Tafuta memba wawili wa gymkhana wakudhamini kwenye fomu yako, halafu ukishaipeleka jina lako linawekwa kwa notice board. kama kuna memba ana kikwazo atakipeleka kwa wahusika, kama hamna unaitwa kwenye interview, ni fomaliti tu hakuna anayefeli. Kisha ukipita unalipia entrance fees, ziko juu kidogo, about 750k. Ila baada ya hapo ada kwa mwaka ni 178k kwa single memba, kwa family memba sijui.
Kwenye golf lazima upate pro golfer akufundishe, wanachaji 15k per session. Unahitaji kama 10 sessions hivi unakua tayari kucheza. Halafu kuna kulipia green fees kila mwezi elfu 10 na caddy (kijana wa kubeba golf bag yako uwanjani) elfu 5 kila siku unayocheza.
Kama una lingine uliza