Nitawasiliana na wanasheria wa jf

kanewi

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
298
Reaction score
200
mtoto wa rafiki yangu mwenye umri wa miaka sita ameangukiwa na geti la shule anayosoma na kuvunjika mguu,geti la shule linaonekana limeoza wakati wanatoka nje kurudi nyumbani ile kufungua geti likachomoka kwenye na kumvunja mguu.walimu wakampigia simu mzazi kumtaarifu jamaa akawahi pale na kumpeleka mtoto hospitari moi ambapo mpaka sasa anapata matibabu baada ya kuvunjika mguu wa kushoto,vipimo vya x-ray vilionyesha hivyo.mtoto anamaumivu makari sana na mzazi anamtibia bila ya msaada toka shule,.jamaa anataka kujua sheria zinasemaje baada ya mtoto wake kupona??naomba mnisaidie nikamshauri.,
 
Mpeleke mahakamani na udai gharama za matibabu na gharama nyinginezo. Sheria ipo. Inaitwa sheria ya madhara au Torts. Ukienda kwa wakili atakupa maelezo ya ziada.
 
Huyo jamaa yako ni lazy affair ndio maana hata mtoto wake kampeleka kwenye shule iliyooza.

Mwimbie aje yeye mwenye kuuliza, kwanini anakutuma wewe?
 
huyo jamaa yako ni lazy affair ndio maana hata mtoto wake kampeleka kwenye shule iliyooza.

Mwimbie aje yeye mwenye kuuliza, kwanini anakutuma wewe?
sio hivo ndugu yangu uhai wa mtoto kwanza madai baadae ,utafuatilia utazungushw utaishia mtoto kukatw mguu ndugu yangu!!!
 
sio hivo ndugu yangu uhai wa mtoto kwanza madai baadae ,utafuatilia utazungushw utaishia mtoto kukatw mguu ndugu yangu!!!

Kwahiyo yeye anachotaka ni kupatiwa pesa za matibabu au kuwajibishwa kwa walioacha geti lililooza bila kulitoa?

Bado siajelewa uhusino wa kuzungushwa na mguu kukatwa.
 
Kwahiyo yeye anachotaka ni kupatiwa pesa za matibabu au kuwajibishwa kwa walioacha geti lililooza bila kulitoa?

Bado siajelewa uhusino wa kuzungushwa na mguu kukatwa.[
 
Mpeleke mahakamani na udai gharama za matibabu na gharama nyinginezo. Sheria ipo. Inaitwa sheria ya madhara au Torts. Ukienda kwa wakili atakupa maelezo ya ziada.

Yap, hapo kuna principle inaitwa OCCUPIER 'S LIABILITY, the school has a duty to ensure safety of all people around its premises, so jamaa anaeza kufungua kesi ya tort au dahawa kwa kiswahili dhidi ya wahusika wa shule
 
Reactions: EMT
 
Atafute mwanasheria amshauri kitaalam nini cha kufanya.

Mpaka mtoto kuangukiwa na geti la shule ni kitu serious.
 
Mzazi huyu alikuwa sahihi kwanza kushughulikia afya ya mtoto...kesi za TORT zina span ya Limitation Period ya miezi sita toka mtu alipodhurika ...Hivyo iwapo mzazi atataka pesa ni wajibu wa shule kumlipa fidia timilifu kwa uzembe wao wa kushindwa kuchukua tahadhari na kwa mujibu wa sheria (torts) Inawajibika Kulipa gharama zote alizoingia kwa kumtibia mtoto,gharama za maumivu na madhara ya kimwili aliyopata pamoja na usumbufu wa Kisaikolojia awasiliane na mwanasheria kwa hakika atalipwa.Tukumbuke nia ya sheria hii ya Tort is there to compensate not for retribution kama sheria nyingine za Jinai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…