Nitashangaa kama serikali haijaandaa "VIONGOZI WA MAANDAMANO". Gwajima au Polepole wangefaa sana. Hao ndiyo wana ushawishi pande zote

Common Folk

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
909
Reaction score
4,050
Ulishajiuliza kwa nini Kenya Gen Z walikuwa wanaandamana huku wakiwa na viongozi ila serikali haikuwa inawakamata hao viongozi (wanaharakati)?. Kenya kwa sasa iko shwaaariii!

Jibu ni kwa sababu ni rahisi ku-contain maandamano yenye viongozi kuliko yasiyo na viongozi. Leaderless demonstrations ndiyo ngumu zaidi duniani kuikabili na kuweza kufikia muafaka wa muda mrefu.

Serikali hii ya CCM ni kama wanaishi kisiwani hawaelewi na hawataki kujifunza mbinu zinazofanya kazi kwenye changamoto kama hizi.

Viongozi wa juu wamekalia kufanya propaganda za kipumbavu zisizo na mantiki yeyote kwa mtu mwenye akili.

Na ukweli ni kwamba hata kama watu hawatatoka barabarani, ila maandamano yameshafanikiwa kwa 90% mpaka sasa. Hilo linathibitishwa na "MAIN TOPIC" midomoni mwa watu nchi nzima kwa sasa ni #D9, huko mitandaoni ndiyo usiseme, ingia social network yoyote post ya kwanza unayokutana nayo ni MAANDAMANO YA #D9.

Nchi yote kwa sasa iko busy na D9. Serikali iko busy na D9. Vyombo vya ulinzi viko busy na D9. Taasisi zote za serikali ziko busy na D9. Watalii wamekimbia nchi sababu ya D9. Dunia nzima macho yote yako Tz sababu ya D9.

Ningekuwa nina maamuzi hapo juu ya kiserikali, basi ningeshamset Gwajima awe pale mbele ili iwe rahisi kufanya negotiations na Gen Z.
Your browser is not able to display this video.
 
Wanaamini katika ubabe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…