Juzi tu Mzee mmoja wa kibongo ka-staafu alikuwa mwajiriwa huko Botswana nikamwuliza khali ya ajira huko vipi? Kasema mambo mazuri yapo hapahapa Bongo,Botswana si ile ya zamani wamesomesha wana wataalamu wa kutosha ajira si bwerere kama enzi hizo! Nikamwuliza mzee mbona huko maisha mazuri na mishahara nasikia iko juu? Akajibu Mishahara mikubwa pia matumizi ni makubwa hakuna ndizi ya sh 200 kama Bongo ndizi moja sawa na buku ya kibongo,vitu vingi wanaagiza toka nje.Labda uwe single utaweza mudu maisha lakini kama unategemewa na familia au ukoo,utakuja rudi Bongo huna hata kiwanja.
Ahsante.