto ni kumweka katika mazingira salama ya kusoma, awe na walimu wanaotimiza wajibu, kujifunza kwa lugha za kimataifa tangu mdogo, n.k.
Ni kweli kuna watoto wana akili zao hata wakisoma shule zisizo na walimu wanafaulu lakini wakipelekwa shule za private kuna mazingira ya kuwafaulisha zaidi, hata wanafunzi wanaofanya vibaya shule za serikali wakipelekwa private kuna uwezekano mkubwa wa kuboresha ufaulu wao sababu kuna msaada zaidi kuoka kwa walimu, vitabu, mazingira, n.k. Kwa ushahidi usio na shaka, wanafunzi wengi wa private wanafaulu kuliko wa shule za serikali (nje ya vipaji maalum)

| VYOO |
| Private wanajitajidi sana kwenye usafi wa vyoo, wapo waajiriwa wa kusafisha vyoo |
| Shule nyingi za serikali vyoo ni vichafu sana, kuingia chooni kukuta mlima ni kawaida |
| UWAJIBIKAJI WA WALIMU |
| Shule nyingi za private kuna walimu wa kutosha na wanafuatiliwa kuingia darasani kufundisha kila kipindi |
| Walimu wengi wa serikali wamesharidhika na kazi ya kudumu, kukosa vipindi ni kawaida, mwanafunzi kupasua awe kajiongeza sana |
| LUGHA |
| Shule za private kujifunza zina utaratibu wa kutumia kiingereza tangu chekechea, wakifika form one washazoea |
| Shule nyingi za serikali wanatumia kiswahili, ni mpaka form 1 wanatumia kiingereza |
| COMPUTER |
| Shule nyingi za private zina madarasa maalum ya computer |
| Shule nyingi za serikali hata kukuta zina umeme ni muujiza, achilia mbali computer |
| MRUNDIKANO MADARASANI |
| Shule za private darasani hakuna kurundikana, ni rahisi mwalimu kumsaidia kila mwanafunzi |
| Shule nyingi za serikali kuna mrundikano usipime, Mwalimu anakazia wale wenye uwezo tu |
| MZAZI/MLEZI KUPEWA TAARIFA |
| Shule za private wanajitahidi kukupa taarifa za maendeleo ya mtoto hata masuala madogo |
| Shule nyingi za serikali kupata updates za mtoto labda liwe tatizo kubwa sana |
| USALAMA |
| Shule za private nyingi zina fensi, geti na mlinzi |
| Shule nyingi za serikali hakuna fensi, mlinzi wa mchana wala geti |
| MADAWATI / VITI |
| Shule za private kila mwanafunzi ana dawati na kiti chake |
| Shule nyingi za serikali dawati moja wanafunzi wawili, viti changamoto |
| ADHABU KWA WATOTO |
| Shule za private nyingi hutoa adhabu kwa kuzingatia vipimo sahihi |
| Shule nyingi za serikali walimu hawana mipaka ya adhabu, mwanafunzi anaweza kucharazwa viboko 30, kubebeshwa matofali kibao, n.k. |