Nitashangaa sana kuona wafuatao wakirudi katika nafasi za Ukuu wa Mkoa

Nitashangaa sana kuona wafuatao wakirudi katika nafasi za Ukuu wa Mkoa

Sultani Makenga

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
621
Reaction score
1,039
Binafsi nimpongeze mama yetu Rais wa JMT Samia Suluhu Hassan kwa kuanza kazi vizuri na kikubwa zaidi alichonifurahisha ni kuwataka viongozi katika Serikali yake kutumia akili katika kuongoza watu badala ya mabavu, ni jambo jema kwa kweli.

Kaanza kwa kutuletea VP Mpango, kateua mawaziri na juzi tu kateua makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu.Ili safu ikamilike kama yeye alivyosema leo, uteuzi wa maRC,maDC na maDED utafuatia, binafsi simpangii mama watu wa kufanya naye kazi ila mimi kama Mtanzania nina haki ya kutoa maoni na katiba inaniruhusu kufanya hivyo sharti nisivunje sheria tu. Katika uteuzi wa maRC nitasikitika Sana ikiwa nyuso za watu wafuatao zitarudi maana hawa watu ni zaidi ya kero;

1. Loata Sanare - RC Morogoro.
Huyu hatumii akili hata kidogo ni mabavu kwa kwenda mbele.Ukisikia mtu anayeua nzi kwa nyundo ndio huyu. Mwaka jana aliamuru wenyeviti wa Vitongoji wawekwe ndani kisa hawajahamasisha shughuli za maendeleo.Watu wenyewe hawana mishahara wala posho, badala ya kusaidiana nao kutatua kero yeye anaamuru waswekwe ndani kisha anawasha gari kurudi mjini kuponda raha. Huu ni uonevu wa hali ya juu kisa madaraka. Baada ya kuteuliwa huyu jamaa migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ndio imepamba moto maana ana favour watu wa kabila lake wamasai, migogoro ya namna hii ilipungua kwa kiasi kikubwa kipindi Kebwe S. Kebwe akiwa RC.Huyu arudi kukitumikia chama tu(CCM)kama ilivyokuwa huko awali, hafai kuwa RC.

2. Godfrey Zambi - RC Lindi.
Huyu naye anaamini katika ubabe, suala la Elimu tu Lindi limemshinda ukiacha mambo mengine na tatizo kubwa ni ubabe.Huyu kuna muda hutembelea shule na kuwakagua walimu madarasani, hawaamini hata maafisa Elimu wake walioko ndani ya mkoa, kwa kuendekeza ubabe huo huo mkoa wa Lindi haufanyi vizuri kielimu.Huyu apewe kazi ya usimamizi wa Elimu kama uafisa elimu tu ukuu wa mkoa umemshinda.

3. Zainab Telack - RC Shinyanga. Huyu naye hapishani na Zambi.Yeye hukazania zaidi Elimu ila kwa njia zisizofaa,ni mabavu mwanzo mwisho matokeo yake mara zote huharibu, anashindwa kujifunza approach za kiuongozi kutoka kwa jirani yake RC wa Simiyu Mtaka,kingine hupenda sana kufanyia kazi taarifa za majungu.Nasikia huyu alikuwa mwalimu arudi kufundisha tusilalamike tu kuwa shule zetu hazina walimu kumbe kuna walimu wameteuliwa kushika kazi zilizo juu ya uwezo wao kama Zainab Telack alivyo.

4. Gelasius Byakanwa - RC Mtwara. Huyu ni mbabe na ana kauli za kejeli. Ana mambo mengi na hana utulivu kabisa. Leo atasema hili kesho like na dharau kibao kwa wananchi ikitokea kaulizwa swali. Wananchi waheshimiwe maana wananchi ndio Wenye nchi na yeye yuko pale kuwatumikia. Huyu hafai.

5. Chalamila- RC Mbeya.
Huyu ni msikivu kwa wananchi ila ubabe ni mwingi sana,ameuweza mkoa wa Mbeya aonywe aendelee na kazi,asipojirekebisha apigwe chini.

6. Ally Hapi - RC Iringa. Ni kijana ambaye akijirekebisha tabia zake za ajabu ajabu anaweza kufika mbali Tatizo lake ni dharau, kiburi na kujiona kwingi. Mama kasema hataki kufanya kazi na watu wanaopenda kuinua mabega, mi naona Hapi ni mmoja wao, huyu arudi kukitumikia chama tu kama Sanare hafai kuwa RC.

7. Dr Sengati- RC Tabora. Binafsi sioni hata analofanya hapo Tabora, huyu naye tatizo ubabe, mkoa unammiss Sana Aggrey Mwanri,huyu arudi tu UDOM akaendelee kufundisha Political science hafai uRC.

8. Mndeme -RC Ruvuma. Huyu naye tatizo ni ubabe uliopitiliza, huyu atakuja kuleta madhara baadaye.Nilishtuka Sana kumwona siku moja amefula balaa kama kifutu anayemsema Askofu Shoo, akitaka kumtwanga ngumi mtumishi mmoja nikajisemea moyoni huyu mtumishi naye akihamaki si pambano la ngumi linashuhudiwa na hapo ndio mtu kutolewa jicho, kung'olewa pua au meno, ni aibu kubwa kwa serikali.Watumushi wa umma sawa wanakosea lakini kuwavunjia heshima tena mbele za watu haikubaliki hata kidogo. Huyu mama hafai kuwa RC, siku moja anaweza akaleta maafa kama take ya akina Dr Kleruu na mwenzake Ditopile mwaba wa Mzuzuri.Apigwe chini haraka huyo ni liability.

Unaweza kuongezea katika hii orodha
 
Kati ya hao wote hapo, naomba namba 5 apewe kipaumbele! Huyo jamaa amepata tu bahati ya kusoma, ila kichwani ni majanga matupu. Kwenye UDC pia Ole Sabaya nae apewe kipaumbele cha kupumzishwa.
 
Hao mimi naona afadhali, mnafiki ambae anatakiwa kutumbuliwa kwanza kabisa ni John Mongela mkuu wa mkoa wa mwanza. Huyu na katibu wake Matia Levi ni watu waliodhulumu haki za wananchi kwa muda mrefu. Walishatetea mwanajeshi aliyeua mtu ndani ya ofisi ya kata na wao wakasema uongo amepigwa na wananchi. Hawafai hata kidogo.
 
Kati ya hao wote hapo, naomba namba 5 apewe kipaumbele! Huyo jamaa amepata tu bahati ya kusoma, ila kichwani ni majanga matupu. Kwenye UDC pia Ole Sabaya nae apewe kipaumbele cha kupumzishwa.
Hivi unasema kweli kwamba namba 5 kasoma? Basi kama kasoma naomba nimnukuu Faiza " hivi huko shuleni mnakwenda kusoma ujinga". Huyo ni mmojawao.
 
Kuna mmoja mwingine simsemi kwa nia mbaya wala kwa chuki.

Ni mawazo yangu tu

Ila muda umefika vijana nao wachape kazi.

Benedict Mahenge-Rc Dodoma

Huyu mzee amejawa sana na busara + hekima pia hapendi show off za makamera.

Naona sasa Itapendeza akapumzike na wajukuu nyumbani,vijana waendelee kuchapa kazi na kulisogeza taifa.
 
Hivi unasema kweli kwamba namba 5 kasoma? Basi kama kasoma naomba nimnukuu Faiza " hivi huko shuleni mnakwenda kusoma ujinga". Huyo ni mmojawao.
Alikuwa eti ni Assistant Lecturer katika chuo kikuu kimoja pale Iringa mjini! Kuna wakati huyu Rais wa sasa alitoa tamko la wananchi kutokufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji ili kuzuia uharibifu wa wa mazingira na vyanzo vya maji.

Basi kauli ile ilileta mtafaruku mkubwa kwa watu wa Mkoa wa Iringa na Njombe kutokana na ukweli kwamba, wao hutegemea zaidi maeneo oevu ya mabonde (VINYUNGU) kulima mazao ya mbogamboga na yale ya chakula!

Hapa ndipo nilipo muona huyu jamaa ni kiazi! Wakati Wabunge na Wanaharakati mbalimbali wakipaza sauti zao ili wenyeji wa mikoa hiyo kuendelea kulima kwenye Vinyungu vyao maana vilikuwepo tangu enzi za mababu, huyu jamaa kwa sababu ni mtaalamu wa kutunga nyimbo za Kihehe, eti akatunga wimbo wa kuwashauri Wahehe wenzake (Anatokea Wilaya ya Mufindi huyu) wasilime kwenye Vinyungu!

Yaani badala ya kutunga wimbo wa kuwatetea wananchi wenzake, au kutoa elimu kwa Serikali kuhusu umuhimu wa Vinyungu kwa wananchi wa maeneo hayo, yeye akaona bora ajipendekeze kwa Serikali! Yaani hadi Mbunge Deo Sanga alimzidi akili kwa kuwatetea wananchi kwa ujasiri mkubwa kule Bungeni!

Ila mwisho wa siku, lile zoezi lilisitishwa! Na ule wimbo wake wa kinafiki ukabakia tu kama kiburudisho kwa Wanyalukolo wenzake. Kifupi ni mnafiki na mchumia tumbo wa kiwango cha juu sanq.
 
Kati ya hao wote hapo, naomba namba 5 apewe kipaumbele! Huyo jamaa amepata tu bahati ya kusoma, ila kichwani ni majanga matupu. Kwenye UDC pia Ole Sabaya nae apewe kipaumbele cha kupumzishwa.
Mimi kujua kwamba Godfrey Zambi ndo RC wa Lindi nimekumbushwa Leo.
 
Alikuwa eti ni Assistant Lecturer katika chuo kikuu kimoja pale Iringa mjini! Kuna wakati huyu Rais wa sasa alitoa tamko la wananchi kutokufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji ili kuzuia uharibifu wa wa mazingira na vyanzo vya maji.

Basi kauli ile ilileta mtafaruku mkubwa kwa watu wa Mkoa wa Iringa na Njombe kutokana na ukweli kwamba, wao hutegemea zaidi maeneo oevu ya mabonde (VINYUNGU) kulima mazao ya mbogamboga na yale ya chakula!

Hapa ndipo nilipo muona huyu jamaa ni kiazi! Wakati Wabunge na Wanaharakati mbalimbali wakipaza sauti zao ili wenyeji wa mikoa hiyo kuendelea kulima kwenye Vinyungu vyao maana vilikuwepo tangu enzi za mababu, huyu jamaa kwa sababu ni mtaalamu wa kutunga nyimbo za Kihehe, eti akatunga wimbo wa kuwashauri Wahehe wenzake (Anatokea Wilaya ya Mufindi huyu) wasilime kwenye Vinyungu!

Yaani badala ya kutunga wimbo wa kuwatetea wananchi wenzake, au kutoa elimu kwa Serikali kuhusu umuhimu wa Vinyungu kwa wananchi wa maeneo hayo, yeye akaona bora ajipendekeze kwa Serikali! Yaani hadi Mbunge Deo Sanga alimzidi akili kwa kuwatetea wananchi kwa ujasiri mkubwa kule Bungeni!

Ila mwisho wa siku, lile zoezi lilisitishwa! Na ule wimbo wake wa kinafiki ukabakia tu kama kiburudisho kwa Wanyalukolo wenzake. Kifupi ni mnafiki na mchumia tumbo wa kiwango cha juu sanq.
Asante Sana, sasa ndo nimemuelewa kabisa huyu msomi. Yaani hata Mbunge Deo Sanga alimzidi kwa akili na reasoning capacity? Hadi sasa bado tunamshangaa jinsi alivyoweza kuwasiliana na mgonjwa mahututi wakati ule! Ama kweli Mungu hamfichi mnafiki.
 
Back
Top Bottom