Nitapata wapi mtu wa kudhamini wazo langu la kibiashara?

Nitapata wapi mtu wa kudhamini wazo langu la kibiashara?

Kwa mfano mimi nawaza kuanzisha kilimo cha matikiti maji,napaswa kulipia hili wazo au nikishaanza kulima ndo nalipia mbegu na madawa na kadhalika?

Wazo halilipiwi mkuu, na suala la mbegu na madawa malipo kabla au itategemea na mipango na makubaliano utakaofanyika na wadau
 
nitafute nikuandikie business plan na project proposal irakayokuwezesha kukubalika na kudhaminiwa wazo lako.
Keshakuambia idea yake hampi mtu yeyote wanaweza iba. Sasa wewe unataka kaandika kabisa je atakuamini vp kama hutoiba halafu ukauza? On my opinion, nadhani kila mtu ana idea flani, ila kimbembe ni kwenye financial. Ni bora angeingia ubia na mtu kuliko kutaka apate yeye tu. Duniani ya sasa ni win win situation
 
Andaa business plan nzuri na proposal za kutosha. Onesha jinsi mdhamini atakavyonufaika na faida atakayopata kutokana na uwekezaji wake. Siku hizi hakuna anayetoa fedha hivi hivi, hata Mengi au Bakhresa nao wangependa kupata chochote kutoka kwenye huo udhamini watakaokupa.
Pia jua kwamba idea kila mtu anayo, na hao wadhamini wanapelekwa idea na maombi mengi - Andaa idea nzuri zaidi na fanya presentation nzuri zaidi.
Unaweza ukaanza kwa kutumia nguvu na rasilimali ulizonazo mwenyewe kwanza, kisha kumuomba mfadhili au mdhamini akusaidie kukuza na kuendeleza. Ni rahisi zaidi kumsaidia mtu ambaye ameshaanza chochote kuliko mtu ambaye ana wazo tu lakini hajaanza chochote.
ANZA NA ULICHONACHO

Mkuu umenene vema kabisa.Sote tumefanikiwa Kwa ukarimu wako.Ubarikiwe sana tu
 
idea inaendana na implementatio ambazo unajua wewe na soko lako unajua wewe siri yako..

hata mtu akikuiga hawez fanikiwa...

mfano wazo lako likiwa kufuga sungura... hakuna anaeweza kukuibia sababu hao sungura wewe ndio unaejua utawapata wapi na kuwafugia wapi na kuwauzia sokoni wapi..

mi nakushauri usiogope kutoa mawazo yako.. sema uyatoe juu juu tu sio ile deep
 
Naomba nikuite dogo kwa sababu kwenye hii fani ya ujasiriamali unaonekana ni amateur.

The name of the game is capitalism, kwa kifupi you need capital to play the game na kama hauna mtaji na haujui jinsi ya kuraise capital basi we utaendelea tu kuwa mtazamaji.

Inasikitisha sana kuona mtu unataka kuwa mjasiriamali lakini haupo tayari kujifunza, kwa nini nasema hivyo? Kama ungekuwa tayari kujifunza natumai mpaka sasa ungekuwa umetembelea angalau mabenki sio chini ya matano na kujua kwamba hakuna benki nchini inayokopesha a start up business achilia mbali an idea hata uwe na dhamana yenye thamani kiasi gani.

Umezidi kunishangaza pale unapotaka kukopeshwa kirahisi na mtu binafsi bila ya dhamana na sijui hautaki achukue faida, na riba vipi asiweke? Sitaki kukutisha tamaa lakini naomba ujue kama unataka kuwa mjasiriamali basi lazime ujifunze how to raise funds.

Kuna angel investors wanaweza kukusaidia if you are lucky, if you are not lucky basi jaribu venture capitalist kama kweli your idea is really that good and worth their time and money, wapo humu.
Na kimsingi kuna njia kuu tatu za ku-raise capital,
1: Self efforts(EQUITY),
2: Borrowing
3: Share selling

Cha kushangaza sijui ni kwanini mtoa mada kakimbilia kupewa pesa za mtaji badala ya pia kufikiria kutumia juhudi binafsi na au kuuza hisa.

Vigezo vya kukopeshana vinapatikana katika formular hii:-
C.A.M.P.A.R.I. Kama unavyo hivyo vigezo unaweza kopeshwa na Bank au mtu yeyote.
Mi namshauri, ni bora kama ukipambana mwenyewe katika kupata mtaji badala ya kufikiria kuwezeshwa na watu wengine. Tumia nguvu, akili, talents, elimu, juhudi zako, maliasili zinazokuzunguka, na fursa zanazokuzunguka ili kupata mtaji.
 
Keshakuambia idea yake hampi mtu yeyote wanaweza iba. Sasa wewe unataka kaandika kabisa je atakuamini vp kama hutoiba halafu ukauza? On my opinion, nadhani kila mtu ana idea flani, ila kimbembe ni kwenye financial. Ni bora angeingia ubia na mtu kuliko kutaka apate yeye tu. Duniani ya sasa ni win win situation
ingekua ni hivi tusingekua tunafanya kazi za watu,
na katika kupata financial aid muhusika atahitaji kuona mpangilio utakao mshawishi,
Je mtoa mada ana utaalamu wa kuweka wazo lake katika mpangilio ikamshawishi mtu kumsaidia?
kama sivyo umuhimu wa muandishi wa business plan unarudi pale pale,
mimi siuzi wazo la biashara nauza huduma ya kukuandalia mpangilio wa wazo lako la biashara.
 
wakubwa shikamoo na wadogo zangu habarini!

Nina wazo la kibiashara na kwa hapa Dar es salaam sijaona kitu kama hicho.

Gharama ya kukamilisha hili wazo kuwa biashara halisi inahitajika kuanzia milion 3 mpaka 4. Tatizo ni kwamba mimi sina kiasi hicho cha fedha kwa sasa! Pia wazo lenyewe hili la kibiashara linaweza kuonekana kama ni small scale ila likidhaminiwa vizuri (mtaji ukiwa mkubwa) linaweza kuwa large scale!

sasa je wapi naweza kupata mtu wa kunidhamini?

a) bank wanaweza kunidhamini bila ya mimi kuwa na dhamana kama nyumba au ardhi?

b) je mtu binafsi anaweza kunidhamini bila ya kuhitaji asilimia katika faida? mimi kwa hapa nahitaji mtu akinidhamin labda kama mkopo nimlipe kidogo kidogo malipo ya mkopo ila akinidhamin kama msaada nitashukuru zaidi.sijapenda ya kushare profit kwa sababu bado mradi unakuwa haujasimama vizuri


kama kuna mtu ana uzoefu na hali kama hii naomba msaada wenu tafadhari.

nawasilisha!
Marhabaa
Haya mambo mtangulize Mungu sana.
Vijana kama wewe waligundua M pesa
wakaomba udhamini
waliowadhamini wakaichukua ile dili mpaka leo wale vijana ni maskini.
 
mwaga hapa mlolongo ili mtu kabla ya kukupa ajitafakari kwanza / na apime POSSIBILITIES OF FUNDS RETURNS.
 
Maelezo meengi,lakini unazunguka tu. Weka hiyo idea ijulikane.

Pia punguza ubinafsi,yani mtu akudhamini mtaji alaf faidi iwe yako alone??

Grow up!.
 
ingekua ni hivi tusingekua tunafanya kazi za watu,
na katika kupata financial aid muhusika atahitaji kuona mpangilio utakao mshawishi,
Je mtoa mada ana utaalamu wa kuweka wazo lake katika mpangilio ikamshawishi mtu kumsaidia?
kama sivyo umuhimu wa muandishi wa business plan unarudi pale pale,
mimi siuzi wazo la biashara nauza huduma ya kukuandalia mpangilio wa wazo lako la biashara.
Maisha ya sasa hivi yamebadilika sana. Kila kitu hufanyika in a participatory approach. Kwa sababu mtu mmoja huwezi jua kila kitu hivyo uhitaji msaada stakeholders mbalimbali ni muhimu
 
Jaribu kuweka idea yako,not detailed,ili upate mawazo kwa watu tofauti tofauti yatakupa mwanga flani,hata Kama mtu akiiba hiyo idea hataifanya Kama vile unavyotaka kufanya wewe na possibility ya kushindwa ni kubwa,usiogope...Pia jaribu kuanza kuiimplement hata kwa kiwango kidogo ndio itakuwa rahisi kupata msaada wa mtaji wa kuiendeleza zaidi.
 
Usithubutu kuweka wazo lako, watakuibia! Nenda mpelekee Mzee Mengi, peleka kwenye mabenki na tafuta watu Ila usitoe wazo lako, utajuta, naongea kwa experience
kani akiwapa benki au meng atakua ajatoa wazo?acha uchoyo wa kuwabania JF member .atoe wazo tulichanganue naye ataongeza ujuz zaid
 
Ushauri:-
Kwa kuwa Na wazo bila mtaji ni muujiza kuanza kusonga. Fanya utafiti kidogo ktk mabenki Na taasisi mbalimbali za kifedha kujionea Na kujiridhisha juu ya interest zao.
Pia,ni biashara Gani inayohitaji mtaji halafu usitoe riba au gawio la Faida,nafikiri unahitaji kujipanga upya Na ukubaliane Na suala la kurejesha sehemu ya Faida Kw a mtoa mtaji otherwise itahangaika sana humu kwani MTU kukupa Tu kama grant itakuwa ngumu..
 
Usithubutu kuweka wazo lako, watakuibia! Nenda mpelekee Mzee Mengi, peleka kwenye mabenki na tafuta watu Ila usitoe wazo lako, utajuta, naongea kwa experience
Tupe uzoefu kuhusu mahali yalipo yale mawazo aliyopelekewa Mengi na manufaa waliyopata waliobuni mawazo yale?
 
Jidhamini mwenyewe kijana,kwa mjasiriamali wakisasa milioni tatu sio hela ya kuja kutafuta wadhamini,anza na ulicho nacho then nyengine zitapatikana mbele ya safari,na hakuna idea ya siri mzee,hakuna biashara utafanya peke yako,labda iwe hailipi.lakini hata idea yako iwe nzuri na inovative kiasi gani lazima soko litahitaji washindani.kwakifupi una mengi ya kujifunza.
 
Hhahahahahahaa nyie vijana mnachekesha sana. Nashukuru wakubwa zenu baadhi wamewaelekeza jinsi ya kupata mtaji. Hauwezi kupata bila kupoteza,na hauwezi kufanikiwa kwa kujifungia ndani eti "nina wazo zuri naogopa wataniibia" thubuuutu. Hakuna wa kukupa hela bureeee eti hautaki apate faida. Kama hautaki apate faida yeye si ataenda kuweka hela yake sehemu atakayopata faida. Wazo zuri jipya la biashara tena kwa anayeanza haliwezi kuwa la kurudisha mtaji kwa haraka labda kama unataka kuuza mihogo na kwamba badala ya kuuzia manzese sasa unaenda kuuzia masaki. Grow up,mambo yamebadilika sana. Uza hisa kwa wenye mtaji mfanye nao kama unataka kufanikiwa la sivyo endelea kujifungia ndani kwa ubinafsi wa kutaka kupata vyote. Yaani idea tu wewe unagoma kutoa halafu hapohapo unataka hela bila masharti......
 
Back
Top Bottom