Mkuu nina noah voxy engine 1az fse. Inakula mafuta sana na haina nguvu. Kwa kuwa mi ni mgeni wa magari mafundi wamekuwa wakipiga ramli na kuninunulisha vitu vingi vya gharama na shida imeendelea kuwepo.
Fundi wa kwanza aliniambia ni cylinderhead tukafungua engine nzima ikafanyiwa overhaul, kusaga valve na kuosha carbon. Shida ikaendelea kuwa vile vile ulaji wa mafuta, gari haina nguvu, na check engine light inawaka.
Fundi wa pili Nikabadilisha oxygen sensor pia, pump ya mafuta, fuel pressure pump(D4). Tatizo likaendelea vile vile.
Fundi wa tatu tukabadilisha fuel pump ya kwenye tank, fuel pressure pump(D4), Driver injector, Nozzles zote na bomba lake, MAF sensors lakini bado gari haina nguvu na ina misfiring na check engine light inawaka.
Jana nikaita fundi akaifanyia diagnosis na computer ikaleta code P0172 na Code P1349. Naomba msaada wa utatuzi wa tatizo langu. Nianzie wapi ?