Nitaweza kujenga nyumba?

Nitaweza kujenga nyumba?

nimechafukwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
288
Reaction score
230
Nina uwezo wa kusave 600.000 kila mwezi nko mkoani Arusha bado sina kiwanja ni mfanyabiashara mdogo.

Je, nitaweza kujenga ka self contain na kununua kiwanja kwa hiyo saving au najidanganya?
 
Usikate tamaa katika maisha weka malengo yako tu utafanikiwa.
 
Nina uwezo wa kusave 600.000 kila mwezi nko mkoani Arusha bdo sina kiwanja ni mfanyabiashara mdogo je ntaweza kujenga ka self contain na kununua kiwanja kwa hyo saving au najidanganya??
Pesa nyingi sana hiyo kama unajipanga nayo. . . . .weka target zako huku ukitafuta kiwanja taratibu ili ujue bei ukishapata kiwanja then unaanza taratibu. . . .Laki sita ina maana ukinunua tofali kwa 1100/= unatofali 540 za inch tano sasa unakuwa unawekeza pesa kwa mfyatuaji zikifika za kutosha nyumba yako unapeleka site then unaandaa material kama kokoto lori moja na mchanga kama tripu tano hivi huku unashughulikia ramani na kibali cha ujenzi ukivipata waweza vuta pumzi ya cement na ujira wa fundi. . . .

Itachukua muda ila inawezekana ukiamua
 
Kwa uhakika wa hicho kipato unaweza ukakopesheka kwenye vikundi vya kuweka na kukopa na ukaweza kununua kiwanja.., ukajipanga vyema na kuanza kujenga. Sikushauri uzikusanye ukisubiria ziwe nyingi ndio uanze ujenzi bali tumia kama kianzio kupata mkopo n.k.

Ila kwa Arusha inakubidi ujipange haswa maana ujenzi ni ghali sana kuanzia ardhi, building materials na wakati mwingine hata ufundi!

Kila la kheri.
 
Hiyo laki Sita unayosave ni bora uongeze msingi wako na kutanua mtaji na kupata super profits...usizike hela kijana.
 
Kaka hio ni pesa ndefu sana ushauri wangu ukianza ku save tu anza kuulizia viwanja mkuu na nyumba ikiwa haijamalizika ila inaweza kukalika hamia utaimalizia kidogo kidogo kaka.
 
Back
Top Bottom