Ndugu mtoa mada nikwambie tu kwamba huyo fundi anayesifia kila pikipiki eti mashine achana nae.
Kwanza pikipiki nzima huna haja ya kuhangaika na fundi maaha changamoto ndogondogo ni kawaida, cha msingi angalia;
INJINI
~kwanza sikiliza mlio wa engine. Ingine isiyo na shida inarun smooth haina kelele haigongigongi ndani hata asiyefundi ataweza tofautisha nzima na mbovu.
~hakikisha engine haivujishi oil, hapa kuwa makini na aliyeosha pikipiki ili akuoneshe.
~angalia bolts za kwenye engine zisiwe zimefunguliwa mara kwa mara, zilizofunguliwa mara kwa mara vichwa vyake vinakuwa na injury
~hakikisha haitoi moshi, weka kidole kwenye bomba la exhaust, unatakiwa kupata rangi nyeusi kavu isiyo na mchanganyiko wa oil.
CHASIS
~angalia chasis isiwe imechomelewa, isiwe na kutu sana, isiwe na sehemu zilizopinda.
USUKANI
~usukani uliopinda ama tenki lililobonyea huashiria ajali, epuka hiyo.
SHOCK UP ZA MBELE
hakikisha hazijapinda na hazivujishi oil
HALI YA VIFAA VINGINE
angalia hali ya vifaa vingine kwa macho vitasema utunzwaji wa pikipiki ulikuwaje, mf. dashboard kama hiyo iliyong'olewa inaashilia hata utunzwaji wa pikipiki sio mzuri achana nayo.
Lakini niseme pia plate namba sio kigezo. namba C inaweza kuwa imetunzwa kuliko hata D. Hapa hata jicho tu linaweza ona baadhi ya ishara.
Kwa upande wa TVS kama ni cc150 achana nazo maana zina changamoto nyingi sana, TVS cc125 ni stahimilivi sana na imara pia.
Kama walivosema wadau hapo juu, kwanza angalia aliyekuwa anaitumia kwa mishe mishe zake binafsi na sio bodaboda. mfano hiyo namba C inayosona 176,000 Km ni wazi hiyo ni bodaboda.
Kingine ukipata mwenye nyaraka halali basi sawa, japo kwa upande wa pikipiki ni wachache sana hufanya transfer ya majina wengi hubaki na majina ya kampuni kwenye kadi.
Kila la kheri.