Nitapataje mafunzo ya urubani hapa Tanzania

chilubi

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
8,188
Reaction score
6,244
Habari zenu wakuu.... Juzi natizama taarifa habari ITV nakumbuka kama nimeskia kuwa kuna chuo kinatoa mafunzo ya aviation na masomo yanaanza august, kwa wale wenye taarifa naomba mnijuze nijue ni chuo gani, jina limentoka.
 
usintake vyuo vya hapa nchi maana sisi kwa kuchakachua hatujambo usije ukaangusha ndege.
chuo kipo uwanja wa ndege dar afa ml. 30
 
ni kweli chuo kipo tabata magengeni crdb bank ghorofa ya 2.
 
hiko chuo kipo waliwahi kuja ofisin kwetu na form za kama mtu anataka kujiunga na chuo akasomee mambo ya aviation waliacha ..... ukiweza nikumbushe on Tuesday nikutumie zile brochures zao.
 
Sio kile chuo kilichojifanya kinatoa mafunzo ya urubani kisha TCAA wakatoa tamko kuwa hakijasajiliwa kufundisha uruban?
 
usintake vyuo vya hapa nchi maana sisi kwa kuchakachua hatujambo usije ukaangusha ndege.
chuo kipo uwanja wa ndege dar afa ml. 30

Mil. 30 private pilot license au mpaka commercial pilot license
 
aviation studies ni pana hata nit wanataka kuanzisha ila hayo ya upilot sijui
 
Mil. 30 private pilot license au mpaka commercial pilot license

30 Mil fo PPL,CPL itazidi hapo,na vyuo vya hapa havitoi CPL,yampasa mwanafunzi aende South afrika au kwingineko,wale jamaa wa Tabata magumashi,nenda old Terminal kuna fying school inaitwa Moswood frying school,au zenj Tropical frying school..
 
http://www.tcaa.go.tz/news_detail.php?news=1924

link hiyo kuhusu chuo cha Tabata
 
private pekee! commercial nenda amerca mkuu

Kwenye website yao wameonyesha kwamba wanatoa leseni zote mbili private na commercial. Kwa maelekezo yao, ofisi zao zipo terminal 1, uwanja wa Mwl. J.K Nyerere. Wataanza September kutoa mafunzo.

Tiba
 
30 Mil fo PPL,CPL itazidi hapo,na vyuo vya hapa havitoi CPL,yampasa mwanafunzi aende South afrika au kwingineko,wale jamaa wa Tabata magumashi,nenda old Terminal kuna fying school inaitwa Moswood frying school,au zenj Tropical frying school..

Hawa tropical nlikwenda kama 2years back wakanambia wamefunga flying school, au mkuu umeskia saiv wamerudi tena? Zenjy kipo cha Zenith lakini nna friend wangu imemchukua 2years kwa ppl sasa naona mda mrefu kwa course ambayo ni ya 3-6 months, na kipo ZRP lakini hawatumii cessna wanatumia lightaircraft ambayo nimeskia ukimaliza lazima urudi kufly cessna....
 
Kwenye website yao wameonyesha kwamba wanatoa leseni zote mbili private na commercial. Kwa maelekezo yao, ofisi zao zipo terminal 1, uwanja wa Mwl. J.K Nyerere. Wataanza September kutoa mafunzo.

Tiba

Mkuu icho chuo kinaitwaje? Nataka jina, kisha nliskia kuhusu NIT vipi hawa jamaa wao bado kuanza kufundisha urubani?
 
Hawa jamaa wanaitwa Tanzania Pilot Training Centre na website yao ni www.flymwaa.com. Kuhusu NIT, kwa kweli sijui lolote kuwahusu.

Tiba
 
Back
Top Bottom