Nitazidi kuongea hata kama mkiniita tapeli

Duh najuta kuzembea kuzichanga BTC manake tangu January nina 0.421 BTC tu kwenye wallet .....niliacha baada ya kutapeliwa mara mbili...ngoja niingie tena ulingoni kupitia Masternodes
 
Tuchukulie mfano kukawa na rush watu wengi wakawekeza huko. Unadhani nini kitatokea mkuu??
Watu wengi wa Tanzania? Au unaongelea duniani??

Kwenye financial markets watu wakiwa wengi kwenye soko ndo efficient inaongezeka in terms of liquidity.

Ndo itakuwa vizuri kwa soko endapo kama watu wengi wakiwa wawekezaji
 
Duh najuta kuzembea kuzichanga BTC manake tangu January nina 0.421 BTC tu kwenye wallet .....niliacha baada ya kutapeliwa mara mbili...ngoja niingie tena ulingoni kupitia Masternodes
Tumia credible exchange.. na usije kumuamini mtu ukampa pesa zako.. hii naisema wazi..
 
hizi mambo nazielewa ndiyo maana naelewa nini wazungumza. kuna kuwork hard na kuwork smart
Mara nyingi kwenye cryptos.. watu wanangalia zile coins ambazo zina support activity ambayo ipo potential kwa jamii..

Ndo mana utakuta watu wanakuambia Etherium ina potential kubwa kuliko hata Bitcoin
 
Watu wengi wa Tanzania? Au unaongelea duniani??

Kwenye financial markets watu wakiwa wengi kwenye soko ndo efficient inaongezeka in terms of liquidity.

Ndo itakuwa vizuri kwa soko endapo kama watu wengi wakiwa wawekezaji
Duniani nasema kama hivi unavyotangaza na au upepo wa ufahamu wa teknolojia na vitu kama hvyo ukabadilika

Dunia nzima ikawa macho ni huko watu wakazinunua kwa wingi bitcoin leo hii sawa liquidity itaongezeka

Unadhani thamani yake itakua hapo hapo kwenye mil53 za madafu? Itapanda? Itashuka kidogo?? Itashuka sana?
 
Either way.. price ina move popote. Itategemea na demand na supply..
 
Unaongea bla bla nyingi..

Wapo nimesema mimi natoa training? Unanilisha vitu vingi ambavyo sijaviongea, hapo unakuwa hunitendei haki

Kwa kukusaidia tu elimu.. financial markets inatoa financing kwenye sekta zote unazozifahamu dunia hii.

Ufanisi wa financial markets maana yake ni ufanisi wa sekta nyingine zote. Mfano tu mdogo, biashara au kampuni, ikitaka kupata mikopo au mitaji zinajeukia kwenye financial markets kwa ku list equities au debt securities.

Viwanda vinategemea sana financial markets, raw materials zinazotumika viwandani ni commodities ambazo bei zake zipo decided kwenye financial markets..

Nakushangaa sana unaposhindwa kuona kama financial markets ndo key sector kwenye uchumi wa nchi yoyote including hizo unazoziita wewe ni 'real business' ..

Nakushangaa zaidi, unavotumia kutoelewa kwako financial markets kama standard ya maisha kwa watu wengine.. kwamba kwasababu kitu hukielewi vema basi ni matapeli..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…