mtoto wa rafiki yangu mwenye umri wa miaka sita ameangukiwa na geti la shule anayosoma na kuvunjika mguu,geti la shule linaonekana limeoza wakati wanatoka nje kurudi nyumbani ile kufungua geti likachomoka kwenye na kumvunja mguu.walimu wakampigia simu mzazi kumtaarifu jamaa akawahi pale na kumpeleka mtoto hospitari moi ambapo mpaka sasa anapata matibabu baada ya kuvunjika mguu wa kushoto,vipimo vya x-ray vilionyesha hivyo.mtoto anamaumivu makari sana na mzazi anamtibia bila ya msaada toka shule,.jamaa anataka kujua sheria zinasemaje baada ya mtoto wake kupona??naomba mnisaidie nikamshauri.,