Nitumie vigezo gani kununua pikipiki used

Nitumie vigezo gani kununua pikipiki used

Adolph Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
5,950
Reaction score
9,511
Jamani nimetafakari kuhusu biashara zangu nikaona bila kuwa na usafiri wangu binafsi nitaendelea kuteseka mno kwa kudandia dandia za watu.

Nimeamua kutafuta usafiri wangu binafsi kutoka kwa mtu (watu) yaani used nimepata tatu zote tvs.

Moja namba D sikusoma speedometer ya pili namba C speedometer inasoma 176340 ya tatu namba C ila speedometer wameng'oa.

Sina uzoefu na vyombo vya moto hata baiskeli sina wazoefu na vifaa hivyo msaada nimiliki fukuza upepo.

Pia siyo tatizo nikifahamu hatua za umiliki au kubadili umiliki kuwa jina langu...karibuni Great thinkers
 
Zingatia yafuatayo.

1. Namba sio kigezo Cha kununua pikipiki inaweza namba C ikawa Bora kuliko namba D inategemeana na mtumiaji, service na mahali.

2. Ikiwa zote zipo sawa basi namba D ni Bora kuliko C .

3. Kamwe usilete kujuana kwenye kununua pikipiki inaweza kuwa ya wizi.

4. Fuata taratibu zote za manunuzi ya pikipiki maana za wizi ni nyingi kuliko halali.

5. Kamwe usinunue pikipiki iliyokuwa bodaboda labla zile za mikataba.
 
Asante sana ila naomba kufahamu hatua za kununua pikipiki used ikiwemo na taarifa za pikipiki hiyo nazipataje?
 
Asante sana ila naomba kufahamu hatua za kununua pikipiki used ikiwemo na taarifa za pikipiki hiyo nazipataje?
Taarifa unazipata kwenye kadi, kama anaeuza nae alinunua kwa mtu ( kwenye kadi sio jina lake ) akupe mkataba wa mauziano na kama hana hiyo pikipiki achana nayo.

Pikipiki unanunua kwa mkataba wa mauziano na kupewa kadi. Pia kwenda TRA kubadilisha umiliki ( hapa utalipia kodi 10% ya bei na elfu 20 ya kubadili umiliki.) Hapa umemaliza.
 
Kama anaeuza sasa hakubadilisha umiliki mwanzoni endapo kama nae alinunua kwa mtu, mlolongo wake ni mrefu kidogo maana TRA watataka Kodi yao ya mwanzo kwanza ndio ifuate hiyo ya pili.

NDIO MAANA PIKIPIKI NYINGI WATU WANAUZIANA KIENYEJI TU UKIPATA MSALA BASI AJALI KAZINI.
 
Asante, hapa naona la maana ni kwenda TRA na kadi ya pikipiki kwanza kuhakiki au kuna njia ya mtandao?
 
Kama anaeuza sasa hakubadilisha umiliki mwanzoni endapo kama nae alinunua kwa mtu, mlolongo wake ni mrefu kidogo maana TRA watataka Kodi yao ya mwanzo kwanza ndio ifuate hiyo ya pili.

NDIO MAANA PIKIPIKI NYINGI WATU WANAUZIANA KIENYEJI TU UKIPATA MSALA BASI AJALI KAZINI.
Daah kumbe iko hivyo?

Basi itabidi na picha yake iwepo kwenye kadi ya mauziano
 
Jichange nenda kanunue mpya dukani, polee najua hali ngumu ya kimaisha na labda hauna pesa ya kununua dukani, jichange kanunue dukani au kama vipi? Nenda kachukue zilee za mkopo na lipa kiasi ulichonacho na piga nao mahesabu kiasi kilichobaki ulipe taratibu taratibu mpaka umalize deni

Zipo za wizi watu wanafoji mpaka kadi.. watakupeleka jela bila matarajio yako

Bongo mtu akitaka kuuza kitu lazima kiwe na kasoro kubwa eiza kibovu au ameiba pahala ndio ule msemo unaosema uswahilini ukikuta mtu anakula kuku eidha kuku mgonjwa au mgonjwa anayekula kuku.. kwaheri
 
Jamani nimetafakari kuhusu biashara zangu nikaona bila kuwa na usafiri wangu binafsi nitaendelea kuteseka mno kwa kudandia dandia za watu.

Nimeamua kutafuta usafiri wangu binafsi kutoka kwa mtu (watu) yaani used nimepata tatu zote tvs.

Moja namba D sikusoma speedometer ya pili namba C speedometer inasoma 176340 ya tatu namba C ila speedometer wameng'oa.

Sina uzoefu na vyombo vya moto hata baiskeli sina wazoefu na vifaa hivyo msaada nimiliki fukuza upepo.

Pia siyo tatizo nikifahamu hatua za umiliki au kubadili umiliki kuwa jina langu...karibuni Great thinkers
kua mstahimilivu,
Ongeza bidii ya kazi, jichange ununue mpya tyuuuu acha kujitaftia matatixo kwenye shida au tamaa ya kumiliki bodaboda yako 🐒
 
Sikushauri kununua pikipiki used vifaa vingi vinakuwa vimeshachoka ila vimejishikiza tu utaitumia hata miezi 6 mambo shwari siku ukienda kufungua engine utajuta
 
Sikushauri kununua pikipiki used vifaa vingi vinakuwa vimeshachoka ila vimejishikiza tu utaitumia hata miezi 6 mambo shwari siku ukienda kufungua engine utajuta

Mbona mimi nimenunua pikipiki used iko vizuri sana
 
Pia zingatia chasis no ya kwenye kadi na iliyopo kwenye chombo pamoja na Engine no ya kwenye kadi na iliyopo kwenye chombo. Wengi wanafodge kadi hivyo ikiwa tofauti achana nauo kabsa.
 
Ndugu mtoa mada nikwambie tu kwamba huyo fundi anayesifia kila pikipiki eti mashine achana nae.

Kwanza pikipiki nzima huna haja ya kuhangaika na fundi maaha changamoto ndogondogo ni kawaida, cha msingi angalia;

INJINI
~kwanza sikiliza mlio wa engine. Ingine isiyo na shida inarun smooth haina kelele haigongigongi ndani hata asiyefundi ataweza tofautisha nzima na mbovu.

~hakikisha engine haivujishi oil, hapa kuwa makini na aliyeosha pikipiki ili akuoneshe.

~angalia bolts za kwenye engine zisiwe zimefunguliwa mara kwa mara, zilizofunguliwa mara kwa mara vichwa vyake vinakuwa na injury

~hakikisha haitoi moshi, weka kidole kwenye bomba la exhaust, unatakiwa kupata rangi nyeusi kavu isiyo na mchanganyiko wa oil.

CHASIS
~angalia chasis isiwe imechomelewa, isiwe na kutu sana, isiwe na sehemu zilizopinda.

USUKANI
~usukani uliopinda ama tenki lililobonyea huashiria ajali, epuka hiyo.

SHOCK UP ZA MBELE
hakikisha hazijapinda na hazivujishi oil

HALI YA VIFAA VINGINE
angalia hali ya vifaa vingine kwa macho vitasema utunzwaji wa pikipiki ulikuwaje, mf. dashboard kama hiyo iliyong'olewa inaashilia hata utunzwaji wa pikipiki sio mzuri achana nayo.

Lakini niseme pia plate namba sio kigezo. namba C inaweza kuwa imetunzwa kuliko hata D. Hapa hata jicho tu linaweza ona baadhi ya ishara.

Kwa upande wa TVS kama ni cc150 achana nazo maana zina changamoto nyingi sana, TVS cc125 ni stahimilivi sana na imara pia.

Kama walivosema wadau hapo juu, kwanza angalia aliyekuwa anaitumia kwa mishe mishe zake binafsi na sio bodaboda. mfano hiyo namba C inayosona 176,000 Km ni wazi hiyo ni bodaboda.

Kingine ukipata mwenye nyaraka halali basi sawa, japo kwa upande wa pikipiki ni wachache sana hufanya transfer ya majina wengi hubaki na majina ya kampuni kwenye kadi.

Kila la kheri.
 
Pia zingatia chasis no ya kwenye kadi na iliyopo kwenye chombo pamoja na Engine no ya kwenye kadi na iliyopo kwenye chombo. Wengi wanafodge kadi hivyo ikiwa tofauti achana nauo kabsa.
Hiyo chasis no ipo upande gani wa tvs ili nilinganishe?
 
Back
Top Bottom