Nitoe tahadhari kwa mnaotaka kununua simu za Sony Xperia Z1, Ni bei rahisi kamera kali ila utajuta kwenye Network.

Nitoe tahadhari kwa mnaotaka kununua simu za Sony Xperia Z1, Ni bei rahisi kamera kali ila utajuta kwenye Network.

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Ni kwa toleo lile lilioandika nyuma Docomo kutoka Japan - SO-O1K.

niliwahi kununua simu hii yani kamera ni kali, ram si 4gb, battery inachaji fasta na inakaa, simu ngumu, n.k ila kwenye network sasa!!

ukiwa mjini centre utaiona simu iko poa kabisa inashika 4g+ ni ngumu kujua kuna tatizo kwenye mtandao.

Yani kiufupi unaweza kutumia 4g ukiwa eneo lenye 4g+ hasa centre tu, nje ya hapo sahau

Kuwa makini, chukua tahadhari.

Binafsi nilishaiuza kwa mwengine ila yaye uzuri anakaa town kwenye 4g+
 
Ukiweka line ya 4g au ukitumia wifi inakuwaje?!
 
Ukiweka line ya 4g au ukitumia wifi inakuwaje?!
ukiweka line ya 4g hadi uwe sehemu yenye 4g+, bila hivyo huambulii kitu.

Kwenye wifi inakamat vizuri tu ia uwe eneo lenye wifi
 
Labda sio zote ni hiyo ya kwako ilikuwa na hiyo hitilafu.Vipi umeuliza wengine wenye simu kama yako? Wenye changamoto hiyo?.
 
Sio mjuzi sana ila Nimewahi na ninaendelea kutumia unlocked phones.

Mitandao yote hapa kwetu wameweka frequency bands za 4g, 3g na 2g kwenye website zao, ni vyema kuzipitia na kufahamu.

Mfano kwa mtandao wa Tigo.
tiGO provides its 2G (GSM) services on 900/1800 MHz, 3G signals on 2100 MHz, and 4G signals on 800 MHz frequency bands.

Kabla hujanunua simu unapaswa uangalie simu yako inaweza kukupa access ya 4g, 3g na 2g kwa frequency bands zipi? Na zina uwiana na za mitandao yetu??

Sorry kama ntakuwa nimetoka nje ya ulichomaanisha.
 
Kwanza kama unataka refurbished ya Sony kwa 250,000/= ni heri ukanunue Sony Xperia XZ2
 
Back
Top Bottom