Nitumie mbinu gani kupambana na hii UTI?

Nitumie mbinu gani kupambana na hii UTI?

functional

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2018
Posts
738
Reaction score
792
Jamani ndugu zangu habari za muda huu?

Hivi ni mimi tu au na nyie ndugu zangu kila nikipata demu lazima aniachie UTI, yaan imeshakuwa kero sasa dawa zenyewe zinadunda tu.

Nitumie mbinu gani wapendwa?
 
Jamani ndugu zangu habari za muda huu?

Hivi ni mimi tu au na nyie ndugu zangu kila nikipata demu lazima aniachie UTI, yaan imeshakuwa kero sasa dawa zenyewe zinadunda tu.

Nitumie mbinu gani wapendwa?
"Hivi ni mimi tu au na nyie ndugu zangu kila nikipata demu lazima aniachie UTI, yaan imeshakuwa kero sasa dawa zenyewe zinadunda tu."

Ni wewe tu mkuu wengine hawapati.N wewe unapata kwakuwa haujipendi.Unaloweka kavukavu😳😳
 
Jamani ndugu zangu habari za muda huu?

Hivi ni mimi tu au na nyie ndugu zangu kila nikipata demu lazima aniachie UTI, yaan imeshakuwa kero sasa dawa zenyewe zinadunda tu.

Nitumie mbinu gani wapendwa?
🌳 UGONJWA WA U.T.I NA DALILI ZAKE 🌳
⚡Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) husababishwa na vimelea kitaalamu hujulikana E. Coli.
⚡Vimelea hawa wakiingia kwenye njia ya mkojo huleta maambukizi na kusababishwa ugonjwa wa UTI.
⚡Kutokana na sababu za kimaumbile, Wanawake huathirika zaidi na ugonjwa wa UTI kuliko wanamume, hii ni kwa kwasababu kuna ukaribu zaidi katika njia hizi mbili za haja kubwa na mkojo. Na pale mtu anaponawa baada ya haja kubwa ni rahisi zaidi kuhamisha vimelea hivi vya E. Coli kwenye njia ya mkojo pale ambapo hujifuta kuelekea mbele. Na ndiyo sababu, kwa wanawake, hushauriwa kunawa kuanzia mbele kuja nyuma.
wa.me/255656303019
Endapo utanawa kuanzia nyuma kuja mbele, kuna uwezekano wa kuhamisha vimelea hivi ambavyo husambaa hadi kwenye kibofu, na endapo hautotibiwa vyema, basi hupanda hadi kwenye figo.

⚡Pia, Wanawake huathiriwa sana na UTI kwa sababu wana njia nyembamba ya mirija ya mkojo (urethra) ambayo, inawapa bakteria wa UTI urahisi wa kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo.
⚡Kujamiiana pia kunaweza kupelekea kupata bakteria wanaosababisha UTI.

🌿 DALILI ZA UTI 🌿
👉Maumivu wakati wa haja ndogo, na hisia ya mkojo kuchoma choma
👉Kubanwa na mkojo mara kwa mara
👉Maumivu ya kiuno na maumivu ya chini ya kitovu
👉Mkojo wa njano sana, na muda mwingine unatoa harufu
👉Uchovu
👉Homa
👉Kichefuchefu na kutapika
Kuna baadhi ya watu hawawi na dalili yoyote (asymptomatic bacteriuria)
wa.me/255656303019

⚡Unapohisi dalili hizi ni vyema kwenda kwa daktari ili upate tiba muafaka badala ya kuanza kutumia madawa bila ya mpangilio maalumu kitu kitakachoweza kukusababishia kukomaza ugonjwa. Pia, kuna baadhi ya dalili za UTI hufanana na zile za magonjwa ya zinaa (chlamydia, gonorrhea, and trichomoniasis), hivyo, vipimo vya maabara huitajika kuweza kutambua kama unachoumwa ni UTI au ni magonjwa ya zinaa (STD)

🌿 JINSI YA KUJIKINGA NA UTI 🌿
👉Kunywa maji mengi
👉Baada ya haja kubwa ni vizuri kunawa kuanzia mbele kurudi nyuma
👉Pendelea kwenda kukojoa pindi unapojisikia umeshikwa na mkojo. Na hakikisha umetoa mkojo wote.
👉Hakikisha sehemu za siri zipo safi kabla ya kujamiia
👉Ni vizuri kupata haja ndogo mara baada ya kujamiana ili kusafisha bakteria ambao wanaweza kuwepo kwenye njia ya mkojo,
wa.me/255656303019
👉Tumia juisi ya Cranberry ina vitu kitaalamu Vitamins and antioxidants ambavyo husaidia kuzia (siyo kutibu) maambukizi haya.
👉Hakikisha sehemu za siri zipo kavu, pendelea kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba, pia zenye kuacha unafasi (loose-fitting), epuka jinsi zinazobana au nguo za ndani za unailoni kwa sababu zitapelekea kuwa na hali ya unyevunyevu na kuleta mazingira rafiki kwa ukuaji wa bakteria.

Kwa ushauri na tiba wasiliana nasi
What's app / call
+255656303019
~Chief Sang'ida
 
Back
Top Bottom