Nitasimama na SIMBA yangu daima

Nitasimama na SIMBA yangu daima

Nilijitambua kuwa mimi ni SIMBA mwaka 1982, almost miaka 41 hivi iliyopita.. Ni shabiki kindakindaki wa SIMBA sports club .. Mimi si shabiki maandazi
SIMBA ni timu kubwa sana Tanzania, Afrika na duniani kote.. Simba imekuwa role model kwa timu nyingi kwa mengi mazuri iliyoyafanya.. Ina mafanikio mengi kitaifa na kimataifa. Inaheshimika na kutambulika sana kuliko hata mpinzani wetu.. Ni mojawapo ya timu maarufu popote uendapo
Kwa sifa zote hizo
Kwa mafanikio yote hayo
Kwa ukongwe wote huo
Kwa umaarufu wote huo.. Nitaanzaje kuichukia timu yangu hii kwa changamoto ndogo ndogo za kupita?

Kwenye maisha kuna kupata na kuna kukosa
Kuna nyakati za mafanikio na kuna nyakati za maanguko
Kuna nyakati za furaha na kuna nyakati za huzuni pia

SIMBA tunapitia kipindi kigumu lakini si kama maadui zetu wanavyoaminisha watu mitandaoni.. Ni changamoto za muda hazitakuwepo milele.. Ni nyakati za nzige.. Tunazitafakari...hatukati tamaa tunapambana tutazishinda na kuwa imara zaidi.. Washindi zaidi wakubwa zaidi na zaidi

Soka lina matokeo matatu
Kushinda
Kushindwa
Kutoa suluhu
Kwasasa sisi ni washindwa wa muda.. Tunaachia nafasi za furaha kwa wengine wanaokua.. Ni muhimu kufanya hivi pia.. Huwezi kuwa mshindi daima .. Maisha yana pande mbili nasi kwasasa tuko upande wa pili

Acha kwasasa adui afurahi lakini hili nalo litapita kama mengine yote yalivyopita
Viva SIMBA.... Viva Forever.[emoji173]View attachment 2525426
Simba imebaki jina tu sasa. Inaserereka kinyumenyume kama liverpool. Tutegemee simba kushika nafasi ya mwisho bila kufunga bao caf cl group stage. Na nbc premier league mtaambulia nafasi ya 5
 
Simba imebaki jina tu sasa. Inaserereka kinyumenyume kama liverpool. Tutegemee simba kushika nafasi ya mwisho bila kufunga bao caf cl group stage. Na nbc premier league mtaambulia nafasi ya 5
Dua za kuku hizi
 
Kufungwa mechi mbili tatu tu, tayari mshachanganyikiwa....

Ushabiki wa hizi timu kongwe ni kama utumwa vile...
 
Simba nzee haiwezi kuwinda, hukamata na kula senene.
4082ec9fdbbc104084fbf249bfc53a20.jpg
 
Kufungwa mechi mbili tatu tu, tayari mshachanganyikiwa....

Ushabiki wa hizi timu kongwe ni kama utumwa vile...
Sio kuchanganyikiwa ni kutiana moyo na kuwaonesha maadui vile tulivyo imara.. Hata mtoto nyumbani akifeli humtukani bali unamtia moyo.. Labda hili uwaambie wale wa upande wa pili wanaoona huu ndio mwisho wa SIMBA
 
Simba imebaki jina tu sasa. Inaserereka kinyumenyume kama liverpool. Tutegemee simba kushika nafasi ya mwisho bila kufunga bao caf cl group stage. Na nbc premier league mtaambulia nafasi ya 5
20230221_145245.jpg
 
Maneno yako yamekurudia, chunga mdomo unapo tamkia wengine mabaya usisahau karma is really
Nadhani hata tafsiri halisi ya karma hujui na namna karma inavyofanya kazi katika uhalisia wake! SIMBA kamwe haitakuwa vile mnavyoomba iwe mark these words!
 
Nadhani hata tafsiri halisi ya karma hujui na namna karma inavyofanya kazi katika uhalisia wake! SIMBA kamwe haitakuwa vile mnavyoomba iwe mark these words!
Haitakua mara ngapi? hapo hakuna timu, ulijifanya mtabiri mara Jezi ya Yanga nzito haya twambie nyie wenye jezi nyepesi mnaendeleaje?
 
Haitakua mara ngapi? hapo hakuna timu, ulijifanya mtabiri mara Jezi ya Yanga nzito haya twambie nyie wenye jezi nyepesi mnaendeleaje?
Hapa ndipo kiwango chako cha ufahamu kilipofikia, pole sana kumbe hata ile mada hukuielewa kabisa na ikakuumiza kwa namna ya ajabu mno ! Kwahiyo kwa akili yako unadhani yanga itabaki hapo ilipo siku zote? [emoji23] kuifunga Mazembe ndio umeona mko vizuri sana?
Kasome hiki kitabu kitakusaidia mengi
b4bddb65803198b5f70908582af4f9fa.jpg
 
Broo kuna mvurugano wa viongozi pale klabuni,kuna watu wasaliti pale...inshu ya ule uchaguzi imeibua madudu mengi sana! Kuna watu wamesusa.
 
Sio kuchanganyikiwa ni kutiana moyo na kuwaonesha maadui vile tulivyo imara.. Hata mtoto nyumbani akifeli humtukani bali unamtia moyo.. Labda hili uwaambie wale wa upande wa pili wanaoona huu ndio mwisho wa SIMBA

Mpira pesa na mipango...

Ukiona jahazi linaenda mrama ujue kimojawapo au vyote hapo havipo sawa...
 
Back
Top Bottom