Nitapataje mkopo? Dhamana yangu ni nyumba

Nitapataje mkopo? Dhamana yangu ni nyumba

Lugha baba!!
Dhamana ya kwanza ya mkopo ni

1. Uwezo wa kulipa

2. Nia ya kulipa

Hakuna benki au taasisi yoyote ya fedha itaweza kukukopesha kwasababu tu eti unadhamana ya nyumba. Lazima uwe na biashara au wazo la biashara( taasisi chache sana kama zipo ndio zinakubali kukopesha wazo au biashara zinazo anza).

Kama sio hivyo basi lazima uwe muajiriwa wa taasisi rasmi iliyosajiliwa na unalipwa kwa uhakika mshahara wenye kueleweka na hiyo benki au taasisi ya fedha iwe na sera na bidhaa(product) ya kukopesha waajiriwa

Baada ya yote hayo ndio inafuata suala la kuweka dhamana mali inayokubalika kuwekwa dhamana na benki husika. Kila taasisi ya fedha ina sera ya kukubali kupokea aina ya dhamana. Kuna wengine wanakubali nyumba au viwanja vyenye hati kubwa(title deeds), wengine leseni za makazi na wengine hata hati za mauziano tu. Wengine hawakubali kiwanja kitupu hata kiwe Kariakoo au Masaki. Lazima kuwe na jengo hata likiwa dogo au bovu. Wengine wanapokea hata magari au mashine

Kuna dhamana nyingine ina nguvu sana, dhamana ya pesa taslimu. Hii maranyingi inakua kwenye mabenki na unatakiwa uweke pesa kwenye akauti ya muda maalumu(fixed deposit) kisha unaweza kukopeshwa hadi asilimia fulani ya pesa ulizoweka kutegemea na sera za benki husika. Tena bank zingine ukiweka cash wanapunguza mlolongo wa taratibu(procedures)
 
Kumbe huwa mnatufanyi kusudi eeh!!
 
Kumbe huwa mnatufanyi kusudi eeh!!
Banks zipo kwa ajili ya kutengeneza faida, sio kwa ajili ya kisaidia shida za watu. Utakapo kia umepambana na kupata mtaji au una biashara yenye mafanikio tayari basi watakua rafiki yako wakidai hapo sasa wanataka "kukusaidia". Ukianguka ki uwezo wa kipesa wanakukimbia kama corona
 
Uchumi wa dunia unapita kwenye majaribu, Watu wanafikiri kubadili pesa kuwa nyumba, viwanja, na asset nyingine. Kuwa makini maana Upo njia tofauti.
 
"akanishauri kama nataka pesa nzuri nisiuze kwa mtu bali niende benki nichukue mkopo watanipa pesa nzuri then niwe kama vile ndo nimeiuza baada ya kuchukua huo mkopo."

Hii technic mabenki wengi washaistuka...
Siku hizi kama unaweka dhamana nyumba wanataka ile unayoishi kabisa...

Cc: mahondaw
 
Ahsanten kwa mawazo yenu, mmenifungua pakubwa, Nimeamua kutochukua huo mkopo kwanza na pia nimeahirisha kuiuza nyumba kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi kupewa mkopo bila kuwa na kazi au biashara! Wanachoaangalia una nini cha kukufanya ulipe! Lengo la benki siyo kuuza nyumba ...kwahiyo dhamana pekeee haiwezi kukupa mkopo maana itakuwa kama unawauzia
Ni kweli kabisa,lengo la benki ni kumuendeleza mteja sio kumfilisi,ukienda benki utaeleza malengo ya mkopo(biashara) na kiasi cha mkopo unachohitaji,
Benki itakuja kutembelea biashara na dhamana yako ili kuona kama inaendana na kiasi cha mkopo unaoomba.
Kisha utapewa ushauri kulingana na hali waliyoiona kwenye biashara yako sambamba na kuridhia kiasi ulichoomba au kukipunguza.Pia utatakiwa kupeleka vielelezo mbalimabali kama vile leseni ya biashara,tini namba na tax clearance.
Kwa ujumla,ni mchakato ambao unaweza kuchukuwa mwezi mzima au miezi kadhaa
 
Back
Top Bottom