Naunga mkono hoja. Ifikie wakati hiki kikundi kinachojiita ccm, kiwekwe kando ili kipate wasaa mzuri wa kujitafakari. Kwa sasa kimejichokea na kinaiendesha hii nchi kijanja janja tu kupitia porojo na propaganda zilizopitwa na wakati.
Haiwezekani kampeni za mwaka huu ziwategemee wasanii tu ili kuwavutia wasikilizaji. Mgombea wao hana jipya, kila siku stori zake ni zile zile! Elimu bure, sijui kuongeza ndege!!
Cha kufurahisha zaidi, tangu nianze kuzifuatilia hotuba zake, sikumbuki kama kuna siku aliwahi kuwaongelea watumishi wa umma na wale wahitimu wa vyuo anao wasotesha mtaani bila ajira kwa miaka yote hii mitano.