Hii post imefanya moyo wangu usisimke sana kwa kuona mtu anavyokuja kupata madhara na asijue yametokana na nini. Carotone??? WEKA MBALI NA NGOZI YAKO!!!
Carotone (pamoja na michanganyiko yake) sio kipodozi salama na huweza kusababisha madhara yafuatayo:
Madhara hayo ni pamoja na:
- Ugonjwa wa saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na kibofu cha mkojo
- Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo
- Magonjwa ya moyo na kutopumua vizuri
- Kutokwa na chunusi kubwa kubwa
- Ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele
- Ngozi kuwa nyembamba sana na laini hivyo kupata michubuko na majeraha kwa urahisi
- Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi
- Kichefuchefu, kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu
- Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu (hasa kichwani)
- Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na waliopo tumboni
- Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi
- Kuchubuka kwa ngozi
- Ngozi kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali
- Upofu, uziwi na upotevu wa fahamu wa mara kwa mara
- Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
Matokeo mabaya hayaji haraka haraka, ila wakati unakuja kuyaona unakuwa tayari umeshachelewa. Acha kabisa Carotone na vipodozi vyote visivyo salama (Ukipenda orodha kamili ya vipodozi visivyo salama, madhara yake na ushauri zaidi omba na utatumiwa bure kabisa kwa email. Tuma meseji kwenda namba 0719326693 kuomba).
Carotone, Caro light, Maxi tone, Extra Clair, Perfect White, Express White, Rico, Jaribu nk vyote ni vibaya na ni miongoni mwa zaidi ya vipodozi 200 ambavyo utavikuta kwenye hiyo email
- AFYA ZAIDI CONSULTANTS