Niulize chochote kuhusiana na biashara ya duka la jumla

Niulize chochote kuhusiana na biashara ya duka la jumla

JF inabidi wajipange kwenye constructive thread kama hii moderators wasaidie kuhakikisha masuala yote muhimu yanayohusiana na biashara hii yameulizwa na kupatiwa majibu au laa wametafuta experienced people ktk biashara hii na wametupa insights
Naomba nieleweke kuwa simaanishi Moderators waingilie mijadala yetu, Laa ninachomaanisha waje humu walete maswali ambayo yana changamoto tuulizane na tupatiane majibu
Kwa mfano kuna suala la Profitability ya hii biashara ikoje ?
Ili ufanikiwe kwenye biashara hii ni vigezo gani vinahitajika ?
Kuna changamoto gani ?

Na kadhaalika na kadhaalika
 
JF inabidi wajipange kwenye constructive thread kama hii moderators wasaidie kuhakikisha masuala yote muhimu yanayohusiana na biashara hii yameulizwa na kupatiwa majibu au laa wametafuta experienced people ktk biashara hii na wametupa insights
Naomba nieleweke kuwa simaanishi Moderators waingilie mijadala yetu, Laa ninachomaanisha waje humu walete maswali ambayo yana changamoto tuulizane na tupatiane majibu
Kwa mfano kuna suala la Profitability ya hii biashara ikoje ?
Ili ufanikiwe kwenye biashara hii ni vigezo gani vinahitajika ?
Kuna changamoto gani ?

Na kadhaalika na kadhaalika
Hakika Kuna nyuzi zipo huko ni za maana Sana ila nashangaa hazipewi majibu yaliyokamilika.
 
Tuufufue huu uzi,ukifufuka nashusha nondo,hakika ni biashara nzuri lkn uwe mvumilivu hii ndo sifa sio unaulizia Friday na changamoto tu,mtu anaeuliza faida na hesabu za karatasi hatoboi.

Mtu anaefanya
 
NOMBA ELIMU WADAU, NATAKA KUANZISHA DUKA LA JUMLA BUNJU B MABWEPANDE NA SIJUI PA KUANZIA!
 
Moja kwa moja twende kwenye mada

Kama unamalemgo yakufua biashara ya duka hii jumla achana na haya maduka ya mtaania ya Mangi nazungumzia biashara ya jumla mfano pipi, Tambi, Unga, Mafuta,sabuni,nk...

Karibu nipo tayari kushare my experience yangu kwenye hii biashara nayafahamu mengi zaidi na zaidi kwenye hi biashara...

Bidhaa nyingi zinapatikana kwenye viwanda ndipo wanapo nunua hawa matajiri nakuweka kwenye maduka yao ya Jumla

Almost asilimia 98% zinazalishwa hapa hapa Nchini.

Unga wa sembe,unga wa ngano Mfuta yakupikia, Pempers, Sabuni Soft aina zote, chumvi, biscuits, Tomato,majani ya chai,madaftari Aina zote marapa sabauni za unga Aina zote vibiriti nk...

Chamsingi nikuangalia bidhaa zipi utaanza nazo kutokana na mataji wako.

Mkuu naomba namba yako nipate elimu kwako!
 
Mimi mpaka saivi nimeshapata frem na nimelipia kabisa nishaweka mashelfu nishanunua Freezer na mzani pia.
Nina mtaji wa 1.5M nataka niidondoshe apo dukani. Nahitaji mawazo yenu wakuuu. Location chanika mwisho.
 
Ukweli ni kwamba nimejifunza nkivyotaka kuvifahamu. Mimi nilifanya biashara ya jumla ila ilikua vinywaji (juice za viwabdani, energy, maji). Changamoto za hapa na pale ikiwemo za kifamilia zikaingilia Kati nikastop. Ila nataka kurudi Tena kwa location ya Dar this time.

Nikizungumzia biashara ya vinywaji nlivyotaja faida yake ni ndogo mmno. Katoni ya juice ama energy unakuta unapata 300/- or 400/- kifupi yahitaji mzunguko haswa. Nikawaza wakati Bado nafanya hiyo biashara, ya kuwa hapa Kuna haha kubwa sana ya kuongezwa na bidhaa zingine tajwa kwenye huu uzi (pipi, sabuni, unga, bublish nk nk) Ili kufikia malengo binafsi.

Kuhusu records, siku hizi Kuna software nyingi zingine mpk za kulipia pesa kdg kwa mwezi, unaweka taharifa zako vizuri za dukani na mpaka report ya mauzo kwa weekend, mwezi unapata plus stock unapata alert kuwa mzigo upo chini ya idadi fulani inategemea na ulivyoset. Uzi nimeuoenda sana, nna swali dogo la ufahamu ikiwa umeweka kijana wa kusaidia kwenye mauzo kiasi gani haswa pendekozo la malipo ya kumpa.

Biashara hii ya jumla inaniwazisha Kila uchwao jinsi nnavyoipenda. Nimejifunza mambo mengi kupitia wafanya biashara fulani wakubwa pale Moro mjini nikiona wanavyo operate imenipa uzoefu wa awali nikijumlisha na nkivyokua nauza vinywaji + limebaki jambo moja TU.
Mungu atasimamia hili
 
Wakati nauza vinjwayji nlibahatika kupata frem pahala pengine mkoa huo huo nkawa nauza mayai jumla. Jirani yangu alikua na duka la jumla "Ngosha" kupitia namna alivyo ipelekea biashara yake kwa kweli alikua ana ni inspire sana.
1. Ana Fanya delivery kuanzia saa 12 asbh licha ya boda zingine kuja kufuata mzigo wenyewe anafunga duka saa moja usiku.
2. Ana frem ndogo TU ila ana stoo kubwa ya kushusha semi hata 3 (shikamoo Ngosha).
3. Dukani anakaa mkewe na yeye na ndugu yake wa karibu. Na ana vijana wa kazi yapata watatu wengine.
4. Msosi wa wote unasongwa ugali wa pamoja na vijana wake wanaishi nyumba iyo iyo moja upande wa vymba vya nje.
5. Kwa jinsi alivyo na wateja wengi baadhi ya waleta bidhaa mfano sigars wanamuchia mzigo na kufuata hela wkt mwingine na baadhi wengine.
6. Ana mini canter yake moja ya kupeleka mzigo kwenye duka lake la jumla location ingine.
7. Ana simu design ya land line ipo busy kupokea order aasbh mpk jioni, na order zinapalekwa na boda maalumu ndio kazi yake kuu. Nadhani Kuna umbali fulani ana chaj.

Nilichokiona kwa haraka haraka ni Bado wa kutumia madaftari kwenye kuweka hesabu. Unajua Ina cost muda sana especially unapaotaka pata tathmini fulani ya mauzo ya Muda fulani. Ukiwa na software hata Ile dashboard inakuletwa zile taharifa za awali bidhaa gani imeuzika sana na ipi inasinzia bila kutumia nguvu nyingi. Na unaweza access hata ukiwa haupo dukani as long as uliowaacha wanaingiza Kila mauzo.

Kifupi Kuna la kujifunza kwa Kila mtu.
 
Hivi hawa watu wenye biashara hii wanapitia njia gani kutajirika maana kutwa naona wanasumbuliwa na TRA
 
Back
Top Bottom