manumba malecha
Member
- Apr 25, 2020
- 43
- 27
Moshi mweusi mkuuMoshi wa namna gani: mweupe au mweusi?
Nadhani air filter yako imachefuka au imeanza kuziba kwa hiyo haipitishi hewa ya kutosha kuchoma mafuta yote; angalia air filter kwanza unipe mrejesho kabla sijafikiria kukupeleka kwingine. Kwa vile unasema ukishachanganya pedeli basi moshi unakwisha, inaonyesha kuwa inabidi ufungue njia ya hewa iwe kubwa sana ndipo injini yake iaweze kuchoma mafuta yote. Ukikaa nyuma ya exhaust wakati inaotoa moshi huo unaweza kusikia harufu ya mafutaMoshi mweusi mkuu
Kwanza huo siyo uendeshaji mzuri wa gari; utauwa transmission yako sasa hivi. Huwezi kubadili gear ya automatic transmission ukiwa una accelerate. Kwanza kwa nini ubadili gia; ukishaweka D ianache yenyewe ijiendeshe; hata ukitaka kusimama wewe kanyaga breki tu, transmission itajipanga hadi kusimama. Usifanye hiyo kama manual ya kubadili badili gear; nakuhakikishaia kuwa katika miaka 25 iliyopita nadhani kama nimewahi kuendeshea L au 1 ni kipindi kidogo sana; huzihitaji sana hizo position labda uwe kwenye foleni za ajabu sana, ambako pia ina maana hutakanyaga accelerator kiasi hicho. Siku zote D, R na P zinakutosha sanaPia kuna sababu gani ambayo Kwa gari za automatic ukikanyaga accelerator ikiwa katika mwendo halafu ukabadili gear badala ya kubadili inawasha taa ya overdrive kwenye dashboard ambapo hupeleka kuzima Kwa gari
Ahsante Sana mkuuKwanza huo siyo uendeshaji mzuri wa gari; utauwa transmission yako sasa hivi. Huwezi kubadili gear ya automatic transmission ukiwa una accelerate. Kwanza kwa nini ubadili gia; ukishaweka D ianache yenyewe ijiendeshe; hata ukitaka kusimama wewe kanyaga breki tu, transmission itajipanga hadi kusimama. Usifanye hiyo kama manual ya kubadili badili gear; nakuhakikishaia kuwa katika miaka 25 iliyopita nadhani kama nimewahi kuendeshea L au 1 ni kipindi kidogo sana; huzihitaji sana hizo position labda uwe kwenye foleni za ajabu sana, ambako pia ina maana hutakanyaga accelerator kiasi hicho. Siku zote D, R na P zinakutosha sana
Kula mafuta kunasababishwa na vitu vingi sana; ukipitiapitia humu utaona nimeshawahi kuvirodhesha. Sababu mojawapo na kubwa ni hiyo ya air cleaner kuwa chafu. Zipo nyingine ndogo ndogo ambazo baadhi zinahusiana na njia ya hewa pia; kwa mfano manifold airflow sensor na manifold Pressure sensor kuwa hazifanyi kazi; oxygen sensors kuwa zimekufa, kutumia oil chafu sana au oil nzito sana kama SAE40 au SAE50. Kutumia matairi yasiyokuwa na upepo mzuri; kuwa na breki ambazo zimejam na kadhalika. Pata fundi akukagulie vyote hivyoNa je Kwa gari aina ya nissani tidiida Kula mafuta Sana tatizo ni nini? Engine ni he 15cc1450 na inakilomeer 110,000
Mkuu hapo kwenye SAE ndio nimeona kunashida kwani ninatumia SAE 40 ASA natakiwa nitumie SAE ngapi Kwa gari Hilo?Kula mafuta kunasababishwa na vitu vingi sana; ukipitiapitia humu utaona nimeshawahi kuvirodhesha. Sababu mojawapo na kubwa ni hiyo ya air cleaner kuwa chafu. Zipo nyingine ndogo ndogo ambazo baadhi zinahusiana na njia ya hewa pia; kwa mfano manifold airflow sensor na manifold Pressure sensor kuwa hazifanyi kazi; oxygen sensors kuwa zimekufa, kutumia oil chafu sana au oil nzito sana kama SAE40 au SAE50. Kutumia matairi yasiyokuwa na upepo mzuri; kuwa na breki ambazo zimejam na kadhalika. Pata fundi akukagulie vyote hivyo
Ahsante Sana mkuuSAE30 au 10W-30
hakuna madhara; hivyo ndivyo inavyotakiwa ifanye.Ila jaribu kusaficha cooling system yako hasa radiator kwani inawezekana imeziba sana kiasi kuwa unaona maji yanayorudi; kwa kawaida maji huwa yanarudi ila mtu huwezi kuyaona kwa haraka.Mkuu kichuguu gari likiwa linarudisha maji kwenye rezevu shida inakuwa ni nini? Na kipi chanzo chake? Na yapi madhara yake?
Mkuu Kichuguu kuna gari hapa aina ya Toyota vitz new model 2005 push to start inasumbua Sana,huwa inazima yenyewe wakati unatembea au kubadilisha gear kwenda reverse au drive.hakuna madhara; hivyo ndivyo inavyotakiwa ifanye.Ila jaribu kusaficha cooling system yako hasa radiator kwani inawezekana imeziba sana kiasi kuwa unaona maji yanayorudi; kwa kawaida maji huwa yanarudi ila mtu huwezi kuyaona kwa haraka.
Hizo brake pad unazofunga ni genuineWadau tatizo la break kuisha unapofunga zinakuwa hata miezi 6 haiishi zinakuwa zimeisha hili tatizo linasababishwa na nini?