Nitumie usafiri gani kusafirisha mizigo yangu kutoka Dar - Dodoma?

DOCTOR UZI

Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
99
Reaction score
79
Wakuu za muda huu,

Moja kwa moja kwenye mada au swali , mm ni mwanachuo nasoma Dom ila naishi dar kuna baadhi ya vitu nataka nivipeleke kwenye geto langu la dom (kitanda 5*6,tv ,fridge)

Sasa wakuu nilikuwa nataka kujua kama kuna usafirishaji mwengine ukitoa wa bus maana hawataki kusafirisha vyote kwa pamoja uchukue kimoja uache viwili na mm nataka vyote niende navyo au vipakiwe kwa pamoja.

Nitumie njia gani au usafiri gani wakuu wangu?
 
Pakia kwenye bus hata mbili. Alafu ulitakiwa kusafiri mapema.
 
Tumia gari za mizigo. Tembelea ofisi zao nyingi zipo kariakoo.
 
Nenda ofisini. Namaanisha kwenye ofisi kamili ya Shabiby. Usipokelewe na vibaka pale watakudanganya kwamba wao ni maanjent wa Shabiby. Hakikisha unakatiwa receipt yenye nembo za Shabiby. Pale vitapokelewa na kusafirishwa katika mabasi yao na utavipokea vyote ofisini kwao.
 
Tumia Boda boda boxer 100 mkuu dk 0 vitu vyako vinafika Dom.
 
Yani wasomi wa siku hizi. Mmekaa kizembe kweli. Hivi huwezi amka apo na kufatilia upate usafiri mpaka kila kitu utafniwe?
UKIGOOGLE BEI YA KITU MTANDAONI BADALA YA KWENDA SEHEMU HUSIKA KUILIZIA KWAKO NI UZEMBE?
 
Unapajua Jangwani mkuu? Fika pale na vitu vyako kuna Fuso za kutosha watakupakilia mizigo yako yote na ndani ya masaa 24 vitakuwa viko East Zoo!
 
Tumia Treni mkuu, sababu bei yake ni nafuu wala haito zidi 20,000 kwa vyote hivyo. Pia ni salama sana kwasababu havitapata mitikisiko.
Maana tren inapaa angani!
 
Kama unatokea Ubungo kuelekea Kimara shuka kituo kinaitwa Rombo au Kibo ulizia mitaa ile,nakumbuka kulikuwa na malori yanayopakia vitu kwenda mikoani...
 
Jf sikuizi inaboa...badala ya kujibu kila mtu anatafuta attention
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…